Utafiti unaonyesha kwamba kunywa vikombe kadhaa vya kahawa yako pendwa kila siku kunaweza punguza hatari ya saratani ya tezi dume

Symon Samba

New Member
Joined
Oct 17, 2024
Posts
3
Reaction score
0
Habari njema kwa wapenzi wa kahawa. Utafiti unaonyesha kwamba kunywa vikombe kadhaa vya kahawa yako pendwa kila siku kunaweza punguza hatari ya saratani ya tezi dume.

Utafiti wa hivi karibuni unaoangazia uhusiano kati ya unywaji wa kahawa na hatari ya saratani ya tezi dume ulijumuisha data kutoka kwa watu 1,081,568 walio na ogani ya tezi dume huko Amerika Kaskazini, Ulaya na Japani1.

Utafiti huo ulibaini kwamba kiwango cha juu kabisa cha unywaji kahawa kilihusishwa na kupungua kwa 9% ya hatari ya saratani ya tezi dume ikilinganishwa na unywaji kahawa wa kiwango cha chini kabisa.

Watafiti walitoa maelezo kadhaa yanayoweza kusababisha hali hiyo. Kahawa husaidia mwili wako kuchakata sukari (glukosi) vizuri zaidi. Pia inasaidia kupunguza inflamesheni (sehemu ya mwili kuvimba, kuwa nyekundu, yenye joto na maumivu) na kuongeza viini vinavyozuia au kupunguza uharibifu wa seli (antioxidants) na hupunguza viwango vya homoni kadhaa ambazo zinaweza kuhusishwa na saratani ya tezi dume.

Haya ni matokeo ya kusisimua, lakini ni muhimu pia kuzingatia mapungufu ya utafiti husika. Huu ulikuwa ni utafiti wa kuangalia/kufuatilia (observational study). Hiyo inamaanisha watafiti wasingeweza kudhibiti au kuchunguza kila jambo lililoweza kuwa limeathiri matokeo ya utafiti. Utafiti zaidi utatuwezesha kuelewa vizuri uhusiano kati ya matumizi ya kahawa na saratani ya tezi dume.

Kwa watu wasio na ogani ya tezi dume hawapaswi kuhisi wametengwa. Wote tunaweza kufurahia faida za kiafya zinazotolewa na kahawa. Kiasi kikubwa cha mapitio ya tafiti za mwaka 2017 kuhusu unywaji wa kahawa yalibaini kuwa vikombe 3 au 4 kwa siku vinaweza kuhusishwa na faida kadhaa za kiafya zikiwemo hatari ndogo zaidi ya kupata ugonjwa wa moyo na mishipa yake pamoja na saratanir2.

Lakini kabla ya kuanza kuandaa kikombe chako cha kahawa kijacho, kumbuka kwamba baadhi ya watu huathirika zaidi na kafeini kuliko wengine. Zingatia dalili za mwili wako unywapo kahawa na punguza kiwango ikiwa inakufanya ujihisi mgonjwa. Daima usitumie kafeini inapokaribia muda wa kulala.

Itunze afya yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…