Utabiri: Yaliyotokea 2015 yakiongozwa na Lowasa yanaweza kutokea 2025 yakiongozwa na Polepole

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,313
Reaction score
4,751
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwa siasa za nchi yetu, upinzani wa kweli utaanzia na kutatokea (originate from) ndani ya CCM yenyewe na si vinginevyo.

Tulishuhudia Lyatonga Mrema alipomeguka ktoka ccm na kutua NCCR- Mageuzi mwaka 1995. CCM waliponea chupuchupu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo. NCCR Mageuzi kikawa chama kikuu cha upinzani.

Mwaka 2015 tukashudia Edward Lowasa alipomeguka kutoka CCM akiwa na vigogo wa CCM kama akina Ngombale Mwiru na kutua CHADEMA. Mwaka huo pia CCM iliponea chuchupu na chadema kikawa chama kikuu cha upinzani.

Inaelekea mwaka huu wa 2025 kutokea kitu kinachofanana na hicho. Humphrey Polepole wa kundi la Gen-Z kutua CHAUMA akiambatana na vigogo kama akina Warioba, Mpina, Gwajima, Mbowe, Mdee nk kutawabana sana pumzi hao CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ikizingatiwa ACT Wazalendo nao watakuwa wanawarushia mishale.

Nani aliwadanganya kwamba Tanzania haina upinzani? Tofauti yetu kubwa na wenzetu ni kuwa upinzani nchini kwetu ni wa ustarabu unaozingatia nguvu ya hoja na siyo matusi.
 
Kwani vinuua mgongo vya wabunge vimeshatoka?

Hakuna anayetaka kuanza kudai watoe pesa kwanza, kisha upepo uanze kuvuma tuone nani anapepea na nani ana stahimili dhoruba.
 
ccm ni dude kubwa mzee, yote yanayoendelea unaweza kuta ni part ya plan
 
Hahhaa Polepole kumbe ni Gen-Z. By the way upinzani hawajui kama wana cheleweshwa na hawa watu. Hii ni mipango ya kuvuka salama.
 
namuona polepole akiipeleka tanzania kusikojulikana niambieni anaipeleka nchi wapi
 
ccm ni dude kubwa mzee, yote yanayoendelea unaweza kuta ni part ya plan
Sidhani haya yaliyotokea mwaka 1995 ya Mrema na ya mwaka 2015 ya Lowasa yalikuwa part ya plan ya ccm. Haiwezekani ccm ikatengeneza plan ya kujiua yenyewe (suicide) kwa kujitia kitanzi shingoni na kujinyonga. Yaani kwenye hayo matukia ccm ilikuwa kidogo tu iiage dunia. Na zamu hii something similar may happen.

Hahhaa Polepole kumbe ni Gen-Z. By the way upinzani hawajui kama wana cheleweshwa na hawa watu. Hii ni mipango ya kuvuka salama.
Gen-Z maana yake ni Kizazi kipya, chenye umri usiozidi miaka 59. Ni kundi la binadamu wa sasa. Kizazi cha kale ni kile chenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea, ni kundi la binadamu wa kale.

Tundu Lissu ana umri wa miaka 57, Polepole miaka 55, Gwajima miaka 54, Mpina miaka 50, Mdee miaka 47. Hawa ni kizazi kipya na ni moto moto kweli kweli. Kizazi cha faster faster. Kizazi cha dot com!
 
ccm haiwezi kufa hio sahau, ndo chama kikubwa afrika
 
Wewe bwana ni muongo sana. Gen-Z ni kizazi cha 1997-2012. Hata hufanyi tafiti kidogo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…