Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,313
- 4,751
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwa siasa za nchi yetu, upinzani wa kweli utaanzia na kutatokea (originate from) ndani ya CCM yenyewe na si vinginevyo.
Tulishuhudia Lyatonga Mrema alipomeguka ktoka ccm na kutua NCCR- Mageuzi mwaka 1995. CCM waliponea chupuchupu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo. NCCR Mageuzi kikawa chama kikuu cha upinzani.
Mwaka 2015 tukashudia Edward Lowasa alipomeguka kutoka CCM akiwa na vigogo wa CCM kama akina Ngombale Mwiru na kutua CHADEMA. Mwaka huo pia CCM iliponea chuchupu na chadema kikawa chama kikuu cha upinzani.
Inaelekea mwaka huu wa 2025 kutokea kitu kinachofanana na hicho. Humphrey Polepole wa kundi la Gen-Z kutua CHAUMA akiambatana na vigogo kama akina Warioba, Mpina, Gwajima, Mbowe, Mdee nk kutawabana sana pumzi hao CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ikizingatiwa ACT Wazalendo nao watakuwa wanawarushia mishale.
Nani aliwadanganya kwamba Tanzania haina upinzani? Tofauti yetu kubwa na wenzetu ni kuwa upinzani nchini kwetu ni wa ustarabu unaozingatia nguvu ya hoja na siyo matusi.