UTAFITI: Mgodi Petra washutumiwa kupiga watu risasi na kuua, kuendesha kituo cha utesaji mgodini na kuwafunga pingu wagonjwa hospitali ya Mwadui

UTAFITI: Mgodi Petra washutumiwa kupiga watu risasi na kuua, kuendesha kituo cha utesaji mgodini na kuwafunga pingu wagonjwa hospitali ya Mwadui

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Taarifa ya RAID, shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake nchini Uingereza ambalo linajishughulisha na kufichua ukiukwaji wa haki za binadamu, limebaini kutendeka kwa vitendo vya kidhalimu katika Mgodi wa Petra Diamonds uliopo Shinyanga

Kwa mujibu wa taarifa yake, shirika hilo limefanya utafiti huo tangu Septemba 2019, kufuatia taarifa kutoka kwa NGO's zingine za kimataifa na wanaharakati wa ndani.

Aidha, utafiti huo umehusisha mahojiano zaidi ya 100 na wakazi wa eneo hilo, wanachama wa asasi za kiraia, mamlaka za mitaa, wafanyakazi wa afya, waandishi wa habari na wafanyakazi wa zamani wa usalama walioajiriwa katika mgodi huo.

RAID imeeleza kuwa utafiti unaibua wasiwasi mkubwa kuhusu masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu, na hivyo tayari wamewasiliana na Petra Diamonds mnamo 29 Agosti ili kueleza wasiwasi wao ikiwa ni pamoja na kuuliza mfululizo wa maswali.

RAID wanatarajia kuwa na mikutano zaidi na kampuni hiyo na kwamba hivi karibuni watachapisha ripoti kamili inayoelezea matokeo kamili ya utafiti huo.

Hata hivyo, masuala ambayo utafiti huo umebaini ni pamoja na:

# Matumizi ya risasi dhidi ya binadamu, vipigo pamoja na mashambulizi mengine, ikiwa ni pamoja na yanayowahusu watoto, yanavyotekelezwa na wafanyakazi wa usalama walioajiriwa na kampuni hiyo na kusababisha majeraha mabaya na vifo. Shirika la RAID limepokea ripoti za mauaji yasiyopungua 7 (kati yao, 2 walikuwa chini ya umri wa miaka 18) na mashambulio 35 yakiwemo ya kupiga risasi, kupiga, na kutesa tangu Petra ilipopata mgodi mnamo 2009. Waathirika wengi wameelezwa kupata majeraha ya kubadilisha maisha. Mgodi huo unatumia kampuni ya Zenith Security, ambayo ni ya Kitanzania, kutoa huduma za kiusalama.

# Mateso na ukatili, udhalilishaji na matendo yasiyo ya kibinadamu katika mahabusu binafsi kwenye Mgodi wa Williamson. RAID pia lilipokea ripoti nyingi za wachimbaji ambao walishikiliwa, kupigwa na wakati mwingine kuteswa. Wengi walishikiliwa kwa siku kadhaa kabla ya kuhamishiwa kwa vyombo vya sheria vya serikali. Walioshikiliwa walielezea kuwa mahabusu ya kampuni hiyo imejaa watu wengi na kuna uchafu na ukosefu wa chakula.

# Wachimbaji wanaopigwa, kupigwa risasi au kujeruhiwa katika Mgodi wa Williamson mara nyingi hupelekwa katika Hospitali ya kampuni ya Mwadui iliyodhibitiwa ndani ya eneo la Mgodi. Shirika la RAID lilipokea ripoti 7 za wahanga waliofungwa minyororo kwenye vitanda vya hospitali na/au kufungwa pamoja na wafungwa wengine wakiwa katika hospitali hiyo. Waathiriwa wengine walisema walinyimwa kupata rekodi zao za matibabu.

RAID pia imechapisha ukosefu wa ushirikishaji kati ya mgodi na jamii. Wengi ya waliohojiwa wamesema hawajui jinsi ya kufikisha malalamiko yao mgodini na pia hugopa ulipizaji kisasi kama wakifanya hivyo. Wachache waliosema walifikisha malalamiko yao, wameeleza hatua ndogo kuchukuliwa au kutochuliwa hatua yoyote kabisa.
========

RAID statement on its research at Petra Diamonds' Williamson Mine in Tanzania

This statement is published in response to a press release by Petra Diamonds on 9 September informing its shareholders of a legal claim by UK lawyers, Leigh Day, on behalf of human rights victims and a letter RAID sent to the company on August 29 raising further human rights concerns. RAID is a UK based non-governmental organisation that exposes corporate abuses and human rights violations, partnering with those harmed to hold companies to account. We have been researching human rights issues at Petra Diamonds’ Williamson Mine since September 2019, following alerts by other international NGOs and local activists.

