Utafanya nini endapo utagundua kuwa umeingia kwenye ndoa na mtu ambaye si sahihi?

😅😅😅hufikirii wazazi uliowasumbua
Aah wazazi majukumu yao yaliishia ukumbini yaliyobaki yote yapo mikononi mwangu.

Kuna wakati natamani kuwashauri watu wasitafute wake au waume kanisani kwa maana wengi kule hawako kwenye comfort zone zao ila naogopa kuzodolewa na ndugu zangu wa imani.
 
inahitaji ujasiri sana
 
Ndoa ndoano,, dunia nayo imebadirika wakuu na kila mtu hapa duniani ana vitu anavyo vitaka ifike mahali tupate vibali vya ndoa za mkataba mambo ya kuishi na mtu kwa vinyongo sio sawa kabisa.
_20240809_143242.JPG
 
inahitaji ujasiri sana
Yeah ila kiuhalisia haya mambo hayapaswi kwenda haraka, na mwanamke ambae unataka umuoe its better ukamfanya kuwa rafiki yako kwanza kabla hata hujamuonesha interest yoyote ya kumtaka hii itampa uhuru na uwazi wa kuishi kwenye uhalisia wake.

Hautaki tangaza nia mapema auigizie aje akulipue baada ya ndoa.

Nimebase upande wa wanaume coz swala la kuoa ni lawanaume ila future na uhai wa ndoa uko mikononi mwa mwanamke.
 
Katika utafiti mdogo nilioufanya nimegundua watu wengi waliingia kwenye ndoa bila kujuana vizuri kiundani.

Sasa baada ya kuingia kwenye ndoa ndipo Mke/Mume anagundua mapungufu Mengi kwa mwenzi wake ambayo hakuyajua kabla ya Ndoa.

Kama ilivyo ndoa za Kikristo zinasema hadi Kifo kiwatenganishe ndipo muachane pamoja na sababu nyinginezo.

Nimesoma Visa na mikasa kutoka kwa wanasaikolojia na wataalamu wengine wa kimahusiano Nimeona malalamiko mengi yaliyomo ndani ya Ndoa.

Malalamiko ya wanaume.
1.Mke hapendi ndugu zake.
2.Mke mvivu.
3.Mke sio Mwaminifu katika ndoa.
4.Mke Mchoyo.
5.Mke hamjali Mumewe.
6.Mke ana Mdomo na dharau.
7.Mke Mchawi.
8.Mke halei vizuri watoto.
9.Mke hataki kulea watoto wa nje wa Mumewe pamoja na mambo mengine kama hayo.

Malalamiko ya Wanawake kwa Wanaume.
1.Sio waaminifu.
2.walevi kupindukia na kuchelewa kurudi nyumbani.
3.Hawajali familia.
4.Hawashirikishi familia mambo yao.
5.Kusikiliza zaidi wazazi wao hasa Mama.

Na mambo mengine kama hayo.

Lakini inaelezwa kuwa kabla ya hapo walikuwa vizuri na kuamua kuingia kwenye ndoa.

Kanisani mliapa mtakuwa pamoja kwenye shida na raha.Lakini baada ya kugundua hayo madhaifu mnaanza kuomba Talaka 😅 mlidhani ndoa ni nini?.

Hakunaga ndoa nyepesi, ndoa ni kitu kikubwa sana kinachobeba mambo mengi sana na ni safari ndefu.

Mwingine anashtuka anapoambiwa mkwe atakuja kuugulia hapa hadi apone. Anaanza kuzunguka zunguka kuomba ushauri.

Hiyo Ndio ndoa.

Sasa wewe ukikutana na utofauti huo utafanya nini?
Tatizo liko kwenye uchaguzi wa huyo mke/mume, vigezo siku hizi vinapuuzwa kinachoangaliwa ni uzuri wa nje, kama mwanamke ni presentable unabeba,ukijipa moyo mengine mtamalizana ndani, matokeo yake mnashindwa kumalizana mnakuja kulia nje, wanawake nao wamebaki na kigezo kimoja tu, Pesa Pesa Pesa, mwanaume akiwa na pesa kwa mwanamke hana kipingamizi, siku hizi wale wanawake wa "Sidanganyiki na pesa zako" hawapo tena, si unaona majina kama "Fataki" siku hizi hayapo. Sasa ukishaingia kwenye ndoa unagundua hafai pamoja na kuwa anapesa au ana shape(tako), unagundua kuwa umeyatimba
 
Huwa najilinganisha na jamaa yangu mmoja kaoa mke yuko rafu balaa nasema sijui nikipata mke wa vile sijui kama ntaweza kuishi nae

Nguo anatupatupa hovyo ukienda kwake nguo zimejaa kwenye kochi muda wote kukaa hadi muanze kusogeza nguo, kisu utakuta juu ya meza, sufuria chini , ye mwenyewe anahiyo khanga yake ameiteua ya kushindia nyumbani ni nyeupe ila hadi imebadilika rangi sijui haifui, daah ila kutana nae barabarani alivyojiremba sasa pini kinoma.

Mi mwanamke wa vile siwezani nae kwenye nyumba chafu hata kukaa huwa naona sina amani
 
Dah kipengele kwa kweli
 
😅😅😅
 
Hapo hakujua kabla huyo
 
Back
Top Bottom