UTAFITI: Marais Wanawake waongoza kudhibiti maambukizi ya COVID19 duniani

UTAFITI: Marais Wanawake waongoza kudhibiti maambukizi ya COVID19 duniani

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Tofauti na matarajio ya wengi, utafiti uliofanywa na Shirika la Centre for Economic Policy Research na Jarida la World Economic Forum umebaini kuwa mataifa yanayoongozwa na wanawake yana kiwango kidogo cha maambukizi na athari zinazotokana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu, COVID-19, ukilinganisha na mataifa yanayoongozwa na wanaume

Utafiti huo uliozihusisha nchi 194 kote duniani umeonesha tofauti kubwa baina ya mataifa 19 yanayoongozwa na wanawake na yale yanayoongozwa na wanaume katika mbinu zilizotumika kukabiliana na athari za maambukizi ya corona

Viongozi wanawake walionekana kuchukua hatua za haraka zaidi ikiwamo kuweka katazo la kutokutoka nje hivyo kupunguza idadi ya watu waliopoteza maisha licha ya athari za kiuchumi zilizojitokeza

Utafiti huo umelinganisha mataifa mbalimbali kwa vigezo mbalimbali ikiwamo idadi ya watu, ukuaji wa kiuchumi na mlinganyo wa wazee katika jamii, kiwango cha matumizi ya fedha za matibabu kwa mtu mmoja mmoja , pamoja na usawa wa kijinsia

Kutokana na uchache mataifa yanayoongozwa na wanawake, watafiti wamelinganisha mataifa hayo kwa kuangalia vigezo vinavyofanana kwa ukaribu baina ya nchi zinazoongozwa na wanawake, mataifa ya Ujerumani, New Zealand na Bangladesh yakilinganishwa na mataifa yanayoongozwa na wanaume ya Uingereza, Ireland na Pakistan

Watafiti wanaamini kuwa utafiti huo utasaidia kuibua mijadala kuhusu ushawishi wa viongozi wa nchi katika kukabiliana na athari za maambukizi ya virusi vya corona

Chanzo: Female-led countries handled coronavirus better, study suggests
 
Kwahiyo Magu nae ni miongoni mwa mademu? 😃😃
 
... feminism at work ... Kwani hao marais wanawake wanajiamulia wapendavyo au wana washauri kwenye sekta mbalimbali waliosaidia kufanikisha malengo? Kwamba hakuna nchi zinazoongozwa na wanaume ambazo zimefanikisha vita?
 
Back
Top Bottom