RAID's research is based on over 100 interviews with local residents, members of local civil society, local authorities, medical staff, journalists and former security personnel employed at Williamson Mine. Our research raises serious human rights concerns. We contacted Petra Diamonds on 29 August to share our concerns and asked for responses to a series of questions. We hope to have further meetings with the company and will shortly be publishing a full report detailing our findings.

The issues our research uncovered are alarming. They include:
  • Shootings, beatings and other assaults, including of children, by security personnel employed by the company on and around the Williamson Mine, causing serious injuries and death. RAID has received reports of at least 7 killings (of which 2 were under the age of 18) and 35 assaults including shootings, beatings, and torture since Petra acquired the mine in 2009. Many incurred life changing injuries. Williamson Mine employs Zenith Security, a Tanzanian company, to provide security at the mine.
  • Torture and cruel, degrading and inhuman treatment at a private detention centre on the Williamson Mine. RAID received numerous reports of artisanal miners and others who were detained, beaten and in some cases tortured. Many were detained for days before being transferred to state law enforcement facilities. Detainees described the Williamson detention centre as overcrowded and filthy, with only a slop bucket for toilet facilities and a lack of food. At this stage RAID is unaware of any lawful basis on which Petra operates this detention centre at the Williamson Mine.
  • Artisanal miners and others beaten, shot or otherwise injured at the Williamson Mine are often taken to company controlled Mwadui Hospital within the Williamson Mine site. RAID received at least 7 reports of victims being chained to hospital beds and/or chained to other detainees while in Mwadui Hospital. Some victims said they were denied access to their medical records.
RAID also documented a lack of engagement by the Mine with local communities. The vast majority of those interviewed stated that they did not know how they could raise concerns with the Mine, and many said they feared retribution if they did. The few who said that they had raised concerns stated that little or no helpful action was taken in response.

Threats to, and harassment and/or intimidation of human rights defenders, local journalists, and other local residents, including by police and/or local authorities, were also reported to our researchers. Such conduct appears to have escalated since RAID’s first mission in November 2019 and has targeted those who met with us and/or lawyers from Leigh Day, a UK law firm. Leigh Day works independently from RAID and have also been following-up on reports of human rights abuses. Petra Diamonds should use its leverage with authorities to seek to prevent such harassment.

“Petra Diamonds decision to inform its board and shareholders about the serious allegations is only a first step,” said Anneke Van Woudenberg, the Executive Director at corporate watchdog RAID. “The company’s investigation into these serious allegations should be thorough, independent and transparent. Petra should work with appropriate authorities to ensure those responsible for any crimes are held to account and provide effective remedy to all those who suffered harm or lost loved ones.”

“Petra’s claim that its diamonds are ethical is meaningless if it does not clearly demonstrate that it has resolved these very serious human rights concerns and takes urgent steps to halt such abuses from happening again,” Van Woudenberg said.
Full statement is also available here.

Source: RAID statement on its research at Petra Diamonds' Williamson Mine in Tanzania
 
The Sherrif, just mind your own life and move. There is nothing you can do
 
If at all these claims by RAID are true then I don’t think it’s wise to advice Petra to self check!

Kesi ya ngedere kupelekewa Nyani, hakuna suluhisho litapatikana!
 
Taarifa hii imechapishwa ikiwa ni majibu ya taarifa kwa umma ilitolewa na Petra Diamonds Septemba 9 ikiwajulisha wanahisa wake juu ya malalamiko ya kisheria kutoka kwa mawakili wa Kiingereza, Leigh Day ikiwakilisha watetezi wa haki za binadamu na barua ambayo RAID iliitumia kampuni hiyo Agosti 29 ikiendelea kuwajulisha wasiwasi wao juu ya haki za kibinadamu.

RAID ni taasisi isiyo ya kiserikali nchini Uingereza ambayo huyaanika mashirika ambayo yananyanyasa na kukiuka haki za binadamu ikishirikiana na waliodhuriwa ili wahusika wawajibike. Imekuwa ikitafiti haki za binadamu katika mgodi wa Petra kutoka September 2019 kutokana na tahadhari zilizotolewa na taasisi nyingine zisizo za kiserikali za kimataifa na wanaharakati wa ndani.

