Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Nimeona hii ni mashairi tu yanaendelea kumpendezesha huyu mama Kizimkazi hakuna lolote hapo.
Je Lissu angeshiriki ingekuwaje maana na amini kwa asilimia kubwa watu wangempigia kura hizo za maoni bwan Lissu, na je wangetangaza?
==================
Kituo cha Sera za Kimataifa-Afrika kwa kiingereza Centre for International Policy-Africa (CIP-Africa) mnamo Septemba 30 hadi 5 Oktoba 2025 kiliendesha kura ya maoni kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika 29 Oktoba 2025.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Oktoba 22, 2025 Mkurugenzi wa Tafiti na Uchapishaji wa CIP, Ndugu Thabit Tilangi amesema kuwa ikiwa uchaguzi mkuu utafanyika hivi sasa, asilimia 84.5 ya walioshiriki kura ya maoni wameonyesha kuwa watampigia kura mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Samia Suluhu Hassan huku Asilimia 8 walibainisha kuwa kura yao ni siri yao.
Ameongeza kuwa asilimia 3 watampigia mgombea wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), asilimia 3 watampigia mgombea wa Civic United Front (CUF). Asilimia 1.5, National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi)
Kura hiyo ya maoni ilifanyika katika mikoa 19 na 17 ya Tanzania Bara na 2 ya pemba na unguja iliyopatikana kwa utaratibu nasibu kwaajili ya kupata maoni na taswira ya hisia za wananchi kuhusu hali ya siasa na uchaguzi wao wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Mikoa iliyofanyiwa kura ya maoni ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Kaskazini Pemba, Kaskazini Unguja, Kigoma, Kilimanjaro, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Ruvuma, Tabora na Tanga ambapo watanzania watu wazima 1,976 walishiriki kutoa maoni ambapo walikiri kuwa ni wapiga kura halali walioandikishwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi.