Utafiti: Madaktari Tanzania Wanatelekeza Wananchi Vijijini

Utafiti: Madaktari Tanzania Wanatelekeza Wananchi Vijijini

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tanzania inatumia kati ya $40,000 & $60,000 kusomesha daktari mmoja (medical doctors), lakini madaktari wanne kati ya kumi wanaomaliza elimu hii wana achana na fani ya udaktari muda mfupi baada ya kuhitimu masomo yao. Hili tatizo (kama sio janga) kwa taifa, hasa ikizingatiwa pia kwamba Tanzania ni moja ya nchi zenye "Doctor to patient ratio" kubwa sana duniani – uwiano huu kwa Tanzania ni Wastani wa Daktari Mmoja Kwa Kila Watu 26,000. Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO), uwiano unaotakiwa ni Daktari Mmoja Kwa Kila Watu 1,000, au chini ya hapo. Kwa maana hii, wastani wa Tanzania umezidi kigezo cha WHO kwa mara ishirini na sita elfu, huku baadhi ya maeneo ya nchi yakiwa na uwiano ambao ni mkubwa na wa kutisha zaidi, kwa mfano:

  • Kigoma – Daktari mmoja anahudumia watu 308,000
  • Mara, Daktari mmoja anahudumia watu 167,000
  • Tabora – Daktari mmoja anahudumia watu 132,000 (huu ni mkoa wa Dr. @hkigwangala).

Mikoa yenye uwiano ulio chini zaidi ya hiyo hapo juu ni pamoja na:

  • Arusha (22,000);
  • Dar-es-salaam (24,000) na
  • Pwani (32,000);

Lakini pamoja na mikoa hii kuwa na unafuu, bado uwiano huu ni mkubwa sana kwa vigezo vya WHO.

Kwa mujibu wa utafiti mwingine uliofanywa hivi karibuni, 42% ya watanzania wanaomaliza elimu zao za udaktari huwa wanachagua kufanya kazi katika miji michache kama ifuatavyo: Dar-es-salaam, Mwanza, Moshi, Mbeya na Arusha. Dar-es-salaam peke yake accounts for 32% ya medical doctors wote nchini, na hali hii ni ushahidi tosha kwamba kama taifa, tumeshindwa kuwapatia hudumu bora za kiafya wananchi walio wengi (hasa vijijini).

Katika karne ya ishirini na moja, ushindani wa nchi kiuchumi unapimwa na hazina ya rasilimali watu iliyoko (Human Capital), ambayo sehemu kubwa inajengwa na ubora wa Elimu na Afya miongoni mwa wananchi (hasa nguvu kazi). Kwa maana nyingine, Labour productivity ni zao la Elimu na Afya Bora ya labor force katika uchumi. Kwa vile ni dhahiri kwamba sekta zote hizi mbili (Elimu na Afya) zinakabiliwa na majanga, nadhani itakuwa sahihi kuhitimisha kwamba tunaendelea kujidanganya kwamba sisi kama taifa sasa tupo tayari in terms of "capabilities" kushiriki kikamilifu in today's competitive global economy.

Cc: Nguruvi3, Zakumi, Zinedine, gfsonwin, zumbemkuu, Kichuguu, JingalaFalsafa, HKigwangalla, EMT, Jasusi, JokaKuu, Ben Saanane, Bongolander et al.
 
Last edited by a moderator:
....madaktari wanne kati ya kumi wanaomaliza elimu hii wana achana na fani ya udaktari muda mfupi baada ya kuhitimu masomo yao.

Labda swali hapo ni kwa nini wanaamua kuachana na udaktari muda mfupi baada ya kumaliza masomo yao? Of course, the fact kuwa mtu amesomea fani fulani does not necessarily mean that atafanya kazi kwenye hiyo fani. Kuna surveys zinadai kuwa baadhi ya madaktari huwa wanajuta kusomea fani hiyo muda mfupi baada ya kumaliza masomo yao.

Kwa mfano, mwaka jana huko Marekani kati ya madaktari 24,000, ni asimilia 54 tuu waliosema wangechagua tena udaktari kama kazi yao. Moja ya sababu walisozitaja ni kuanguka kwa kipato, pamoja na sababu nyingine ambazo zina-apply zaidi kwenye context ya Marekani: Why Do So Many Doctors Regret Their Job Choice? - Forbes

Pia survey iliofanyika Uingereza na kuchapishwa mwaka jana unaonyesha kuwa "less than one-third of newly qualified doctors in the UK want a career in general practice" - Reasons why doctors choose or reject careers in general practice: national surveys.

Tukija hapa kwetu, juzi nilikuwa nasoma The Citizen kuwa kati ya Januari hadi katikati ya mwaka huu madaktari 184 wa Kitanzania walienda nje ya nchi "in search for greener pastures" - Where TZ doctors go for greener pastures - National - thecitizen.co.tz. Wengi wa madaktari hao wameenda Uganda, Kenya na Marekani.

Gazeti hilo hilo linadai kuwa asilimia 40 ya madaktari wanaachana na fani hiyo - Revealed: 40pc doctors ditch profession yearly - National - thecitizen.co.tz. Baadhi ya sababu za madaktari kuachana na fani hiyo zimeelezwa kwenye hizo links.

Swali lingine la kujiuliza ni kuwa madaktari pekee ndiyo wanaoongoza kwa kuzikacha fani zao?
 
Tatizo kwa Tanzania si mishahara tu ya madaktari. Madaktari wetu hawana vitendea kazi. Nadhani hii ndiyo iliyopelekea mgomo uliotusababishia madhara ya Ulimboka. Serikali yetu ingejikita katika kuwawezesha madaktari wetu kwa kutoa vifaa vya kisasa zaidi katika hospitali zetu badala yake Kikwete akawataka warudishe nyumba na waende kwingineko. Angalieni mishahara ya wabunge na ulinganishe na kiasi wanacholipwa madaktari, utaelewa ni kwa nini Kigwangalla aliamua kugombea ubunge badala ya kufanya kazi aliyosomea.
 
Mkuu sidhani kama tutakuwa wakweli tukisema tatizo ni vitendea kazi au mishahara. Mimi naona tatizo kubwa linalotukabili wa Tanzania ni uongozi. Madakatari wetu wana uzalendo na moyo mkubwa sana wa kuwasaidia wagonjwa, tatizo ni kuwa we over pay politicians and regard them highly than all others walimu, madereva, wanafunzi, polisi...

Takwimu zinatisha, lakini among our politicians who really cares? ukisikia wanaumwa, hata mafuta tu au tumbo, wanakwenda hospitali Ulaya. Unadhani kweli watajali hospitali zetu, au madaktari wetu?
 
Bongolander,
We are essentially saying the same thing. Only you said it better.
 
Hongera sana kwa mabandiko yako ya kiuchunguzi/tafiti. Unasaidia sana kurejesha hadhi ya JF kwa mabandiko yenye maudhui safi kwa uboreshaji wa maisha ya watanzania.

Hata hivyo mimi nina haya...kwa namna nilivyoitafakari mada yako.

