Utaendaje Bar unaaagiza soda 4 unakunywa wakati wenzako wanakunywa bia,huu ni Ushamba

Utaendaje Bar unaaagiza soda 4 unakunywa wakati wenzako wanakunywa bia,huu ni Ushamba

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Nipo eneo fulani hapa nachakata kinywaji kiwe mkojo

Sasa Kuna wadau kama wanne wapo Meza ya Jirani ,halafu nahisi ni wasukuma hawa manake nipo kwako huku

Hiyo meza waliyokaa wadau ,watatu wanakunywa bia,huyu mwenzao wamemlundikia soda tatu Tena spalleta na chupa ya maji

Hivi mdau unakubalije kwenda bar wenzako wanakula gambe ,wanapiga maji ya dhahabu wewe umekomaa na misoda yako

Mimi nikiwa na rafiki mnywa soda siwezi kwenda nae Bar atanihaibisha na misoda yake

Yani mwanaume mzima umekaa na chupa tatu za soda Tena jamii ya Fanta unakunywa wakati wenzako wana maji ya dhahabu

Comeee on braza acha ushambaaa

Kula bia wewe.
tapatalk_1564163011686.jpeg
 
Nawewe unaendaje bar unaagiza beer wakati wengine wanakunywa Whiskey za 400K.
Kunywa unachopenda kutokana na pochi lako kiongozi
 
Ushamba ni hali ya kustaajabu jambo!

wewe unayemshangaa mwenzio anayekunywa soda 3 ndie mshamba!

by the way kwanini uingilie (why do you care about) life style ya mtu mwingine!

kila mtu anafanya kila anachokiamini yeye!

by the way "MIND YOUR OWN BUSINESS"
 
Bila Shaka hapo juu wote nyie ni wanywa soda mtakufa kwa kisukari walahi nawaambia
 
Jamaa kazingua..vipo vinywaji vinavyoendana na walevi,, angekua anakula zake balitka tu hapo mbona mambo yangekua fresh
 
Jamaa kazingua..vipo vinywaji vinavyoendana na walevi,, angekua anakula zake balitka tu hapo mbona mambo yangekua fresh
kwani baltika ina ladha tofauti na pombe, anaeweza kunywa baltika bhasi anaweza kunywa pombe. Labda ungesema bavaria au energy drink yoyote maana kwa muonekano huwa poa kuliko soda na kama ana guts anaweza tumia sweet wine
 
Back
Top Bottom