3-Star General
Member
- Feb 21, 2024
- 60
- 137
Juzi nilikuwa na kazi moja kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Jiji la Arusha siku nzima. Sasa, kutokana na msongamano unaotokana na ongezeko kubwa la magari ilibidi nijipe dual-work na kufanya simple observational cross sectional study (Utafiti mdogo wa kutazama katika wakati mahususi).
Lengo: Kuangalia popular cars in Arusha mjini.
Mbinu iliyotumika: Time-based observation.
Kwamba, ni gari au magari gani yatajitokeza kwa wingi ndani ya sekunde 30, 60, 90 na 120. Zoezi hili lilifanyika kwa muda wa masaa 6 mfululizo.
Viashiria: Utambuzi wa gari kwa ngazi ya aina ya gari (Mfano: Nissan-navara au Toyota-Harrier au BMW-3series na sio just a Nissan, Toyota au BMW etc).
Matokeo: Ndani ya kila sekunde 30 angalau Toyota-Land cruiser 1 ilionekana. Hii pia imechochewa zaidi na uwepo wa land cruiser za kubeba watalii (Ambapo hii yaweza kuwa confounding factor) japo cruiser tofauti na za utalii zilijitokeza angalau moja ndani ya kila sekunde 60.
Vilevile gari zilizojitokeza angalau mbili ndani ya kila sekunde 60 ni Toyota Rav4 (model zote) na Toyota Alphard.
Ndani ya kila sekunde 90 angalau Toyota Noah moja ilionekana na ndani ya kila sekunde 120 angalau Toyota IST moja na Subaru forester moja ilionekana.
Hitimisho: Magari popular (yanayopendwa/yaliyopo kwa wingi) Jijini Arusha ni Toyota Land cruiser, Rav4, Alphard, Noah, IST na Subaru Forester. Huku Toyota Land cruiser, Rav4 na Alphard zikionekana zote ndani ya Dakika1 au mara kwa mara ukigeuka nyuzi 360 popote ulipo ndani ya Arusha Mjini. (Kama upo Ars mjini popote ulipo ukizungusha macho nyuzi 360 utajionea mwenyewe).
Athari chanya za utafiti huu: Hizo ndo the most popular cars Arusha. Hivyo, wauzaji wa magari waongeze stock za magari hayo. Wauzaji wa vipuri vya magari wafikirie kuwa na stock kubwa ya vifaa vya magari hayo as common things occur commonly.
Nb: Utafiti huu ni kwa ajili ya kushare experience tu, hakuna any conflict of interest.
Wasalaam