Mkuu ukiwa na "the more or less Dead Civil Services (ikiwemo huduma ya kitabibu/udaktari", unategemea kitu gani hapo...!!?

The "Vibrant Active Civil Services" haiathiriwi na maamu ya wanasiasa wawili watatu ...!, hii inakuwa na mfumo wake thabiti..ambao hauyumbishwi na wanasiasa.

Nchi ambazo zina mfumo imara wa Civil Services....ni pamoja na Neitherland...,hata Tanzania ile ya Nyerere Civil Services system iliyo imara na bora. Aliowakabidhi uongozi wakaivuruga.

Mkuu hivi uliwahi kusikia kupinduana kwa mawaziri wakuu wa Italy kumesababisha huduma za umma kuzorota...!?

Lakini hapa kiko wapi...kila uchaguzi ukikaribia, ama kubadilisha baraza la mawaziri...purukushani kibao kwenye huduma za kijamii ikiwemo utabibu. Kwa sasa tuna 'more or less Dead Civil Services'

Kwa hiyo ili kumaliza tatizo hili lazima tuimarishe mfumo wa huduma za umma ambao hautaathiriwa na misuguano ya kiasiasa na tamaa za wanasiasa
 
Kwa maoni yangu binafsi ni kweli serikali inawalipa kidogo wafanyakazi wake. Lakini tujiulize je serikali ingekuwa inawapa hapa madaktari na wafanyakazi wengine mishahara inayotosha wangebaki vijijini? Ukweli wa mambo ni hapana. Wasomi walilazimishwa kwenda JKT ili wapate mbinu za kuishi vijijini lakini bado ni vigumu kuwarudisha huko.

Imefika wakati tukubali kuwa maisha ya vijijini hayavutii na watu wanahamia mijini. Hivyo cha muhimu ni kukuza miji hili watanzania wengi waishi mijini na vijiji vingi viwe karibu na mijini.
 
Ningependa kujadili michango ya wadau mbalimbali kama ifuatavyo:

EMT - Ni kweli kwamba hata nchi zilizoendelea, wapo madaktari ambao huwa na tabia kama za madaktari wetu - abandon their profession, lakini hili sio tatizo kubwa sana kwao kwa vile private returns to education (udaktari) katika nchi nyingi za OECD ipo juu, tofauti na kwetu. Ndio maana kwa nchi kama marekani bado doctor to patient ratio ni nzuri i.e. Daktari Mmoja Kwa Watu Mia Tatu (1:300), kiwango ambacho ni way below the WHO's requirement of 1:1000.

Lakini pamoja na hayo, bado serikali inaona kuna umuhimu wa kuwapatia wananchi wengi zaidi access to healthcare (rejea malengo ya Obama Care), ambayo pamoja na malengo yake mazuri, inakabiliwa na upinzani mkubwa sana. Suala hili linanikumbusha changamoto za Mwalimu Nyerere katika kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa kwa watanzania (wakati wa ujamaa). Pamoja na ukweli kwamba malengo yake yalikuwa ni mazuri, wengi walipingana na bado wanamkosoa mwalimu na juhudi zake hizi. Wanasahau kwamba 1961 Tanzania ilipopata uhuru, jumla ya idadi ya watu Tanganyika (total population) ilikuwa ni milioni tisa (9 million), huku 90% wakiwa vijijini, na nchi ilikuwa na jumla ya medical doctors kumi na mbili tu!. Leo hii, hawa hawa wanaompinga Mwalimu na kuunga mkono liberalization of the sector wanashindwa kutupa majibu kwanini basi hiyo sekta binafsi imeshindwa kufanikisha hata robo ya mafanikio ya Mwalimu katika kufikishia watanzania walio wengi huduma za afya. Leo hii, huduma nyingi za afya zinatolewa zaidi na non-profit sector; Zakumi, ningependa kusikia maoni yako juu ya hili;

Vinginevyo serikali imekuja na kitu kinaitwa Community Health Fund (CHF) ambayo inalenga zaidi kuwapatia bima za afya watanzania wanaoisho vijijini. Pamoja na juhudi zote, watanzania waliojiandikisha na mfuko huu hawavuki 500,000. Ikizingatiwa karibia 70% ya watanzania bado wanaishi vijijini (sawa na karibia watanzania milioni 32), ina maana CHF imefikia less than 2% of the population. Katika moja ya sababu kwanini wananchi wengi hawana mwamko na kujiunga na mfuko huu ni pamoja na kwamba, kutokana na mapato yao kuwa ya msimu (kilimo), kulipa shillingi 15,000 kama ada ya mwaka bado ni nyingi sana kwa baadhi ya familia. Lakini sababu kubwa zaidi ni kwamba wanalalamikia huduma mbovu zinazotolewa chini ya CHF, hivyo kuturudisha pale pale kwenye tatizo la uhaba wa madaktari kwa wananchi walio wengi;

Nakubaliana na hoja ya Jasusi kwamba moja ya matatizo ya msingi ni mishahara midogo na ukosefu wa vitendea kazi; Vile vile Bongolander kwamba fani ya udaktari haipewi heshima/hadhi yake (pamoja na ya ualimu); Kwa kweli hii inastaajabisha kwani productivity ya uchumi wowote hutegemea ubora wake wa HUMAN CAPITAL (Elimu na Afya ya labour force), kitu ambacho ndio msingi wa capabilities and productivity katika uchumi. Ni vigumu kuelewa uongozi wetu wa nchi unamaanisha nini pale unapopiga porojo kwa macho makavu eti tumejipanga kuingia kwenye kundi la nchi zenye "uchumi wa kati" - are they serious? Mpiga kelele kajadili suala hili la uongozi mbovu.

Wakuu MpigaKelele, Bongolander na jasusi – kwa kuongezea tu, msingi wa tatizo ni kwamba - Pamoja na ukweli kwamba 75% ya mahitaji ya wananchi ya afya yapo katika first level (i.e. basic clinics and dispensaries), huku asilimia 25% tu ya health needs zikiwa katika higher level i.e. referral hospitals and specialty hospitals), katika kupanga bajeti za wizara ya afya na ustawi wa jamii kila mwaka, serikali huwa haitengi fedha kwa kufuatana na mahitaji haya. Badala yake, asilimia 75% of Resources (madawa, vifaa, mishahara, posho, education and training etc) huwa zinapelekewa kwenye level ya juu (referral hospitals na Specialties), huku levels za chini ambazo zina wananchi walio wengi (basic clinics and dispensaries), zikiambukia only 25% of the budget. Ni kwa maana hii, madaktari wengi hukimbilia levels hizo za juu ambazo ndio zina maslahi Zaidi kutokana na kuwa prioritized katika budget allocations.

Muhimu:

Tukumbuke kwamba 90% ya magonjwa yanayowasumbua watanzania walio wengi na pia magonjwa ambayo yanaua watanzania wengi, yanaweza kutibiwa katika lowest levels (dispensaries and clinics) iwapo vitapatiwa tu wataalam wa kawaida, vifaa basic tu vya diagnosis, na madawa. Lakini kutokana na serikali kutojali eneo hili in terms of budget and resources allocation, matokeo yake ni wataalam wengi kurundikana kwenye higher levels of the 3 tier health system kufuata maslahi kutokana na mgao wa bajati; kwa maana nyingine, mfumo wetu wa bajeti unafanya resources misallocation kwa kiasi kikubwa sana. Magonjwa yanayowasumbua na pia kuua watanzania wengi ni haya:

  • Malaria; Acute Respiratory Infection ; Numonia ; Kuhara; Eye infection; Skin Infection; Anaemia; na UTI; Magonjwa ya kulala hayapo mengi kama yale ya kutohitaji kulala; Malaria accounts for over 50% ya magonjwa yote, mengine ikiwa ni TB, Ukimwi, na kuhara (about 30%).

Tunabakia kujiuliza – sasa inakuwaje allocation ya bajeti inapendelea zaidi ngazi za juu (referrals and specialty hospitals) wakati 90% ya mahitaji ya afya ya watanzania ni ya magonjwa ambayo hayahitaji referral and specialty hospitals na badala yake yanaweza kutibiwa kwenye clinics, dispensaries iwapo kutakuwa na kipaumbele in terms of vifaa vya msingi tu na wataalam?

Mwisho ni hoja ya Zakumi kwamba hakuna incentives za madaktari kuhamia vijijini. Nakubalia na msingi wa hoja hii lakini solutions unazoleta kwa kweli zinashangaza kidogo; Kama nimekusoma vizuri mkuu Zakumi, unashauri kwamba tuje na sera za kuhimiza urbanization ili wananchi walio mbali na maeneo yenye huduma nzuri za afya (yani vijijini) waweze kuhamia karibu na sehemu zenye huduma hizi (mijini), seriously? Is it that simple? Hivi tunavyozungumza, tayari miji mingi inalemewa na kasi ya urbanizasation na kupelekea uhaba wa huduma nyingi za msingi, hali inayochangia kushamiri kwa umalaya, ujambazi, machafuko ya kisiasa kutokana na umaskini n.k. Sasa badala ya wewe kuhimiza turudi kwenye drawing board na kuangalia tufanikishe vipi rural development, wewe unaona solution is to encourage urbanization!? Kwa mtazamo wako, ina maana kwamba 70% of the population ambayo ipo vijijini ihamie kule ilipo 30% of the population, and then things will return to equilibrium.

Mkuu@zakumi, takwimu za afya zinatuonyesha kwamba miji iliyo mingi ina ratio kubwa sana ya patient to doctor, mfano Mara, the ratio is 1:300,000, Kigoma, the ratio is 1:160,000 and so forth and so forth, kwahiyo kwa mtazamo wako, solution ni kuhamishia wakazi wa vijiji vya maeneo haya waende mijini (Kigoma mjini, Musoma mjini)?

Cc Nguruvi3, Kichuguu, Zinedine, Mkandara, zumbemkuu, JingalaFalsafa, gfsonwin
 
Last edited by a moderator:
Vinginevyo serikali imekuja na kitu kinaitwa Community Health Fund (CHF) ambayo inalenga zaidi kuwapatia bima za afya watanzania wanaoisho vijijini. Pamoja na juhudi zote, watanzania waliojiandikisha na mfuko huu hawavuki 500,000. Ikizingatiwa karibia 70% ya watanzania bado wanaishi vijijini (sawa na karibia watanzania milioni 32), ina maana CHF imefikia less than 2% of the population. Katika moja ya sababu kwanini wananchi wengi hawana mwamko na kujiunga na mfuko huu ni pamoja na kwamba, kutokana na mapato yao kuwa ya msimu (kilimo), kulipa shillingi 15,000 kama ada ya mwaka bado ni nyingi sana kwa baadhi ya familia. Lakini sababu kubwa zaidi ni kwamba wanalalamikia huduma mbovu zinazotolewa chini ya CHF, hivyo kuturudisha pale pale kwenye tatizo la uhaba wa madaktari kwa wananchi walio wengi;

This CDF was also externally imposed on us. I don't think the idea originated from the government.

Remember the World Bank's Agenda for Reform which advocated for the for the introduction of user fees in developing countries and a long-term policy for the introduction of health insurance?

This is what set the health agenda policy for the late 1980s, which took up the theme of a smaller role for government in health care, but with emphasis on a more centralised approach to finance.

Hii ndiyo iliyo-redefine the roles of public and private sector in health care, resulting into massive changes in finance and provision of health services in Tanzania.

Ripoti ya WB, World Development Report (1993), ilisizitiza kuanzishwa kwa user fees and insurance, decentralisation of health services na kutaka private sector kugharamia na kutoa huduma za afya.
 
Mchambuzi;

Sikutaka kuingiza mambo ya Nyeree katika mjadala huu, lakini naona umenitafuta. Hivyo nitajibu lakini ningependa emotions mziweke pembeni na kujadili facts. Nitaanza kwa history.

Katika miaka ya 50 liberals katika nchi za magharibi walianza kujadili matatizo ya kuondoa umasikini. Miongoni mwao alikuwa Robert McNamara. Ambaye baadaye alikuwa President wa World Bank. Walikuja na nadharia kadhaa za kuondoa umasikini. Zifuatazo ndizo nazokumbuka.

Ya kwanza. Nchi tajiri zikitoa 1% ya GDP zao kusaidia nchi masikini, mchango wao hautafanya nchi tajiri kuwa masikini. It's just 1% of GDP. Mchango huu kama utatumika vizuri utasaidia kuondoa umasikini. Formula hii bado inatumika. Misaada ya Marekani kwa nchi masikini ni 1%.

Ya pili: Nchi masikini zikisaidiwa katika huduma za Afya na elimu, zitaweza kujisadia zenyewe. Magonjwa yalikuwa yanafanya nchi masikini kupoteza talents. Yalikuwa yanafanya watu kutumia muda wao mwingi wa kazi kwenye matibabu na hivyo kutokuwa wazalishaji.

Kutokana wasifu wake wa kazi na msimamo wake, mwaka 1968 Robert McNamara alichaguliwa kuwa rais wa Benki ya Dunia. Kitu cha kwanza alichofanya ni kufanya mageuzi ya benki kuwa ya kuondoa umasikini duniani.

Kwa bahati nzuri mission mpya za benki ya dunia ikawa inafanana na mipango ya maendeleo ya jamii ya Julius Nyerere. Hivyo mafuriko ya misaada yakafunguka. Sio kwa Tanzania pekee yake bali kwa nchi nyingi za dunia ya tatu.

Kitu alichofanya Nyerere alitumia misaada kwa kazi zilizotakiwa. Hakutumia misaada hiyo kujinufaisha. Na matokeo ya kazi zake yalionekana. Wastani wa maisha uliongezeka. Vifo vya watoto vilipungua. Na watu walijishughulisha katika shughuli mbalimbali.

