Utafiti: Eti kuangalia tv kwa saa moja kunapunguza dakika 22 za maisha yako !!!

Utafiti: Eti kuangalia tv kwa saa moja kunapunguza dakika 22 za maisha yako !!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
UTAFITI: ETI KUANGALIA TV KWA SAA MOJA KUNAPUNGUZA DAKIKA 22 ZA MAISHA YAKO !!!

  • Ukifuata kila linalosemwa na wanasayansi utashindwa kuishi. Leo watasema kunywa kahawa kunapunguza msongo wa mawazo. Kesho watasema kunywa kahawa huko huko kunaongeza shinikizo la damu na uwezekano wa kupata pigo la kiharusi. Leo watasema hiki na kesho watasema kile ali mradi ni vurugu tupu. Kibaya zaidi ni ukimya wao kuhusu nini cha kufanya hasa pale tafiti zao zinapotoa matokeo yanayokinzana.

  • Kwa vile nyingi ya tafiti hizi hufanyika huko Ulaya na Marekani, Waafrika inabidi kuyapokea matokeo ya tafiti hizi kwa uangalifu sana kwani huwa hayazingatii mazingira yetu na mtindo wetu wa maisha (japo sasa tunajitahidi sana kuwaiga kwa kila kitu).

  • Utafiti uliofanywa mwaka jana na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Queenesland unaonyesha kwamba kuangalia runinga kwa watu wenye umri wa miaka 25 na kuendelea kuna madhara makubwa kiafya na kunapunguza muda wa kuishi. Utafiti huu unaonyesha kwamba kwa kila saa moja unayoitumia ukiangalia runinga basi unajipunguzia dakika 22 katika maisha yako. Hii ni sawa na kuvuta sigara mbili.

  • Wanasayansi hawa wanasema kwamba tatizo hasa siyo kuangalia tv bali madhara ya kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu ambako kunasababisha magonjwa ya moyo, kisukari, kunenepeana na matatizo mengine ya kiafya yanayosababishwa na mtindo wa maisha ya kubweteka (sedentary lifestyle). Kufanya mazoezi, hata kama ni dakika 15 tu kwa siku ni jambo la muhimu na kumeonyeshwa kuwa na faida nyingi za kiafya ikiwemo kuongeza siku tatu katika maisha yako.

  • Ati, kwetu sisi Waafrika, kuna ukweli wo wote katika utafiti huu? Utafiti huu unapatikana HAPA.
 
Kuangalia televisheni muda mrefu kunapunguza umri.

Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kwamba kuangalia televisheni kwa zaidi ya masaa mnne kwa siku kunapunguza umri.

Wataalamu wa Australia wamegundua kwamba, watu ambao hukaa kwa muda mrefu wakitazama televisheni, wanakabliwa na hatari kubwa ya kupatwa na matatizo ya afya hasa magonjwa ya mishipa ya damu, suala ambalo huhatarisha maisha yao na kuwapunguzia umri.

Wanasema kwamba, kukaa muda mrefu mbele ya TV kuna hatari kubwa kwa maisha ya mtu kutokana na kuwa shughuli za kawaida za mtu ambazo ni pamoja na kusimama na kutumia misuli ya mwili huwa hazifanywi na mtu hukaa tu chini.

Wataalamu hao wameelezea kuwa, watu wengi kwa siku hujongea tu kutoka kiti kimoja hadi kingine, kutoka katika gari kuelekea ofisini na kutoka katika kiti cha ofisini hadi nyumbani katika kiti kingine mbele ya televisheni.

Uchunguzi huo umetahadharisha kwamba, hata watu wenye afya zao za kawaida wanaweza wakawa wanakabiliwa na hatari kubwa kutokana na kukaa kwa muda mrefu suala ambalo huathiri kiwango cha sukari na mafuta katika damu.

Hatari ya kukaa kwa muda mrefu haiwezi kuondolewa kwa kuanza kufanya mazoezi, kwani uchunguzi huo umegundua kuwa, hata watu wanaofanya mazoezi, iwapo wanaangalia tv kwa muda mrefu, pia wana hatari ya kuwa na maisha mafupi.
 
Tumekusoma na tumekusikia. Kuanzia leo na kuendelea mie na hobby yangu ya kuangalia movies, in between niwe nanyanyuka kidogo kwenda kunywa maji n.k? :wink2:
 
Mh, nadhani utafiti huo pia unategemea mazingira ya muangaliaji mwenyewe,
mfano mazingira ya Ulaya ni tofauti na huku kwetu ambako aina ya maisha
tunayoishi tayari ni mazoezi tosha, wala huhitaji kwenda Gym. Sidhani kama
kuangalia TV kunaweza kutupunguzia maisha, badala yake kutatuongezea
kwa kuwa hutufanya kusahau stress nyingi za kimaisha na kutuliwaza...
 
Inawezekana kuwa na ukweli mwingi juu ya utafiti huo, lakini ni kwa mazingira yapi? Mfano kwa Mtazania wa kawaida na maisha ya kubangaiza kama yangu kutwa na mihangaiko ya maisha hata jioni nikiangalia TV kwa saa tatu mfululizo sidhani kama nitapata madhara hayo yaliyotajwa.

Hapa cha msingi ni mazoezi ama maisha ya kazi ili kuuweka mwili katika hari nzuri, maana kama issue ni kukaa sehemu moja kwa saa moja and above wale wa maofisini mbona kwao ni kiama.
 
Wanasayansi hawa wanasema kwamba tatizo hasa siyo kuangalia tv bali madhara ya kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu ambako kunasababisha magonjwa ya moyo, kisukari, kunenepeana na matatizo mengine ya kiafya yanayosababishwa na mtindo wa maisha ya kubweteka (sedentary lifestyle). Kufanya mazoezi, hata kama ni dakika 15 tu kwa siku ni jambo la muhimu na kumeonyeshwa kuwa na faida nyingi za kiafya ikiwemo kuongeza siku tatu katika maisha yako.

Kuna ukweli ndani yake. tatizo ni kuwa wengi tunaoangalia TV kwa muda mrefu ni watu wa tizz kila siku kwa kuelewa mapungufu ya miili yetu kukosa mazoezi kwahiyo huenda tutakuwa na masiha marefu kulikoni!
 
hii ningeamini tu kama siku ninayozaliwa ningeambiwa nitaishi miaka mingapi...
lakini kwa fumbo ambalo lipo sasa ni ngumu kujua

Mwenyezi Mungu alikupangia uishi miaka 120. Jisomee Mwanzo 6:5. Lakini kwa vile unaipenda hii dunia kuliko Muumba wako basi miaka itapungua kulingana na dhambi unazomtesa nazo Mungu wangu!
 
Kuangalia televisheni muda mrefu kunapunguza umri.

Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kwamba kuangalia televisheni kwa zaidi ya masaa mnne kwa siku kunapunguza umri.

Wataalamu wa Australia wamegundua kwamba, watu ambao hukaa kwa muda mrefu wakitazama televisheni, wanakabliwa na hatari kubwa ya kupatwa na matatizo ya afya hasa magonjwa ya mishipa ya damu, suala ambalo huhatarisha maisha yao na kuwapunguzia umri.

Wanasema kwamba, kukaa muda mrefu mbele ya TV kuna hatari kubwa kwa maisha ya mtu kutokana na kuwa shughuli za kawaida za mtu ambazo ni pamoja na kusimama na kutumia misuli ya mwili huwa hazifanywi na mtu hukaa tu chini.

Wataalamu hao wameelezea kuwa, watu wengi kwa siku hujongea tu kutoka kiti kimoja hadi kingine, kutoka katika gari kuelekea ofisini na kutoka katika kiti cha ofisini hadi nyumbani katika kiti kingine mbele ya televisheni.

Uchunguzi huo umetahadharisha kwamba, hata watu wenye afya zao za kawaida wanaweza wakawa wanakabiliwa na hatari kubwa kutokana na kukaa kwa muda mrefu suala ambalo huathiri kiwango cha sukari na mafuta katika damu.

Hatari ya kukaa kwa muda mrefu haiwezi kuondolewa kwa kuanza kufanya mazoezi, kwani uchunguzi huo umegundua kuwa, hata watu wanaofanya mazoezi, iwapo wanaangalia tv kwa muda mrefu, pia wana hatari ya kuwa na maisha mafupi.

Nadhani mimi nitakuwa nimebakiza wiki ya kuishi sasa......
 
Mara nyingi tafiti za wazungu ni for African consumptions wao hawazitumii hata siku moja! inabidi kuwa macho nazo ukizi apply you are in for it. mzungu fulani aliwahi kuniambia anatamani afrika ndio ingekuwa ulaya!
 
Hata kutembelea JF kwa muda wa zaidi ya saa moja ni hatari kwa maisha yako
Roho inanidundaje ,maana mie nikitoka kuangalia pira kama tatu 90minsx 3 napiga akina john cena ,movie or tamthilia moja ndio usingizi!nafwaa mapema wajameni!
 
kama ni hivyo leo mimi ndio mwisho.. uhai kwishiney....
 
Back
Top Bottom