Uko zako uraiani na ushamaliza mihangaiko yako ya kila siku...!!unaangalia taarifa ya khabari unaona rafiki yako, mfano classmate wako wa sekondari, anaonekana ktk TV akitafutwa na Polisi kama mhalifu sugu na mwenye mtandao mkubwa hadi polisi.. na zawadi nono kwa atakayefanikisha kukamatwa kwake!!
Siku chache, unakutana nae uso kwa uso ukiwa mihangaikoni... anakusabahi..anaonekana ni mtu mstaarabu na mwenye hela... mnabadilishana mawili matatu ila wewe huna amani naye anaonekana hana amani na wewe...!!
utamuuliza kuhusu habari zake ktk tv...utamsalimisha polisi(kumbuka kuna zawadi nono nawe umifulia)?!:A S 39:
Jiulize yafuatayo;
1. Wewe unaweza kuathirika kwa uhalifu huo kwa namna yoyote?
2. Je, zawadi nono hiyo kweli ipo? Na kama ipo, inatosha kuwa suluhisho la kufulia kwako?
3. Urafiki wenu utaathiri vipi maisha, jamii na nchi yako?
Lakini utambue yafuatayo pia;
1. Ni mtu anayekufahamu pengine hadi nyumbani...!
2. Anao mtandao mkubwa sana polisi, ukimripoti huenda umejipeleka kwake...!
3. Pia ni mtu ambaye tayari hana amani nawe, hivyo amekwisha tambua utofauti kati yenu...!
Cha kufanya;
1. Kaa kimya, na kamwe usizungumze naye kuhusu tuhuma hizo.
2. Kaa mbali naye na umkwepe kuongozana naye kabisa.
3. Kama utaripoti polisi, angalia usipelekwe na tamaa za zawadi nono, tembelea vituo mbalimbali na utumbukize maandishi yako kwenye masanduku ya maoni, then ishia zako kimyakimya. Wasipolifanyia kazi basi wewe umetimiza wajibu wako. Vinginevyo, kaa kimya na umuombe mungu akulinda na akuweke mbali naye...!