Utafiti: Wanaopendelea ajira asilimia kubwa hufa maskini tofauti na wajasirimali

Utafiti: Wanaopendelea ajira asilimia kubwa hufa maskini tofauti na wajasirimali

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
download.jpg images (1).jpg images.jpg

Ujasirimali

images (4).jpg images (3).jpg images (2).jpg

Office work



[h=1]‘Vijana msiwaze kuajiriwa, jiajirini'[/h]Vijana wameshauriwa kuacha kutegemea ajira za ofisini, badala yake watafakari namna ya kujiingiza katika ujasiriamali ili kuondokana na umaskini.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Kitivo cha Elimu ya Biashara na Uchumi cha Chuo Kikuu cha Iringa (IUCo), Enock Ugulumo kwenye maadhimisho ya wiki ya ujasiriamali iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho mjini Iringa.

Maadhimisho hayo yalilenga kuwaongezea vijana na wanafunzi wa chuo hicho maarifa katika kujitegemea. Utafiti wa wataalamu mbalimbali duniani unaonyesha asilimia kubwa ya watu wanaotegemea ajira, hufa wakiwa maskini, tofauti na wale wanaojiajiri.

Alisema chuo hicho kimeanzisha mpango huo ili kuibua vipawa vya vijana na kuwawezesha wanafunzi kutumia elimu na ujuzi walionao kuibua ajira mpya, jambo ambalo litatoa fursa kwa jamii kupata nafuu ya upatikanaji wa kazi.

"Mfumo huu wa ujasiriamali ambao unaendana na mafunzo kwa vitendo, umelenga kuwafundisha wanafunzi namna ya kutengeneza bidhaa na kutoa huduma, kama sehemu ya kukabiliana na tatizo la ajira," alisema.

Mkurugenzi wa kitengo cha ujasiriamali wa chuo hicho, Dk Hosea Mpogole alisema mpango wa ujasiriamali kwa wanafunzi ulioanzishwa chuoni hapo utapunguza kero ya ajira nchini. "Vijana wakiwaza namna ya kujiajiri, Taifa litapaa kiuchumi," alisisitiza.
 
Sisi vijana tuna matatizo hatupendi kujiajiri wanataka wote wavae tai waingie ofisini kama hakuna uzalishaji tutaishije? vijana tubadilike.
 
Nyie bwana mnatuchosha wooote mnao preach vijana wajiajili, mmekomalia office za watu, hii kitu wangekua wana ongea wakina mengi, bakharesa ningeelewa, acheni vijana wachague jinsi wao wanavyotaka kuishi
 
Nyie bwana mnatuchosha wooote mnao preach vijana wajiajili, mmekomalia office za watu, hii kitu wangekua wana ongea wakina mengi, bakharesa ningeelewa, acheni vijana wachague jinsi wao wanavyotaka kuishi

Bora anayejua kwamba nafasi za ajira maofisini hakuna na hivyo kuwaelekeza njia za kujikwamua kiuchumi kuliko kuwaacha vijana waendelee kuchakaza kandambili kutembeza "RESUME"
 
Sasa yeye hapo IUCo anajitolea au ameajiriwa?Muongo mkubwa "mwangalie kwanza"(see him first). Mfanya kazi serikalini anaweza akakopa bati, hela nk. Huko ndo kwenye hela. Mjasiriamali atakopa wapi?Masharti kibaooo mabenki yanaringa ajabu.
 
Nyie bwana mnatuchosha wooote mnao preach vijana wajiajili, mmekomalia office za watu, hii kitu wangekua wana ongea wakina mengi, bakharesa ningeelewa, acheni vijana wachague jinsi wao wanavyotaka kuishi

Bangua kichwa yako big.
 
nitarudi....

Inategemeana na malengo ya mtu hata kama analpwa 30elfu mwez anaweza kutoka akiamua lakn kama hata anapata milion mwez kama hana malengo ni bure tu, vlevle mtambue kuwa haijaarish mtu anaingza sh. Ngap? Lakn je anatunza sh. Ngap? Mko apo ee.
 
Last edited by a moderator:
Kungekuwa na pesa watumishi wote wangekuwa matajiri

Katika orodha ya matajini ni kutoka umachingani, wajasirimali, kama ni waajiriwa hataondokana na kashfa ya urasimu na ubadhirifu kwa kuninufaisha binafsi kutokana na mali ya umma.
 
Kweli ulichosema matajiri wengi walikuwa wamachinga,watunishi wa umma wengi waganga njaa tu.
 
inategemeana na malengo ya mtu hata kama analpwa 30elfu mwez anaweza kutoka akiamua lakn kama hata anapata milion mwez kama hana malengo ni bure tu, vlevle mtambue kuwa haijaarish mtu anaingza sh. Ngap? Lakn je anatunza sh. Ngap? Mko apo ee

Tatizo la ajira ni kwamba unapangiwa kiwango cha pato na mwajiri anahakikisha pesa hazitoshi kumaliza matatizo yako na kile kiasi anachokulipa kinatosheleza kujikimu kwa muda mpaka utakapopata mshahara mwingine. Mjasirimali njia ikimfungukia atavuna kadiri ya uwezo wake.
 
  • Thanks
Reactions: Kbd
Binafsi ajira ilinilemaza sana mpaka nilipogutuka usingizini i decided to burn a ship. Unless fainali uzeeni!!
 
Kujiajiri ni vizuri ila siyo wote wanao tafuta kazi sasa hawana plan zakujiajiri kuna wanao tafuta kazi ili apate kamtaji wakuanzia naka exposure kidogo coz mazingira kwa sasa hayaruhusu yeye kuanza biashara.,
PS:wote wakiacha kazi wakijiajiri hii nchi itaendeshwaje?
 
Back
Top Bottom