Matatizo mkubwa ya kiuchumi yalitokea miaka ya 70 kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kujitakia, nchi za kiafrika zilishindwa kutimiza wajibu wakujitegemea kifedha. Kufikia mwishoni mwanzoni mwa 80, Zaidi ya nchi 30 za kiafrika ikiwemo Tanzania zilishindwa kumudu kulipa madeni yake.

Hivyo nadharia ya kusaidia huduma za afya, elimu na maji ikapungua nguvu zake. 1981 Robert McNamara akaondoka WB na tukaanza kupewa vidonge vya kufanyia reform uchumi na huduma za jamii.

Ndugu Mchambuzi kwa kifupi tu, huu ndio mtazamo wangu. Nyerere alifanya juhudi kubwa kuanzisha mfumo wa afya ambao ulisadia watanzania wengi. Tatizo kubwa ni kuwa mfumo wenyewe ulikuwa tegemezi. Ulitegemea sana foreign donors.

Kuhusiana na mawazo yangu kuhusu urbanization nitarudi baadaye. Wako katika kusukuma gurudumu la maendeleo,

Z10
 
Mchambuzi;

Kitu alichofanya Nyerere alitumia misaada kwa kazi zilizotakiwa. Hakutumia misaada hiyo kujinufaisha. Na matokeo ya kazi zake yalionekana. Wastani wa maisha uliongezeka. Vifo vya watoto vilipungua. Na watu walijishughulisha katika shughuli mbalimbali.

Ndugu Mchambuzi kwa kifupi tu, huu ndio mtazamo wangu. Nyerere alifanya juhudi kubwa kuanzisha mfumo wa afya ambao ulisadia watanzania wengi. Tatizo kubwa ni kuwa mfumo wenyewe ulikuwa tegemezi. Ulitegemea sana foreign donors.

Mkuu Zakumi:

Kwa kuongezea tu, tafiti nyingi zinaeleza kwamba Tanzania ilipiga hatua kubwa zaidi katika sekta ya afya katika kipindi cha Ujamaa kuliko kipindi baada ya ujamaa (Structural adjustments policies); Kwa mfano, Lugalla in his study titled: "Economic Reforms and Health Conditions of the Urban Poor in Tanzania" ananukuu taarifa za Wizara ya afya na ustawi wa jamii pamoja na tume ya mipango ambao kwa pamoja wanaeleza kwamba:

Kufuatia ujio wa mageuzi ya kiuchumi (SAPs), maendeleo ya miundo mbibu sekta ya afya yamekuwa madogo sana ikifananishwa na kipindi cha Ujamaa. Wizara na tume ya mipango zinaongeza kwamba kipindi cha Ujamaa ndicho kilicho boresha zaidi upatikanaji wa afya kwa wananchi (in terms of distance to healthcare facilities) kuliko kipindi baada ya Ujamaa. Wanatoa mfano kwamba - kati ya mwaka 1967 to 1985, idadi ya hospitali nchini iliongezeka kutoka 116 hadi 152 (ongezeko la kama 31%t). Vituo vya afya navyo viliongezeka kutokea vituo 46 hadi vituo 260 (ongezeko la asilimia 465%!!), huku zahanati zikiongezeka kutoka 1,237 hadi 2,852 (ongezeko la 131%). Nchi haijawahi to experience kitu kama hiki tena ever since. Kwa maana hii basi, ni sahihi kuhitimisha kwamba - kipindi cha Ujamaa kilijali zaidi afya za watanzania kuliko vipindi vilivyofuatia (mwinyi, Mkapa, Kikwetwe - kwa pamoja), chini ya uliberali na soko huria;

Kufuatia mageuzi (post ujamaa period) - ambapo sekta ya afya yalishika kasi kuanzia miaka ya mwanzo ya tisini, qualified health workers kwenye vituo vya afya, zahanati na hospitali wamekuwa ni haba; Kutokana na hili, kama kawaida ya serikali isiyojali, ikaja na Voda Fasta ya manesi (kama ilivyo kwa walimu) ambapo hivi sasa, manesi wengi ni wahitimu wa darasa la saba ambao wanapelekwa kwenye introductory course ya nursing kwa mwaka mmoja kisha wanakuwa unleashed kwenda kucheza na maisha ya watanzania;

cc Nguruvi3
 
@Mchambuzi.
Rober Mcnamara alikuwa rais wa WB kati ya 1968 na 1981. Changamoto ya kwanza baada ya uhuru ilikuwa kupata watu wa kutoa huduma nchi ikiwa na 9 qualified medical doctors na Nurses.

Alichokifanya Mwalimu ni kuanzisha mafunzo kwa kada za RMA, Medical assistants(MA), Assistant medical officers(AMO). Hii ilikuwa ni kupata wataalam wa kukabiliana na matatizo ya kawaida yanayopeteza maisha

Mwaka 1968 mpango wa pili wa maendeleo ulishaanza na ujenzi wa vituo vya afya na zahanati ulikuwa umepamba motO, pamoja na kubadilisha chuo cha AMO kutoa mafunzo ya Medical officers.
Hivyo kulikuwa na jitihada za makusudi za kusaidia huduma za afya na wala si kwasababu ya McNamara.

Fani ya udaktari imebadiika kutokana na mahitaji ya dunia.Daktari anaweza kufanya kazi katika mashirika ya Bima, madawa, utafiti, takwimu n.k. Ukilinganisha na anayefanya clinical na yule anayefanya nje ya clinical vipato vyao ni katika ratio ya 1:3 Ndivyo ilivyo duniani kote.

Kwa nchi kama Marekani, kazi ya clinical ina ugumu kwasababu nyingi zikiwemo litigation.
Madaktari kutoka magharibi wanahamia mashariki ya kati kwasababu kipato ni kizuri bila hofu ya litigation n.k. Lakini pia kuna mashirika mengi yanayowahitaji nje ya kazi ya clinical yenye stress sana.

Tanzania inakabiliwa na changamoto za vipato. Madaktari wanaona masilahi mazuri nje ya fani yao na hivyo kukimbilia huko. Daktari anayefanya kazi katika mashirika na taasisi za kitaifa au kimataifa wastani ni 1:3 Kwanini asichangamkie fursa hiyo kwa vile 'maisha bora ni kwa kila Mtanzania'.

Upungufu wa vifaa unachangia kukatisha tamaa. Tanzania inapokuwa na CT scan moja Muhimbili ambayo inaharibika kwa miezi sita bila matengenezo inasikitisha. Madaktari wanabaki kufanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi. Inakuwaje bilioni 27 zitoke hazina bila kujua nani amezitoa, na zingenunua CT scan ngapi

Hivi nani atakuwa na muda wa kufikiria kucheza na maambukizi wakati wapo wanaoishi kiulani.
Kwanini naye asitafute njia halali za kuongeza kipato ili hali ana familia.

Kuna suala la siasa, hili nalo linachangia sana. Inapotokea kuna kundi linatibiwa nje ya nchi ni wazi haliridhiki na hali iliyopo. Mbunge au waziri atakuwa na uchungu gani huduma zikirota wakati kipato chake kinamruhusu achilia mbali serikali kumsimamia masilahi yake

Suala la incentives katika nchi zainazojali huduma ya afya zinafanyika kutokana na maeneo.
Kwa mfano daktari wa Lindi, Singida au Kigoma anapewa mshahara tofauti na daktari wa Dar au Arusha.

