Utabiri wangu mechi ya Simba na Yanga, tarehe 8 Machi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Nimechungulia anga la SIMBA kuna ung'avu mkubwa na nyota nne zinawaka kuzunguka kichwa cha mnyama SIMBA akiwa kakanyaga zulia jekundu na kuzingirwa na mataa yanayomeremeta, mekundu. Kwa upande wa YANGA kuna utusitusi na hali ya kufifia.

Huku vitu kama nyota vikiwa vimepoteza nuru. Kuna nyota mbili zinawaka na kufiifia kama umeme wa single phase wenye load iliyozidiwa pembezoni na chini kuna rangi ya khaki kama njano na ni kavu kama jangwani.

Chochote anachotaka kukifanya YANGA kwenye hiyo ndoto kinapata msaada na mwanga toka upande wa SIMBA.

Tafsiri yake ni ninini?
  • SIMBA atatawala mchezo mwanzo mwisho kasoro dakika chache tu za mwisho.
  • SIMBA itatoka kifua mbele kwa kulipenya lango la YANGA mara NNE.
  • Yanga watabahatika kupata kifuta machozi cha bao mbili au moja. Kama nia mbili, kila kipindi kitapata moja.
Kama huamini utabiri huu au unabisha njoo na wako lakini usiwe wa kufoji. Ama kaa tulia tusubiri kipenga cha mwisho tarehe hiyo ya 8.3.2020.

Jr[emoji769]
 
Mimi mfano ni yanga alafu nikutane na bango kama hili na kuangalia kwa makini aliyeweka uzi ni mtu anayesemwa kwa mengiiii hasa yale yanayoogopesha. Aneeeweeeeeiiiiiii hiyo tarehe ni siku ya wanawake nasikia dunianI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…