Utabiri Wangu: Bingwa wa Ligi ya NBC 2023/24 ni Azam FC

Utabiri Wangu: Bingwa wa Ligi ya NBC 2023/24 ni Azam FC

Hili swala lipo kihisia zaidi. Ni mapema mno kuweza kutabiri.

Kwanza, hujajua uzito na ujazo wa vikosi husika. Usajili ndo kwanza unaanza. Azam haina hata kocha bado. Haijasajili bado mchezaji mpya.

Pili, Ligi yetu ya NBC wenye kuonyesha kiu ya kulitaka haswa ni wawili. Wanachukua kwa kupokezana, Lunyasi na Utopolo. Azam bado haijajijenga kuwa mtafuta Ubingwa.

Hata kama Azam atachukua, si kwa sababu uliona kiutaalam bali hisia zako zilikuongoza kuropoka.
Azam kocha wanae mbona
 
Hatakuwa bingwa kwa sababu
1. Atakuwa na kikosi kidogo
2. Bado kuna wasaliti na wababaishaji
3. Atapambana kujitutumua kimataifa amalize nguvu zake huko
4. Idaadi ya magoli na points walizomzidi Simba na Yanga ni kubwa
5. Kocha na benchi la ufundi ni jipya
6. Atafanyiwa fitna na ndugu wa kariakoo ambazo hajawi ona.
N.B: Ajikite na kupunguza gepu ili ajaribu 2024/2025
 
Sisi kazi yetu ni kuquote na panapo majaaliwa ya uzima na afya, tuurejelee huu uzi mwaka kesho...
Mwaka kesho mbali huko kote? tumpe tu mzunguko wa kwanza ukiisha aje atwambie hicho kitimu chake kipo nafac ya ngape!
 
Ina maana Simba ndo tusibebe kwa miaka 3?
 
Back
Top Bottom