Utafanya nini kuboresha mwonekano wako zaidi?

Utafanya nini kuboresha mwonekano wako zaidi?

lyzbeth

Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
40
Reaction score
8
Kuonekana mrembo na mdogo imekuwa ni jambo la msingi sana katika tamaduni nyingi sasa. Katika ulimwengu wa sasa, tunaguswa sana na picha nyingi vutivu za watu maarufu. Kwa Tanzania tunao baadhi ya hao watu maarufu wenye mionekano ya kirembo kama Madam Rita wa Bongo star search na Jackline Mengi aliyewahi kuwa Miss Tanzania.
Pale mtu anapokuwa na mwonekano mzuri huwa anajengeka kiakili na anapata ujasiri zaidi na kukubalika katika jamii, kwa sababu ya fikra walizonazo kwamba wanaonekana wanavutia kutokana na matarajio yao hivyo inawapa ujasiri wa kutosha zaidi. Mwonekano mzuri pia unaongeza wateja/mashabiki wengi katika fani za burudani. Watanzania wengi walio maarufu wanazidi kuwa na mvuto zaidi na kuongoza katika mambo ya urembo na ulimbwende.
Ongezeko la upasuaji kwa ajili ya urembo Tanzania ni dogo tofauti na nchi za nje, lakini bado ongezeko hili linakua hasa maeneo ya mijini. Kinachofurahisha ni kwamba nia ya kuwa mrembo sio tu kwa wanawake tena. Wanaume nao wanajikita kwenye usemi wa ?mwonekano wa kitoto? hasa wale wanaojihusisha sana na kazi za Sanaa na vyombo vya habari.
Hali hizo zimesababisha watu kufanya upasuaji ili wasizeeke na ratiba za kujipodoa zinazidi kushamiri siku hadi siku. Tunaona jinsi hospitali na kliniki za Tanzania zinavyoongezeka hasa kwenye kutoa taarifa za michakato ya urembo na vipodozi. Ingawa Tanzania bado inajitahidi kukimbizana na spidi ya njia za kisasa za urembo, tunaona jinsi watanzania wengi wanavyosafiri kwenda ughaibuni kwa ajili ya upasuaji.
Kwa mujibu wa Dk. Kuldeep Singh, mshauri mwandamizi wa upasuaji hospitali za Apollo, kuna hatua tofauti mtu anaweza kuchagua ili aonekani mrembo na mdogo pia. Kipodozi cha botox kinaweza kutumika kupunguza makunyanzi na utokwaji wa jasho. Utumiaji wa tishu laini kwenye ngozi kitaalam ni hatua mojawapo inayoweza kutumika kupunguza makunyanzi, kuboresha nyama za chini ya mashavu, kidevuni na puani pia.
Kuondolewa kwa nywele sehemu za usoni hasa kwa ajili ya matibabu ni njia iliyoshika kasi kwa watanzania, uzuri wa njia hii haihusishi kuondoa sehemu yoyote ya ngozi bali ni nywele tu, na haitoleta madhara na inaweza kupunguza nywele mara azote.
Kutokana na chaguzi tofauti za maisha kama kula vyakula vyenye kalories nyingi na upungufu wa kufanya mazoezi, ongezeko la vitambi limezidi kushamiri. Kwa mujibu wa takwimu za utafiti za idadi ya watu na afya au Tanzania demographic and health survey (TDHS) uliofanywa 2010 na taasisi ya takwimu Tanzania pamoja na ICF Macro walikuta kwamba 22% ya wanawake wa watanzania wana uzito mkubwa zaidi ya jinsi wanavyotakiwa kuwa. 15% wanauzito uliozidi na 6% wana vitambi. Kulingana na ongezeko la vitambi upasuaji wa kuondoa mafuta (liposuction) ni baadhi ya njia iliyopata umaarufu katika harakati za kupata umbo zuri. Uhitaji wa kupunguza mafuta pasipo upasuaji ni jambo litakalo endelea kusaidia kutengeneza mbadala wa teknolojia mpya. Dk. Rajkumar Palaniappan wa hospitali za Apollo zilizopo Chennai anasema upunguzwaji wa mafuta mwilini ni kitu cha kawaida kwa wote wenye tatizo la uzito mkubwa hasa kwa njia ya upasuaji au kula mlo sahihi. Watu hao wanabakiwa na ngozi iliyodhoofu, wakihitaji aina tofauti wa upasuaji kama wa sehemu ya mwili ya juu na chini.
