Utafiti tofauti ya kinga wanaoishi mijini na vijiji kufanyika

Utafiti tofauti ya kinga wanaoishi mijini na vijiji kufanyika

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Utofauti wa kinga ya mwili kati ya wanaoishi mjini na vijijini umewaibua wataalamu wa afya kuendesha utafiti ili kubaini chanzo cha tofauti hizo na kupima ufanisi wa chanjo katika maeneo hayo.

Wataalamu hao ni kutoka Taasisi ya Utafiti (KCRI), hospitali ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) pamoja na wataalamu kutoka chuo kikuu cha Leiden Nchini Uholanzi.

Akizungumza juu ya utafiti huo leo Septemba 20, 2022 mwanasayansi wa maabara kutoka KCMC, Dk Jeremia Pyuza amesema utafiti huo utafanyika katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha utakaofanyika kwa miezi 18 kuanzia Septemba 27, utatoa mwelekeo katika ugawaji wa chanjo za magonjwa mbalimbali.

"Matokeo ya utafiti huu, yanaenda kutuelekeza katika dhima kubwa kwamba je chanjo mbalimbali zinazotolewa kwa watu wa Tanzania, zinafanyaje kazi, kati ya watu wa kijijini na mjini, na kama ipo tofauti je inatafsiriwa vipi kwenye maswala ya kinga ya mwili.

"Hii inatupa picha pia kwamba je, tunatakiwa kuongeza dozi, au kubaki na dozi zilezile tunazozitumia na hii itaisaidia hata nchi kwenye matumizi ya chanjo na amesema Pyuza ugawaji wa chanjo katika maeneo mbalimbali," amesema Dk Pyuza.

Akielezea juu ya kinga ya mwili, Pyuza amesema kinga ya mwili ni uwezo wa mwili kupambana na magonjwa na vilevile uwezo wa mwili kuzuia magonjwa.

Uwezo wa kinga ya mwili unapimwa pale mtu anapopewa chanjo, lakini mtu ambaye kinga yake haipo vizuri hata anapopewa chanjo kuzalisha chembe mwili kutokana na chanjo hiyo pia unakua ni mdogo," amesema Pyuza

Naye daktari bingwa wa magonjwa ya ndani KCMC na mshiriki katika utafiti huo, Dk Elichilia Shao amesema utafiti huo utabaini chanzo cha utofauti uliopo kati ya watu wanaoishi mjini na vijijini ili kuiwezesha Serikali katika ugawaji wa chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali.

"Tunafanya hivyo kwani tunaona magonjwa yanakuja kwa namna tofauti, tumeona watu wanachanjwa lakini wanapata magonjwa, mfano ni kifua kikuu, ukiangalia kwenye mabega watu wamepata chanjo lakini pia wapo wanaougua ugonjwa huo"amesema shao na kuongeza

"Pamoja na hiyo tumeona kwenye homa ya ini, wapo watu waliopata chanjo, lakini mmoja anatengeneza kinga ya mwili kubwa zaidi kuliko mwingine ndio maana tumeamua kufanya utafiti huu ili kubaini ni nini sababu ya tofauti hii iliyopo," amesema.

Kwa uapande wake Dk Anastazia Ngowi ambaye ni Mshiriki katika utafiti huo, amesema utafiti huo ni fursa kwa jamii kwani umelenga kubaina chanzo cha tofauti katika kinga ya mwili pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya kinga ya mwili.

"Utafiti huu ni fursa kwa wanajamii yetu, utafiti huu unaenda kutoa elimu juu ya kinga ya mwili, jamii yetu inaelimishwa juu ya kinga ya mwili, namna ya kuiboresha kinga ya mwili na kinga ya mwili ni muhimu kwani inapokua bora ndiyo inakusaidia kujikinga na maradhi,” amesema Ngowi.

Mwananchi
 
Mchongo tu.

Sioni kama kuna area of study hapo
 
Tafiti zimeja kwenye maktaba zetu na vyuoni kama mlima na hatufanyii kazi tuaendelea kufanya tafiti solution ziro. xo dumb and useless
 
Back
Top Bottom