Utafiti wa RAID umehusisha mahojiano na wakazi 100, taasisi za kijamii, mamlaka, wahudumu wa afya, wanahabari na walinzi ambao wamewahi kuajiriwa kwenye mgodi wa Williamson. Utafiti wetu umeibua wasiwasi mkubwa juu ya haki za binadamu na kuwasiliana na Petra Agosti 29 kuwashirikisha wasiwasi wetu na kuomba majibu. Inatarajia mikutano zaidi na kampuni husika na kuchapisha ripoti nzima ikielezea kwa kina matokeo.

Masuala yaliyoshtua kwenye utafiti wetu yanajumuisha
  • Upigaji risasi, kupigwa na mashambulio mengine yanayojumuisha watoto kutoka kwa walinzi waliojiriwa na kampuni hiyo ndani na kuzunguka mgodi na kusababisha maumivu makubwa na vifo. RAID imepata ripori ya mauaji si chini ya watu saba ikiwemo wawili wenye umri chini ya miaka 18 na mashambulio 35 upigaji risasi, upigaji na utesaji tangu Petra imiliki mgodi huo 2009 wengi wakipata vilema vya kudumu. Mgodi wa Williamson umeipa kandarasi kampuni ya ulinzi ya Zenith, kampuni ya kitanzania kutoa huduma ya ulinzi mgodini.
  • Utesaji na ukatili,udhalilishaji, matendo yasiyo ya kibinadamu kwenye kituo binafsi cha kushikilia watu mgodini. RAID imepokea ripoti mbalimbali kutoka kwa wachimbaji na wengine waliowekwa kizuizini mgodini, kupigwa na kuteswa, wengi wakishikiliwa kwa masiku kadhaa kabla ya kufikishwa kwenye mamlaka za serikali. Wanaoshikiliwa wanaelezea kituo cha kushikilia watu mgodi kina msongamano mkubwa na kichafu kikiwa na ndoo pekee kujisaidia na ukosefu wa chakula. Mpaka sasa RAID haijui kama kituo cha kushikilia watu ndani ya mgodi kama kipo kisheria.
  • Wachimbaji na wengine wanaopigwa na kuumizwa ndani ya mgodi wanapelekwa kwenye hospitali inayoyodhibitiwa na mgodi ndani ya eneo la mgodi. RAID imepokea si chini ya ripoti saba juu ya waathirika waliofungwa pingu kwenye vitanda vya hospitali au/ na kwa waathirika wengine hospitalini hapo. Baadhi walisema wamezuiwa kupewa rekodi zao za matibabu.
RAID pia imechapisha ukosefu wa ushirikishaji kati ya mgodi na jamii. Wengi ya waliohojiwa wamesema hawajui jinsi ya kufikisha malalamiko yao mgodini pia hugopa ulipizaji kisasi kama wakifanya. Wachache waliosema walifikisha malalamiko yao hatua ndogo zilichukuliwa au kutochuliwa hatua yoyote kabisa.
 
Mtu mweusi anapojipendekeza kwa mweupe mwenye pesa. Ushamba na ulimbukeni sijui utaishia lini?
 
Kiukweli katika hili la matumizi ya nguvu , kuna kitu kinaitwa PLAN= Principle+Legality+Accountability+Necessity.
Human Rights huwa inafuatwa na walinzi wote wapo very trained na wanafanya kazi kwa kuzingatia hayo, sasa hivi tusubiri uchunguzi.

Hao Raia wanaoingia mgodini kwanza wanaingia kundi kubwa sana, na huwa kundi likishawaona walinzi hao huanza kuwashambulia , muda mwingine hufunga barabara ili wasipite mwisho wa siku walinzi hutumia silaha ili wapate njia na silaha ni kitisho dhidi ya adui yeyote, wamejeruhi walinzi, wamekata mapanga walinzi, wamewahi kuua mlinzi, tukija kwa walioumia kazini WCF analitambua hilo na wengi wanafungua madai yao walipwe sitahaki.

Kilichopaswa kufanyika nikutoa elimu kwa wananchi wanaouzunguka mgodi ili wajue kabisa kuingia kwenye himaya ya mtu bila ruhusa na ukafanya fujo Utapigwa tu .
 
Tanzania hii hii iliyobatizwa na wanaLumumba kuwa Tanzania ya Magufuli mambo haya ya mabeberu yanafanyika hapa hapa nchini chini ya vyombo vya dola na sheria vya serikali ya CCM Mpya !
 
Back
Top Bottom