Aina nyingine ya upasuaji ambayo inakuja kwa kasi ni hii ya kupandikiza nywele. Kutokana na matokeo mazuri yaliyoonekana hivi karibuni kwa kutumia njia zilizoboreshwa, wanaume wengi zaidi wanachagua huduma hii ili kuondoa vipara vinavyowafanya waonekane wazee.
Kuna faida nyingi za kufanya upasuaji wa urembo na pia pasipo kutumia upasuaji kwa viwango vizuri, taasisi zilizodhibitishwa kama hospitali za Apollo zimefungua kituo maalumu cha kutoa huduma za urembo huko New Delhi. Dr Kuldeep Singh aliongeza ?matibabu ya ngozi yanazoeleka sana siku hizi. Kila njia kama isipofanywa kwa umakini inakuwa ni hatari. Hivyo ni muhimu kuchagua njia iliyo salama, ya kuaminika na yenye matibabu bora kwa ujumla.
Pamoja na faida zote na manufaa ya upasuaji wa ngozi, yapo baadhi ya madhara. Kwa sababu hatua nyingi ni za muda mfupi, zinatakiwa zirudiwe mara kwa mara kwa kipindi maalumu cha muda, kwa mfano njia ya botox kwa wastani ya miezi 5, tishu inayowekwa kwenye ngozi ni kila mwaka 1 hadi 2, na zile hatua za kubana ngozi ni za kila miaka 2. Matumizi makubwa ya kuweka tishu kwenye ngozi yanaleta mwonekano feki licha inahusisha asidi ya hyaluronic ambayo inaisha nguvu baada ya muda. Watu wenye aleji na sindano ni vyema wachukue tahadhari. Kila sindano inaweza kuleta michirizi kwenye ngozi na itakuwa mbaya zaidi pale ngozi inapopata jua. Hatua za upasuaji zinaweza kuleta makovu ya muda mrefu kidogo na muda wa kupata nafuu nao kuongezeka, wengine wanaweza kufanya mara mbili wengine hapana.
Vijana wengi Tanzania wanaanza kutafuta hatua za utunzaji wa ngozi zao. Mbali na kuhakikisha mtu anahudumiwa na kliniki iliyothibitishwa, Dk. Kuldeep Singh anashauri pale inapotokea matibabu kwa rika la vijana, mawazo na maamuzi mengi lazima yaende kwenye maamuzi hasa ya upasuaji wa plastiki au njia zisizohusisha upasuaji. Sio kwamba upasuaji sio sahihi kwa vijana ila upo uwezekano mkubwa vijana kushindwa kuelewa madhara ya muda mfupi na mrefu watakayopitia. Ni muhimu kuwa matarajio yao yawe bayana na sio tu kushawishiwa na matangazo na marafiki. Dk. Singh anashauri utunzwaji mzuri wa ngozi, na kuondolewa kwa nywele hasa kwa vijana.
 

Attachments

  • 112.jpg
    112.jpg
    87.8 KB · Views: 137
mwonekano mzuri ni jinsi tu unavyojiweka mwenyewe ....vaa nguo znazoendana na mwili wako...ambazo znaficha sehemu za mwili wako usizozipenda wewe na kuangaza zle unazozipenda...hii yakupa confidence ambayo ni nzur kwa muonekano wako.. ukivaa accesories mfanoshanga, bangili na vitu kama hivyo usivae vingi sana .pia usafi wa mwili.. kama mtumiaji wa vipodozi..usitumie vingi sana na utumie vinavyoendana na rangi ya ngozi yako.. .kwa sura yenye ngozi laini...tengeneza mask ya mayai, asali na ndimu ila ngozi yako ikiona ndimu kali ucweke ndimu...iache usoni dakika kumi na tano au 20 af safisha uso...rudia mara moja kwa wiki ..au hata kwa mwezi...ila ukipaka af ngozi inawazsha jua imekukataa hvyo waweza kutumia njia zingine...na mazoezi
 
Back
Top Bottom