Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
UTAFANYAJE MKEO AU MUMEO AU MZAZI WAKO AKIWA NA MAMBO YA KISHIRIKINA? Hivi ÑDIVYO UTAKAVYOFAÑYA.
Anaandika, Robért Heriel
Mtibeli.
Mtu yeyote ambaye haamini nguvu za Mungu huyo ni mshirikina.
Mtu yeyote ambaye anaamini nusu kwa nusu ñguvu za Mungu huyo ni Mshirikina.
Inaweza ikatokea kwenye maisha yako moja ya Watu wako wa karibu wakawa wanajihusisha na mambo ya kichawi au ushirikina.
Yaweza kuwa ni Mumeo au mkeo au wazazi au wazazi wa mumeo au mkeo.
Ikitokea ukajua kuwa moja ya Watu wako wa karibu ni wachawi au washirikina iwe kwa wao kujionyesha waziwazi au kwa kificho.
Au wanakushauri mambo ya kishirikina au uchawi wakisema kuwa huenda mambo yako hayaendi sawasawa kwa sababu kuna vitu haujafanya. Na vitu hivyo ambavyo haujafanya wàkakuambia ni kwenda kwa waganga wa kienyeji, kwenda kufanya mambo ya kishirikina iwe ya kimila au kiutamaduni.
Ikiwa ni Baba au Mama ndiye anayekushauri mambo hayo jitenge naye. Wala usiwe karibu na yeye. Tena asije nyumbani kwako akakaa kwa muda mrefu asije akawafundisha familia yako elimu yake ya kipumbavu.
Nawe usiende kwa baba au mama yako ukakaa kwa siku nyingi zizidizo siku saba. Na mkeo asikae kwa wazazi wako ikiwa unajua ni washirikina na wanamawazo ya giza.
Na watoto wako wasikae kwa wazazi wako(Bibi na Babu zao) ambao ni washirikina na wachawi.
Watakapokuuliza kwa nini unafanya hayo. Waambie ni kwa sababu wao ni washirikina na wachawi ndio maana unafanya hayo.
Kwa sababu mshirikina hana elimu nyingine ya kumpa mwanao wala binti yako au mkeo zaidi ya kumpotosha.
Ikiwa mkweo ni mshirikina au mchawi usiruhusu wanao wakakae huko. Wala wao wasijekukaa hapo kwenu kwa muda mrefu usiozidi siku saba.
Elewa, mzazi wako anaweza kumpotosha mkeo na kumfundisha mambo ya kishirikina.
Anaweza kumfundisha kwenda kwa waganga ili wakudhibiti wewe au kukupa sumu ambazo hawazijui wao wenyewe.
Hakuna mafanikio ya maana yanayotokana na ushirikina na uchawi. Ni akheri uwe maskini na wakuone hauna muelekeo kuliko kufuata njia zao.
Ni akheri ufe kuliko kupata msaada wowote, nasisitiza wowote kutoka kwenye uchawi na ushirikina.
Waambie wewe hutaki mafanikio kutoka kwenye uchawi na ushirikina.
Waambie wao wakifanikiwa kwa njia hiyo inatosha. Wafanikiwe wao kwa mambo hayo na sio wewe.
Ikiwa mkeo au mumeo anamambo ya kishirikina au kichawi vunja hiyo ndoa na familia siku hiyohiyo usisubiri. Wala usiweke mjadala wa kumbadilisha.
Kabla hujaoa wala kuolewa, hakikisha unamwambia mwenza wako kuwa siku utakayojihusisha na ushirikina na uchawi ndio siku ambayo mahusiano haya yatafika mwisho na hakutakuwa na mjadala na hakuna atakayesikilizwa.
Ikiwa mtoto wako ulimfundisha kutojihusisha na mambo ya ushirikina au uchawi lakini kwa hiyari yake akakaidi na kufuata maamuzi yake. Waeleze Ndio siku hiyohiyo hautakuwa mzazi wao, hautakuwa Baba yao, hautakuwa Mama yao.
Wasitajwe kwa jina lako. Na wala usiwape urithi wowote ule.
Na wala wasije ukajihisi vibaya kuona wengine watakuwa wamefanikiwa na hawategemei urithi au chochote cha kuwapa.
Wasije nyumbani kwako wala wewe usiende kwao.
Usichukue chochote kutoka kwao wala wao wasichukue chochote kutoka kwako.
Kwa maana waliamua kukudharau na kukaidi.
Hivyo ndivyo Watibeli walivyo.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam