Utafiti kuhusu mitandao ya kijamii na demokrasia

Utafiti kuhusu mitandao ya kijamii na demokrasia

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,186
Reaction score
7,492
Salama wakuu,

Wakuu wana JF, Tunafanya utafiti kuhusu Mchango wa mitandao ya kijamii kwenye demokrasia Tanzania.

Lengo la utafiti huu ni kutafuta taarifa zitakazojibu maswali mbalimbali kuhusu uhusiano wa mitandao ya kijamii na demokrasia.

Maswali yanayohitaji kupatiwa majibu ni pamoja na swali, je! Mitandao ya kijamii inasaidia kukua kwa demokrasia au inaharibu demokrasia iliyopo.

Katika utafiti huu, watafiti wataisoma zaidi jamiiforums miongoni mwa mitandao mingine.

Kama ikikupendeza, tunakuomba kusadia kujibu maswali machache kwa kubonyeza link. Ni maswali rahisi sana sana na yanahitaji muda mfupi sana kujibu.

Asante.
 
Hesabuni hapa hapa maoni, kwenye link hatutaki tunajua hiyo ni kazi ya mabeberu kuelekea october 2020 mnata kufilter social network zetu mtuletee habari za uchochezi dhidi ya serikali yetu.

Mitandao ya kijamii inaharibu demokrasia kwasababu wanasiasa wanachukulia kama platform za kuropoka badala ya kutoa maoni kistaarabu.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuna maswali mengi mengi sio moja tu Mkuu. Ndio mantiki ya link. Ila hata kujibu hapa sivibaya ila ukijibu kwenye link itapendeza zaidi.

Kingine usiwe na negative perception ya vitu kabla hujajiridhisha kama kweli kuna ubaya kwenye kitu husika. Kwa mfano unapokutana na mtu usianze kuwaza kwamba atakuloga wakati amekupa salami tu hahahhaah
 
Azizi Mussa,
Mkuu Azizi hayo mambo ya link mmh! 🤔 utawapata wachache ! Wewe orodhesha maswali hapa watu watiririke biashara ya kuwaambia waingie kichochoroni kujibu haifai !
 
Azizi Mussa,
Mkuu Azizi hayo mambo ya link mmh! 🤔 utawapata wachache ! Wewe orodhesha maswali hapa watu watiririke biashara ya kuwaambia waingie kichochoroni kujibu haifai !
Kwa niaba ya wengine, nawashukuru sana wakuu kwa ushirikiano wenu. Response imekuwa ni nzuri sana na tumepata ushiriki wa wadau zaidi hata ya tulivyokuwa tumetaraji. Kwa mantiki hiyo, tumefunga survey na tunawashukuru sana.

Kila la heri kwenye kuendelea kuitumia vyema demokrasia iliyopo.
 
Back
Top Bottom