Kujazana kwa madaktari mijini ni matokeo ya huduma bora. Kwanini Daktari wa Dar aishi katika mazingira mazuri na yule wa Kigoma aishi mahali pasipo na nyumba. Mazingira yana matter sana.

Suala la mishahara: Lazima tukubaliane kila taaluma zina utofauti katika kuzipata na matumizi yake. Dr aliyesoma miaka 6 anapojikuta ana mshahara mdogo mara mbili ya mwenye Diploma ya uhasibu pale TRA inafikirisha. Ni kwanini basi Dr huyu aendelee kung'ang'ania uzalendo ili hali wote tunataka watoto wasome st. au inter school, sote yunaenda kariakoo na vituo vya mafuta pamoja.

Mbunge anapokuwa na mshahara mara 4 ya ule wa Daktari inatia hasira kusema ukweli.
Ndio maana akina Kigwangalla na wenzake wamekwenda Bungeni.
Ni haki yao kwasababu tumetengeneza mazingira hayo. Hawana kosa hadi tutakapobadilika.
`
 
Mkuu Zakumi:

Kwa kuongezea tu, tafiti nyingi zinaeleza kwamba Tanzania ilipiga hatua kubwa zaidi katika sekta ya afya katika kipindi cha Ujamaa kuliko kipindi baada ya ujamaa (Structural adjustments policies); Kwa mfano, Lugalla in his study titled: "Economic Reforms and Health Conditions of the Urban Poor in Tanzania" ananukuu taarifa za Wizara ya afya na ustawi wa jamii pamoja na tume ya mipango ambao kwa pamoja wanaeleza kwamba:

Kufuatia ujio wa mageuzi ya kiuchumi (SAPs), maendeleo ya miundo mbibu sekta ya afya yamekuwa madogo sana ikifananishwa na kipindi cha Ujamaa. Wizara na tume ya mipango zinaongeza kwamba kipindi cha Ujamaa ndicho kilicho boresha zaidi upatikanaji wa afya kwa wananchi (in terms of distance to healthcare facilities) kuliko kipindi baada ya Ujamaa. Wanatoa mfano kwamba - kati ya mwaka 1967 to 1985, idadi ya hospitali nchini iliongezeka kutoka 116 hadi 152 (ongezeko la kama 31%t). Vituo vya afya navyo viliongezeka kutokea vituo 46 hadi vituo 260 (ongezeko la asilimia 465%!!), huku zahanati zikiongezeka kutoka 1,237 hadi 2,852 (ongezeko la 131%). Nchi haijawahi to experience kitu kama hiki tena ever since. Kwa maana hii basi, ni sahihi kuhitimisha kwamba - kipindi cha Ujamaa kilijali zaidi afya za watanzania kuliko vipindi vilivyofuatia (mwinyi, Mkapa, Kikwetwe - kwa pamoja), chini ya uliberali na soko huria;

Kufuatia mageuzi (post ujamaa period) - ambapo sekta ya afya yalishika kasi kuanzia miaka ya mwanzo ya tisini, qualified health workers kwenye vituo vya afya, zahanati na hospitali wamekuwa ni haba; Kutokana na hili, kama kawaida ya serikali isiyojali, ikaja na Voda Fasta ya manesi (kama ilivyo kwa walimu) ambapo hivi sasa, manesi wengi ni wahitimu wa darasa la saba ambao wanapelekwa kwenye introductory course ya nursing kwa mwaka mmoja kisha wanakuwa unleashed kwenda kucheza na maisha ya watanzania;
Mchambuzi, kabla ya mageuzi ya kisiasa na kiuchumi tulikuwa na Hospitali katika hadhi zifuatazo.
1. Hospitali za rufaa : Muhimbili , KCMC, Bugando, Mbeya, Kibong'oto na Ocean road
2. Hospitali za mikoa
3. Hospitali za Wilaya
4. Vituo vya afya na zahanati

Kila hospitali iilkuwa na hadhi kulingana na vigezo tarajiwa. Katika Hospitali za rufaa kilichoangaliwa ni idadi ya wataalam, sifa za watalaam , vifaa. Hopitali ya rufaa inakuwa na mabingwa wa maradhi na hali mbali mbali(Specialists)

Mwaka jana kukaja voda fasta ya hospitali kuwa za rufaa. Hospitali hizo zingine zikiwa hazina hata medical officer. Waliopo ni wasaidizi tu kama clinical officers n.k.
Maamuzi yalitangazwa katika mikutano ya kisiasa bila hata ya kuwasilina na watalaamu.

Kwa pamoja (Mkapa, Mwinyi na Kikwete) hakuna miundo mbinu ya afya waliyoongeza zaidi ya ile iliyowekwa na wajamaa miaka hiyo kwa kutumia 'misaada', Tunaendelea kupata misaada sijui inaishia wapi.
Kama mfumo wa Nyerere ulikuwa tegemezi wa misaada, upi ambao ni bora katika zama hizi tunazopata misaada tena ya mashirika ya kimataifa.

Kilicholetwa na waliberali ni hospitali za kulipia ambako usiku mmoja peke yake kulala ni sh 50,000 sawa na dola 30.Je anayeishi kwa dola 2 kwa siku anafaidika vipi na hali hiyo.
 
Wanabodi hongereni sana kwa mada nzuri iliyosheheni hoja za masingi sana katika kuendeleza sekta hii nyeti ya afya hapa nchini.

ningepehnda kukubaliana na hoja za kila mmoja aliyechangia nikiutambua mchango wa mtoa mada Mchambuzi, na wachangiaji waliofuata kama ifuatavyo EMT, Zakumi, Bongolander MpigaKelele, na Nguruvi3

naomba sasa nije kwenye hoja ambayo mie naona kwamba haijaguswa na wachangiaji wengi.

ni kweli nakubali kwamba madaktari ni wachache sana wanaofika hatua ya kufanya kazi kama MADAKTARI na badala yake wengi hukimbilia kwenye greener pastures.

