Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
- Thread starter
- #21
Mchambuzi;
Mchambuzi;
Hapa tunazungumzia madaktari na huduma wanazotoa vijijini. Ukweli wa mambo, hili daktari wafanye kazi vizuri ni lazima sekta zingine za jamii ziwe nzuri. Na hili daktari afanye kazi vizuri ni lazima awe karibu anaofanana nao kiutaalamu. Na hii sio kwa daktari bali kwa watu wa fani zingine pia.
Hili nakubaliana na wewe ndio maana hapo juu kuna sehemu nimejadili juu ya umuhimu wa mikakati kuwa more holistic, sio kuangalia tu kwamba solution ni good salaries as a motivation of performance;sina maana kwamba good salaries sio kigezo muhimu, bali yapo masuala mengine nje ya good pay yanayochangia motivation;
Kwanini msanii wa bongo flava aishi DSM na sio Mpindimbi. Kwa sababu atakuwa karibu watu wa fani yake. Kwa sababu wagonjwa wengi wako vijijini haina sababu madaktari waende vijijini. Kwanini wanasiasa hawahamii Dodoma?
Katika hili, ina maana tunakubaliana kwamba huduma ya afya imepewa zaidi market value kuliko social value katika nyakazi hizi tofauti na kipindi cha nyuma;Katika hili nikahoji, je kwanini liberalisation, marketization and privatization haven't delivered to the poor in the post 1985 period? Tufanye nini ili hali ibadilike?
Kuhusu swali lako kwanini wanasiasa hawakai dodoma, sidhani kama ni kosa lao bali la serikali hasa in the post ujamaa period;kwa mfano, nchi nyingi zinazoendelea ziliweka jitiada za dhati kuhamisha makao makuu ya nchi na uamuzi huo trickled down kwenye kila taasisi ya ndani na ya nje kwani governments had political will; Kwetu Tanzania, nilipoona tu balozi mpya za marekani, EU, UAE etc zinajengwa DSM nikajua kwamba serikali haina mpango wa dhati wa kuhamia dodoma, vinginevyo tungeona balozi hizi zikihamia dodoma, tazama miji mikuu mingi mipya ya nchi zinazoendelea, balozi nyingi zimefuata serikali;
Siasa za Tanzania ni kufikiri kuwa unaweza kum-train miracle worker ambaye anaweza kwenda kuleta maendeleo vijijini. Nchi imejaribu hivyo kwa miaka 50 na haiwezekani.
Kwanini tuseme madaktari wanatelekeza wananchi vijijini? Kwanini hatusemi wabunge wanatelekeza wananchi vijijini?
Kutofanikiwa kwa miaka 50 haina maana kwamba haiwezekani;and in actual semse, jitiada hazijawa kwa miaka 50 but less (wakati wa nyerere);mimi nakumbuka wakati ule, mzazi wangu alikuwa anafanya kazi mikoani kama RDD, na katika mikoa yote tuliyoishi, nakumbuka maafisa mbalimbali walikuwa wanafurahia kabisa maisha ya kuishi nje ya Dar-es-salaam;nadhani dhana ya decentralisation kimaamuzi na kifedha ikihimizwa, itabadilisha mambo mengi;vinginevyo katika hali ya sasa, dhana ya decentralisation ni nadharia zaidi, maamuzi ya kifedha yanashikiliwa dar-es-salaam, na hata bungeni kila siku tunasikia kwamba hata nusu ya fedha za bajeti hazijafika huko chini wakati ni miezi michache tu imebakia kabla ya ujio wa mwaka mpya wa fedha;
Fani yako Mchambuzi inatakiwa kuleta maendeleo vijijini. Kwanini husemi unatelekeza wananchi vijijini? To single out madaktari ni kuwa wanafiki.
Kwa ufupi wa kamba yangu mkuu Zakumi, najitahidi sana kuelewa matatizo ya msingi ya wanavijiji kwani ni jadi yangu kwenda maeneo mbalimbali kwa gharama zangu mwenyewe kwenda fanya tafiti ndogo ndogo, hasa kuishi na wananchi na kujionea first hand;nimeenda sana singida, arusha, mbeya, na nikifanikiwa zaidi, nitaenda maeneo mengine zaidi;
Chuo cha kilimo cha Sokoine kinatoa wataalamu wengi tu. Je wanakwenda vijijini? Hapana. Je wanawatelekeza wanavijiji kama madaktari? Ndio.
Katika mjadala wetu mwingine nadhani unakumbuka kwamba Nguruvi3 alilijadili hili la SUA vizuri sana;hoja yake ya msingi ni kwamba serikali ikiamua kwa mfano kuondoa porojo za kilimo kwanza na kuzipeleka SUA na pakawekwa performance indicators na targets, mabadiliko sekta ya kilimo yatakuja;vinginevyo sio kwamba wataalam wa kilimo nchini hawajui tatizo nini, wanajua, na wameandika volumes and volumes of reports, lakini zinaishia kuliwa na mende kwenye makabati serikalini;
Definition yako ya urban center ni nini? Eneo husika kufikia hadhi ya manispaa?kama jibu ni ndio, mbona zipo nyingi tu leo?Sekta ya afya invokes political emotions. Lakini wanachofanya madaktari kinachangiwa na movement of labour.
Kama kila mkoa wa Tanzania utakuwa na angalau urban center moja au mbili ambazo zitavutia top talents kukaa katika centers hizo, madaktari na talents zingine zitavutiwa kwenda kwenye miji hiyo na kufanya huduma kuwa karibu na wananchi.
Kama jibu ni hapana, what's your definition?
Urbanization sio inayochangia umalaya, ujambazi, and political unrests. Kinachochangia ni miundo mibaya ya uchumi.
haukunisoma vizuri katika hili kwani unachosema ndicho nilichosema;
Ukikataa kufanya urbanization na kuwapelekea watu huduma nzuri za afya, utaongeza wastani wa maisha na idadi ya watu. Hii pekee yake ni chanzo cha urbanization. Kuna vijiji vingi Tanzania watu wanaishi kimjini lakini hawana mazingira ya kimji.
Nadhani hapa ukifafanua zaidi utanisaidia majibu kwa swali langu kwako hapo juu kuhusiana na your definition of "an urban center"
Vilevile huwezi kukwepa urbanization. Mabadiliko ya hali ya hewa yamefanya vijana wengi kuacha shughuli za vijijini na kuanza kutafuta kazi kuajiriwa. Chukua mfano kazi za ulinzi. Miaka ya zamani wamasai wengi walikuwa wachungaji. Sasa hivi vijana wengi wako happy kufanya kazi za ulinzi.
Ni kweli, urbanisation ni phenomenon ambayo ni unavoidable, kwani hata China hili ni tatizo, na halitokani na mabadiliko ya tabia nchi tu bali pia structural transformation;je sisi Tanzania, is there a structural transformation taking place?
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Last edited by a moderator: