Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
CAF inaona gharama kutumia VAR katika kila mechi, na imeona ni vyema kwa sasa timu zitakazoingia robo fainali ya Klabu za Afrika ndio ziwe zinacheza huku mitambo ya VAR ikiwa imefungwa. Sioni jitihada za Azam, Namungo, Singida BS kufikia ngazi ya robo fainali ya klabu za CAF.
Tayari Simba SC imeshakuwa klabu ya kwanza nchini kutumia VAR katika mechi zake. Klabu ya pili ikawa ni Simba Queens na ilifanikiwa kufika hadi nusu fainali.
Mchuano umebaki kutafuta klabu ya tatu. Naona walau Yanga itawashinda akina Azam, Namungo, Singida BS, Ihefu, Geita Gold nk katika kutafuta kuwa klabu ya tatu nchini. Lakini hawa wanaume wakizubaa, ipo JKT Queens inaweza ikawapiku.