Utafiti: Asilimia 10 ya Watanzania wana Kisukari

Utafiti: Asilimia 10 ya Watanzania wana Kisukari

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Dk. Omary Ubuguyu amebainisha kuwa kati ya Watanzania milioni 60, zaidi ya milioni 5.7 (takribani asilimia 10) wanusumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.

Aliyasema hayo jijini Dodoma katika uzinduzi wa mpango wa kuzuia ulemavu wa kutoona unaoweza kusababishwa na madhara ya kisukari kwenye macho.

"Tanzania inakadiriwa kuwa na takribani asilimia 5.7 ya watu wenye umri wa miaka kati ya 20 na 79 wana Kisukari. Utafiti uliofanyika nchini unaonesha asilimia 35 ya wenye Kisukari wana madhara ya ugonjwa huo kwenye macho na asilimia moja yao, hupata ugonjwa wa kutoona au kuona hafifu amesema.

Aidha, ameeleza kuwa kuna taratibu nyingi za kuzuia ulemavu wa kutoona unaosababishwa na kisukari kwenye retina ikiwa ni pamoja na kuanza uchunguzi mapema kwa walio na kisukari pamoja na kuzingatia tiba na ushauri wa wataalamu ikiwemo kubadili mtindo wa maisha.

Source: Swahili
 
Tufanyeje kujizuia?
Tuwe na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara, lakini pia kula mlo kamili kila siku.

Tupunguze matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi mfano soda, chips/yai (Wanaume wa Dar wanahusika sana kwenye hiki kipengele
)

All in all, kisukari ni ugonjwa mbaya na korofi sana!
 
Tuwe na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara, lakini pia kula mlo kamili kila siku.

Tupunguze matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi mfano soda, chips/yai (Wanaume wa Dar wanahusika sana kwenye hiki kipengele)

All in all, kisukari ni ugonjwa mbaya na korofi sana!
😀😀
 
Daaa mkuu umenichekesa sana eti wanaume wa Dar wanahusika. Leo nimepunguza stress kwa kucheka
 
Hivi wana Sayansi wameshindwaje kuidhibiti au replacement ya hii kongosho ilhali mpaka Figo wsmeweza? Mtu mwenye kisukari anatumia pesa nyingi kwenye Dawa za kuitumia Kila siku kwa maisha yake yote, mbona TB serekali wanagharamia wanashinwa vipi kugharamia Dawa za kisukari?
 
Kisukari type 2 ambayo wengi wanayo ni kutokana na sedentary lifestyle na kula wanga mwimgi. Muhimu, punguza wanga kabisa, ongeza protein matunda na mboga mboga. Acha kula processed foods and drinks. Fanya mazoez hata ya kutembea. Kisukari utakiskia kwa jirani
 
Hivi wana Sayansi wameshindwaje kuidhibiti au replacement ya hii kongosho ilhali mpaka Figo wsmeweza? Mtu mwenye kisukari anatumia pesa nyingi kwenye Dawa za kuitumia Kila siku kwa maisha yake yote, mbona TB serekali wanagharamia wanashinwa vipi kugharamia Dawa za kisukari?
thinkstupid.png
 
Back
Top Bottom