Ninadhani kupata kazi kwa waKenya katika nchi yetu, Marekani na kwingineko kunatoka aa juhudi zao binafsi na za kimfumo pia.
a) Mfumo wetu wa elimu ya juu ni wa kiingereza, na bado watu wengi waliohitimu elimu hiyo hawana ufahamu fasaha wa lugha hiyo.
b) Hakuna ushindani wa kweli "competencies" katika customer care na fani nyingine nyingi kama ilivo kwa wenzetu. Wakati wenzetu wanachagua ualimu, uhudumu ya hoteli, udereva nk kama trades wanazozipenda (au kwa urahisi wa kupata kazi au sababu nyingine) sisi fani hizo zinaonwa kama ni kimbilio baada ya mtu kufeli mitihani ya kidato cha nne au 6. Au kwa aliyemaliza darasa la saba ambaye lazima atakumbwa na tatizo la lugha ya kiingereza.
c) Tabia ya kuona kama anaykwenda nje kufanya kazi sio mzalendo (patriotic).
d) Kuwa na mfumo wa elimu usiokwenda na muda. Mitaala isiyohitaji maabara, ufundishaji wa kutumia "past papers" unaolenga kumwandaa mwanafunzi kujibu mtihani tu, sio kumjengea mazingira ya kukabiliana na current issues.
e) Kuwepo na mfumo wa kumwajiri mtu na kumfanya aamini atastaafu katika kazi hiyo. Sijui kama kuna "performance measurements" ukiachilia mbali "performance improvements". Kufanya kazi kwa mikataba ni jambo la maana ktk kujenga competencies na competitiveness ktk ajira. Mtu anakuwa kazini akiamini hatotoka. Leo hii kuna watu wamefanya kazi serikalini miaka 40!!! Unadhani hawa wana mwamko wa mabadiliko???
Takwimu za waKenya walioajiriwa itakuwa jambo gumu kulipata. Tuangalie kuja kwao kama udhaifu wetu kuliko ubora wao. Tukijifunza jambo moja au mawili kutoka kwao na KUYASHIKA, tutapunguza ujio wao. Ni vibaya kwa nchi ambayo lugha yake rasmi ya kufanyia kazi ni kiingereza lakini watu wake hawajui sehemu kubwa ya lugha hiyo.