SWALA HILI KWA nchi yetu ni kubwasana na hili siwez sana kulaumu manake halitofautiani sana la waalimu.

sasa hoja ya msingi hapa ni ipi? je serikali iendelee kuona hali ikiendelea?? je ni kweli kwamba mishahara ya watumimish hawa ni midogo kiasi cha kukimbia fani hiyo? je mishahara yao haitoshi? na je kuikim,bnia fani ama kukataa kwenye kufanya kazi kwenye mazingira magumu ndio suluhu??

mie nafikiri kwa upande huu wanabodi wenzangu hakuna uzalendo, kama ilivyo kwamba watumish wengi wa serikali hawana uzalendo basi ndivyo ilivyo kwa watumish wa kada hii.

tujiulize hivi nurses wao je wanaish vipi? mbona tunawaona wakijituma katika amzingara magumu zaid? mbona hawa madakktari wao hawawatetei hawa manesi?? (sio hoja ya msingi sana hii)

Siku hizi kuna kitu kimeibuka ambacho (hata mimi ni mhanga wake.....lol) wengi wa madaktari wamebaki kuwa ni watu ambao ni ma admin kwenye vyama mbalimbali na hivyo kupunguza idadi ya madaktari wanaowajibika kwa siku. wengi wamekuwa ni watu wa kufanya tafiti tena tafuiti ambazo ni social zaid kuliko za medcs, wengi wamekuwa ni watu wa kusafiri kwenye warsha na masemina kila siku wanabadili ticket na flights kwenye airports.

kwa namna hii je unategemea ukute madaktari wa kutiosha?

sipingani na warsha wala masemina lkn nenda mahosipitali kuta miradi ya jphgo, kuta miradi ya diabetes, afya ya kinywa etc madaktari ndio wanayoangaika nayo na sio watu wengine muda wa kukaa kuangalia wagonjwa watapata wapi??
 
Mkuu hapa yote uliyosema ni kweli. Lakini mimi ntarudi kule kule, nani mwenye uwezo wa kuwawajibisha madakatari hao? Kimsingi hakuna, kwa kuwa madaktari wanaiga ya mabosi wao.

Huwezi kuwa mkatoliki kukikopo Papa, au huwezi kuwa mwislamu kuliko mtu wa Mecca. Kama serikali, waziri, mganga mkuu hawajali, dakati ni nani kuonesha kuwa anajali sana? Kimsingi ni viongozi wetu ndio waliotufikisha hapa. Hata kama daktari ana moto sana wa kufanya kazi na kukaa kuhudumia wagonjwa kwa saa 12 kwa siku, ataishia kwenda nyumbani kwa daladala, akifika nyumbani anakula chips labda tena anaishi nyumba ya kupanga.

Kama serikali ikuboresha mazingira yao, bila shaka wanaweza kujituma zaidi hata katika mazingira magumu. Tukijaribu kumjali Daktari kama mbunge, au hata kwa nusu kama ya mbunge, au hata robo tu, hali itabadilika.
 
gfsonwin,

Umejadili hoja za msingi sana post #14 ;Na swali lako la msingi halijajibiwa kwamba je, kwahiyo kama tatizo ni maslahi ya madaktari, tutaacha hali hiyo iwe ndio sababu ya kuangamiza wananchi mpaka lini?

Pia umejadili suala la msingi sana juu ya jinsi gani madaktari wanapoteza muda mwingi kwenye research;hii ni kweli, na research nyingi ni kwa maslahi ya wakubwa wa nje ili wapate funds za kuleta misaada huku, na kama unavyojua, NGO ikipata fedha, 80 percent huwa inatumika kwa administration, salaries, workshops etc, na only 20 percent ndio huwa inaenda kupambana na tatizo (umaskini, afya, elimu etc) moja kwa moja; AID industry imetengeneza mfumo wa kunufaisha wasimamizi wa hizo NGOs hapa na wenye nazo huko nje;

Tukichukulia mfano wa sekta ya afya, kuna utafiti uliofanywa na taasisi moja ya marekani iitwayo "Mckinsey (2009), na kwa mujibu wa utafiti huo, 60 percent ya muda unaotumiwa na madaktari nchini ni kwenye managerial, administration and unproductive activities, huku 40 percent ya muda wao ukitumika katika kushughulikia wagonjwa;Utafiti huu unaendana na maelezo yako mkuu gfsonwin;

Kwa mujibu wa utafiti mwingine wa "touch foundation", kufikia mwaka 2008, Tanzania ilikuwa ina jumla ya madaktari 1,339 tu; Utafiti huo unaeleza kwamba tuna upungufu wa wataalam 89,000 (wenye sifa) za kutoa huduma za msingi za afya, na hali ikiendelea kuwa hivyo, idadi hii itazidi 100,000 ifikapo mwaka 2019; tukumbuke pia kwamba Tanzania ni moja yenye nchi zenye kasi kubwa sana la ongezeko la watu duniani (we have maintained alnost 3 percent) for the past 50 years; Cha ajabu ni kwamba hatuoni seriousness ya serikali kukabiliana na suala hili, na wala suala la kuwapatia watanzania walio wengi (vijana) maisha bora; Ukweli uliopo ni kwamba tukiangalia equation ya economic growth ambayo tunaisifia sana, inachangiwa kwa kiasi kikubwa na chota chota ya rasilimali za taifa na ujenzi wa majengo ya kisasa mijini, na yote haya hayana any direct link na maisha ya watanzania walio wengi; Ukiondoa vitu hivi viwili, uchumi wenye link ya moja kwa moja na wananchi walio wengi haukui kwa zaidi ya 4%, na imekuwa hivyo tangia uhuru; Sasa ukichanganya 4% economic growth na 3% population growth, kisha ukiangalia matumizi ya serikali kuinua sekta muhimu za kuwezesha watanzania wawe productive (elimu na afya), unabaki kutikisa tu kichwa;

Pengine serikali inatumia mwanya wa takwimu nyingine kwamba: One in every five children hafiki umri wa miaka mitano (anafariki), hivyo kuhisi labda in the "long run", things will return vyenyewe to equilibrium;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Wadau,

mimi nadhani kuliangalia tatizo hili kwamba chanzo kikubwa ni maslahi duni ya madaktari ni makosa kwani tunakuwa tunatumia an atomistic approach badala ya holistic approach kwani in my very uneducated view , miaka ya nyuma, kulikuwa na tatizo la poor performance miongoni mwa watumishi wa ushuru na forodha ambapo moja ya sababu kubwa kwanini kulikuwa na low motivation na pia rushwa nyingi ilitajwa kwamba ni maslahi kidogo; Reforms zilizofuatia ambazo ndio zikazaa TRA in the 1990s zilitarajiwa kutatua tatizo hili; Je, tunaweza sema kwamba TRA imebadilika sasa na inakidhi mahitaji yanayotarajiwa na watanzania walio wengi baada ya reforms kufanyika, hasa kuboresha maslahi ya watumishi wa TRA? Hoja yangu ya msingi ni kwamba kuna tatizo kubwa zaidi ya maslahi peke yake, but again, this is my very uneducated view, nasimama kupingwa kwa hoja;
MpigaKelele, Bongolander, gfsonwin, Nguruvi3, EMT
 
Last edited by a moderator:
Ningependa kujadili michango ya wadau mbalimbali kama ifuatavyo:

Mwisho ni hoja ya Zakumi kwamba hakuna incentives za madaktari kuhamia vijijini. Nakubalia na msingi wa hoja hii lakini solutions unazoleta kwa kweli zinashangaza kidogo; Kama nimekusoma vizuri mkuu Zakumi, unashauri kwamba tuje na sera za kuhimiza urbanization ili wananchi walio mbali na maeneo yenye huduma nzuri za afya (yani vijijini) waweze kuhamia karibu na sehemu zenye huduma hizi (mijini), seriously? Is it that simple? Hivi tunavyozungumza, tayari miji mingi inalemewa na kasi ya urbanizasation na kupelekea uhaba wa huduma nyingi za msingi, hali inayochangia kushamiri kwa umalaya, ujambazi, machafuko ya kisiasa kutokana na umaskini n.k. Sasa badala ya wewe kuhimiza turudi kwenye drawing board na kuangalia tufanikishe vipi rural development, wewe unaona solution is to encourage urbanization!? Kwa mtazamo wako, ina maana kwamba 70% of the population ambayo ipo vijijini ihamie kule ilipo 30% of the population, and then things will return to equilibrium.

