Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 1,710
- 8,690
Wasaalam ndugu wote humu.
Awali ya yote nawashukuru nyie wote kwani mmekuwa mkitoa ushirikiano mkubwa kwenye kupambana kutokomeza ukatili kwa watoto wetu miaka yote. Sasa nawaalika hapa tupate mrejesho wa kitafiti kwa ufupi kabisa kisha, tuendelee kushirikiana kuendelea na mikakati iliyoboreshwa kupitia matokeo ya utafiti huu. Ahsanteni sana🙌🙏
👇
Matokeo ya utafiti wa Machi-Juni, 2024 yanaonesha ukatili umeshuka kwa kiwango kikubwa ukilinganisha utafiti wa 2009 ambapo, KWA WATOTO WA KIKE: Ukatili wa kingono umepungua kutoka 33% hadi 11%; Ukatili wa kimwili umepungua kutoka 76% hadi 24%; na Ukatili wa kihisia umepungua kutoka 25% hadi 22%.
KWA WATOTO WA KIUME: Ukatili wa kingono umepungua kutoka 21% hadi 5%; Ukatili wa kimwili umepungua kutoka 74% hadi 21% na Ukatili wa kihisia umepungua kutoka 31% hadi 16%.
WALENGWA; Watoto 11,414 wenye umri wa miaka 13 hadi 24 kutoka mikoa yote 31 ya Tanzania Bara na Zanzibar.
WATAFITI; Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii (Tanzania Bara) na Wizara ya Maendeleo ya Jamii (Zanzibar) zimesimamia na kuongoza utafiti huu kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar, Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais –TAMISEMI, taasisi za ZIHHTLP na NPHL, UNICEF na THPS.
WAWEZESHAJI; Serikali ya Marekani chini ya Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI - PEPFAR kupitia Shirika la CDC.
KILICHOPIMWA; utafiti huu ulilenga kupima kiwango cha ukatili wa kingono, kimwili na kihisia na kuelewa hatari na athari za kiafya zinazohusiana na ukatili huu. Ukatili huu ni ukiukaji wa haki za binadamu na unaleta changamoto kubwa za afya na kubadilisha maisha ya watu wanaopitia ukatili. Ukatili huleta athari za muda mrefu za kiafya ikiwa ni pamoja na matatizo ya afya akili, mawazo ya kujiua, tabia hatarishi za ngono, uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya zinaa ikiwemo VVU, matumizi ya dawa za kulevya pia, hupunguza fursa za kimaendeleo na kuongeza umaskini.
FAIDA; kuboresha zaidi mikakati ya kutokomeza ukatili. Aidha, pamoja Serikali itaendelea kuongeza nguvu ya kuzuia na kupinga ukatili. Ikumbukwe, kupungua ukatili ni mafanikio ya ushirikiano wa Serikali na Wadau wote.
SHUKRANI Mhe. Dkt. @samia_suluhu_hassan Rais wa JMT🇹🇿 kwa uongozi mahiri na dhamira nzuri ya kutambua mchango wa Huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamii. @ikulu_mawasiliano @smaujata_tz @lemachutanzania
@Wananchi wote na wanahabari wote na kila mmoja kwa nafasi yake. Wadau wote wa maendelea sekta ya umma na binafsi ahsanteni sana🙌
Kiufupi, Wote Ahsanteni🙌🙌🙌🇹🇿