Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 2,968
- 8,139
Kenya imechaguliwa kuwa sehemu ya utafiti wa vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume.
Nchi nyingine zinazoungana na Kenya ni
Uingereza, Italia na Chile ambapo wanaume watatakiwa kunywa kidonge kimoja kila mwezi.
Taasisi ya taifa ya maendeleo ya afya ya mtoto ilitengeneza kidonge kwa ajili ya kuwahimiza wanaume kutumia njia za uzazi wa mpango.
Inaelezwa kuwa mwanaume anayetumia kidonge anatarajiwa kupunguza idadi ya mbegu za kiume ndani ya saa 72 na kupunguza uwezekano wa kutungisha mimba.
Jaribio hili linatarajiwa kufanyika kwa miaka minne, wataalamu wakisema kuwa mpango huu unahitaji jitihada za pamoja za jinsia zote ili kufikisha lengo la asilimia 70.
Ingawa kumekuwa na msukumo kwa wakenya kukubali kidonge hicho, mpango huo umekosolewa swala la maadili na madhara yake baada ya dawa hizo kuwafikia vijana hali ambayo inadaiwa kuwa vitendo vya ngono vitaongezeka
miongoni mwao.