Mkuu@zakumi, takwimu za afya zinatuonyesha kwamba miji iliyo mingi ina ratio kubwa sana ya patient to doctor, mfano Mara, the ratio is 1:300,000, Kigoma, the ratio is 1:160,000 and so forth and so forth, kwahiyo kwa mtazamo wako, solution ni kuhamishia wakazi wa vijiji vya maeneo haya waende mijini (Kigoma mjini, Musoma mjini)?

Cc Nguruvi3, Kichuguu, Zinedine, Mkandara, zumbemkuu, JingalaFalsafa, gfsonwin

Mchambuzi;

Mchambuzi;
Hapa tunazungumzia madaktari na huduma wanazotoa vijijini. Ukweli wa mambo, hili daktari wafanye kazi vizuri ni lazima sekta zingine za jamii ziwe nzuri. Na hili daktari afanye kazi vizuri ni lazima awe karibu anaofanana nao kiutaalamu. Na hii sio kwa daktari bali kwa watu wa fani zingine pia.

Kwanini msanii wa bongo flava aishi DSM na sio Mpindimbi. Kwa sababu atakuwa karibu watu wa fani yake. Kwa sababu wagonjwa wengi wako vijijini haina sababu madaktari waende vijijini. Kwanini wanasiasa hawahamii Dodoma?

Siasa za Tanzania ni kufikiri kuwa unaweza kum-train miracle worker ambaye anaweza kwenda kuleta maendeleo vijijini. Nchi imejaribu hivyo kwa miaka 50 na haiwezekani.

Kwanini tuseme madaktari wanatelekeza wananchi vijijini? Kwanini hatusemi wabunge wanatelekeza wananchi vijijini? Fani yako Mchambuzi inatakiwa kuleta maendeleo vijijini. Kwanini husemi unatelekeza wananchi vijijini? To single out madaktari ni kuwa wanafiki.

Chuo cha kilimo cha Sokoine kinatoa wataalamu wengi tu. Je wanakwenda vijijini? Hapana. Je wanawatelekeza wanavijiji kama madaktari? Ndio.

Sekta ya afya invokes political emotions. Lakini wanachofanya madaktari kinachangiwa na movement of labour.
Kama kila mkoa wa Tanzania utakuwa na angalau urban center moja au mbili ambazo zitavutia top talents kukaa katika centers hizo, madaktari na talents zingine zitavutiwa kwenda kwenye miji hiyo na kufanya huduma kuwa karibu na wananchi.

Urbanization sio inayochangia umalaya, ujambazi, and political unrests. Kinachochangia ni miundo mibaya ya uchumi. Ukikataa kufanya urbanization na kuwapelekea watu huduma nzuri za afya, utaongeza wastani wa maisha na idadi ya watu. Hii pekee yake ni chanzo cha urbanization. Kuna vijiji vingi Tanzania watu wanaishi kimjini lakini hawana mazingira ya kimji.

Vilevile huwezi kukwepa urbanization. Mabadiliko ya hali ya hewa yamefanya vijana wengi kuacha shughuli za vijijini na kuanza kutafuta kazi kuajiriwa. Chukua mfano kazi za ulinzi. Miaka ya zamani wamasai wengi walikuwa wachungaji. Sasa hivi vijana wengi wako happy kufanya kazi za ulinzi.
 
Mchambuzi;

Mchambuzi;
Hapa tunazungumzia madaktari na huduma wanazotoa vijijini. Ukweli wa mambo, hili daktari wafanye kazi vizuri ni lazima sekta zingine za jamii ziwe nzuri. Na hili daktari afanye kazi vizuri ni lazima awe karibu anaofanana nao kiutaalamu. Na hii sio kwa daktari bali kwa watu wa fani zingine pia.

Hili nakubaliana na wewe ndio maana hapo juu kuna sehemu nimejadili juu ya umuhimu wa mikakati kuwa more holistic, sio kuangalia tu kwamba solution ni good salaries as a motivation of performance;sina maana kwamba good salaries sio kigezo muhimu, bali yapo masuala mengine nje ya good pay yanayochangia motivation;

Kwanini msanii wa bongo flava aishi DSM na sio Mpindimbi. Kwa sababu atakuwa karibu watu wa fani yake. Kwa sababu wagonjwa wengi wako vijijini haina sababu madaktari waende vijijini. Kwanini wanasiasa hawahamii Dodoma?

Katika hili, ina maana tunakubaliana kwamba huduma ya afya imepewa zaidi market value kuliko social value katika nyakazi hizi tofauti na kipindi cha nyuma;Katika hili nikahoji, je kwanini liberalisation, marketization and privatization haven't delivered to the poor in the post 1985 period? Tufanye nini ili hali ibadilike?

Kuhusu swali lako kwanini wanasiasa hawakai dodoma, sidhani kama ni kosa lao bali la serikali hasa in the post ujamaa period;kwa mfano, nchi nyingi zinazoendelea ziliweka jitiada za dhati kuhamisha makao makuu ya nchi na uamuzi huo trickled down kwenye kila taasisi ya ndani na ya nje kwani governments had political will; Kwetu Tanzania, nilipoona tu balozi mpya za marekani, EU, UAE etc zinajengwa DSM nikajua kwamba serikali haina mpango wa dhati wa kuhamia dodoma, vinginevyo tungeona balozi hizi zikihamia dodoma, tazama miji mikuu mingi mipya ya nchi zinazoendelea, balozi nyingi zimefuata serikali;

Siasa za Tanzania ni kufikiri kuwa unaweza kum-train miracle worker ambaye anaweza kwenda kuleta maendeleo vijijini. Nchi imejaribu hivyo kwa miaka 50 na haiwezekani.
Kwanini tuseme madaktari wanatelekeza wananchi vijijini? Kwanini hatusemi wabunge wanatelekeza wananchi vijijini?

Kutofanikiwa kwa miaka 50 haina maana kwamba haiwezekani;and in actual semse, jitiada hazijawa kwa miaka 50 but less (wakati wa nyerere);mimi nakumbuka wakati ule, mzazi wangu alikuwa anafanya kazi mikoani kama RDD, na katika mikoa yote tuliyoishi, nakumbuka maafisa mbalimbali walikuwa wanafurahia kabisa maisha ya kuishi nje ya Dar-es-salaam;nadhani dhana ya decentralisation kimaamuzi na kifedha ikihimizwa, itabadilisha mambo mengi;vinginevyo katika hali ya sasa, dhana ya decentralisation ni nadharia zaidi, maamuzi ya kifedha yanashikiliwa dar-es-salaam, na hata bungeni kila siku tunasikia kwamba hata nusu ya fedha za bajeti hazijafika huko chini wakati ni miezi michache tu imebakia kabla ya ujio wa mwaka mpya wa fedha;

Fani yako Mchambuzi inatakiwa kuleta maendeleo vijijini. Kwanini husemi unatelekeza wananchi vijijini? To single out madaktari ni kuwa wanafiki.

