Utabiri: Yanga itakuwa Klabu ya Tatu nchini kutumia VAR baada ya Simba SC na Simba Queens

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
CAF inaona gharama kutumia VAR katika kila mechi, na imeona ni vyema kwa sasa timu zitakazoingia robo fainali ya Klabu za Afrika ndio ziwe zinacheza huku mitambo ya VAR ikiwa imefungwa. Sioni jitihada za Azam, Namungo, Singida BS kufikia ngazi ya robo fainali ya klabu za CAF.

Tayari Simba SC imeshakuwa klabu ya kwanza nchini kutumia VAR katika mechi zake. Klabu ya pili ikawa ni Simba Queens na ilifanikiwa kufika hadi nusu fainali.

Mchuano umebaki kutafuta klabu ya tatu. Naona walau Yanga itawashinda akina Azam, Namungo, Singida BS, Ihefu, Geita Gold nk katika kutafuta kuwa klabu ya tatu nchini. Lakini hawa wanaume wakizubaa, ipo JKT Queens inaweza ikawapiku.
 
Mashabiki wa simba wengi wao wanapenda sana kujivunia hata yale mafanikio yasiyo na impact yoyote ile katika klabu yao.

Sasa ukiwauliza hiyo VAR, imewaletea impact gani kwenye timu yao! Sidhani kama watakuwa na majibu sahihi.

Haijashangaza hata kuona siku ile ya uchaguzi wao wakilipuka kwa shangwe, kumshangilia Caesar Manzoki, ambaye hakuwa na umuhimu wowote ule kwenye huo uchaguzi!!
 
Ungetabiri mapema kabisa timu ipi itakua ya kwanza kutumia VAR.

watu washatoa bikra alafu unamtabiria jamaa anaemfukuzia demu kua atakua watatu kumla manzi.
 
CAF inaona gharama kutumia VAR katika kila mechi, na imeona ni vyema kwa sasa timu zitakazoingia robo fainali ya Klabu za Afrika ndio ziwe zinacheza huku mitambo ya VAR ikiwa imefungwa...
Kwaiyo kutumia VAR nayo imekuwa mada ya kuleta hapa? Aya baada ya kutumia VAR umeleta kombe gani? Au baada ya kutumia VAR ukaacha kusajili kina kyombo na sawadogo? Ulipewa zawadi gani labda baada ya kutumia iyo VAR? Ujinga nao ni mzigo mkubwa sana kwa watanzania
 
Mi ni yAnGaaaa
 
Simba walitumia lini var!?..au niwaulize berkane!?
 
Rage aliona mbali kabisa..
 
VAR ndio inayotufanya tunashiriki Super league barani afrika na vigogo wenzetu 7 sisi tukiwa wawakilishi pekee wa ukanda huu kwakua pia ndio timu pekee ukanda huu kucheza mchezo wa kimashindano kukiwa na VAR
 
Yule Rage Mungu amuweke, ni mtu mwenye maono sana, hakukurupuka kuwaita mbumbumbuu
 
Mwaka huu wana makombe mengi sana imagine kombe la VAR tayari wanalo, Chama yupo kwenye timu ya wiki ya CAF, Inonga kuitwa timu ya Taifa, Barbara ni secretary huko CAF, Manzoki mjumbe wa mkutano mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…