Kwa ufupi wa kamba yangu mkuu Zakumi, najitahidi sana kuelewa matatizo ya msingi ya wanavijiji kwani ni jadi yangu kwenda maeneo mbalimbali kwa gharama zangu mwenyewe kwenda fanya tafiti ndogo ndogo, hasa kuishi na wananchi na kujionea first hand;nimeenda sana singida, arusha, mbeya, na nikifanikiwa zaidi, nitaenda maeneo mengine zaidi;

Chuo cha kilimo cha Sokoine kinatoa wataalamu wengi tu. Je wanakwenda vijijini? Hapana. Je wanawatelekeza wanavijiji kama madaktari? Ndio.

Katika mjadala wetu mwingine nadhani unakumbuka kwamba Nguruvi3 alilijadili hili la SUA vizuri sana;hoja yake ya msingi ni kwamba serikali ikiamua kwa mfano kuondoa porojo za kilimo kwanza BUNGENI na kuzipeleka SUA na pakawekwa performance indicators na targets, mabadiliko sekta ya kilimo yatakuja;vinginevyo sio kwamba wataalam wa kilimo nchini hawajui tatizo nini, wanajua, na wameandika volumes and volumes of reports, lakini zinaishia kuliwa na mende kwenye makabati serikalini;

Sekta ya afya invokes political emotions. Lakini wanachofanya madaktari kinachangiwa na movement of labour.
Kama kila mkoa wa Tanzania utakuwa na angalau urban center moja au mbili ambazo zitavutia top talents kukaa katika centers hizo, madaktari na talents zingine zitavutiwa kwenda kwenye miji hiyo na kufanya huduma kuwa karibu na wananchi.
Definition yako ya urban center ni nini? Eneo husika kufikia hadhi ya manispaa?kama jibu ni ndio, mbona zipo nyingi tu leo?
Kama jibu ni hapana, what's your definition?
Urbanization sio inayochangia umalaya, ujambazi, and political unrests. Kinachochangia ni miundo mibaya ya uchumi.

Haukunisoma vizuri katika hili kwani unachosema ndicho nilichosema;

Ukikataa kufanya urbanization na kuwapelekea watu huduma nzuri za afya, utaongeza wastani wa maisha na idadi ya watu. Hii pekee yake ni chanzo cha urbanization. Kuna vijiji vingi Tanzania watu wanaishi kimjini lakini hawana mazingira ya kimji.

Nadhani hapa ukifafanua zaidi utanisaidia majibu kwa swali langu kwako hapo juu kuhusiana na your definition of "an urban center"

Vilevile huwezi kukwepa urbanization. Mabadiliko ya hali ya hewa yamefanya vijana wengi kuacha shughuli za vijijini na kuanza kutafuta kazi kuajiriwa. Chukua mfano kazi za ulinzi. Miaka ya zamani wamasai wengi walikuwa wachungaji. Sasa hivi vijana wengi wako happy kufanya kazi za ulinzi.

Ni kweli, urbanisation ni phenomenon ambayo ni unavoidable, kwani hata China hili ni tatizo, na halitokani na mabadiliko ya tabia nchi tu bali pia structural transformation;je sisi Tanzania, is there a structural transformation taking place?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wanabodi hongereni sana kwa mada nzuri iliyosheheni hoja za masingi sana katika kuendeleza sekta hii nyeti ya afya hapa nchini.

ningepehnda kukubaliana na hoja za kila mmoja aliyechangia nikiutambua mchango wa mtoa mada Mchambuzi, na wachangiaji waliofuata kama ifuatavyo EMT, Zakumi, Bongolander MpigaKelele, na Nguruvi3

naomba sasa nije kwenye hoja ambayo mie naona kwamba haijaguswa na wachangiaji wengi.

ni kweli nakubali kwamba madaktari ni wachache sana wanaofika hatua ya kufanya kazi kama MADAKTARI na badala yake wengi hukimbilia kwenye greener pastures.

SWALA HILI KWA nchi yetu ni kubwasana na hili siwez sana kulaumu manake halitofautiani sana la waalimu.

sasa hoja ya msingi hapa ni ipi? je serikali iendelee kuona hali ikiendelea?? je ni kweli kwamba mishahara ya watumimish hawa ni midogo kiasi cha kukimbia fani hiyo? je mishahara yao haitoshi? na je kuikim,bnia fani ama kukataa kwenye kufanya kazi kwenye mazingira magumu ndio suluhu??

mie nafikiri kwa upande huu wanabodi wenzangu hakuna uzalendo, kama ilivyo kwamba watumish wengi wa serikali hawana uzalendo basi ndivyo ilivyo kwa watumish wa kada hii.

tujiulize hivi nurses wao je wanaish vipi? mbona tunawaona wakijituma katika amzingara magumu zaid? mbona hawa madakktari wao hawawatetei hawa manesi?? (sio hoja ya msingi sana hii)

Siku hizi kuna kitu kimeibuka ambacho (hata mimi ni mhanga wake.....lol) wengi wa madaktari wamebaki kuwa ni watu ambao ni ma admin kwenye vyama mbalimbali na hivyo kupunguza idadi ya madaktari wanaowajibika kwa siku. wengi wamekuwa ni watu wa kufanya tafiti tena tafuiti ambazo ni social zaid kuliko za medcs, wengi wamekuwa ni watu wa kusafiri kwenye warsha na masemina kila siku wanabadili ticket na flights kwenye airports.

kwa namna hii je unategemea ukute madaktari wa kutiosha?

sipingani na warsha wala masemina lkn nenda mahosipitali kuta miradi ya jphgo, kuta miradi ya diabetes, afya ya kinywa etc madaktari ndio wanayoangaika nayo na sio watu wengine muda wa kukaa kuangalia wagonjwa watapata wapi??

gfsonwin:

Kwa maoni yangu, suala hili ni sawa na masuala mengine. Huwezi kufanikiwa katika sekta ya afya kama unaboronga katika sekta zingine kama vile za uzalishaji, usafiri n.k

Kuhusiana na swali lako, kuna ukweli kuwa nchi yetu ni kubwa. Na matatizo mengine yanatokana na ukubwa wa nchi. Nchi kama Rwanda ni compact. Barabara ya kukatiza mkoa mmoja wa Tanzania itakuwa imekatiza Rwanda nzima. Hivyo centralized approach inayofuatwa na serikali ya Tanzania kwa kuiga western democracy haina ufanisi.

Labda serikali za majimbo zenye nguvu zinaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa sababu majimbo yatakuwa compact.
 
Back
Top Bottom