Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
- Thread starter
- #21
Kujiajiri ni vizuri ila siyo wote wanao tafuta kazi sasa hawana plan zakujiajiri kuna wanao tafuta kazi ili apate kamtaji wakuanzia naka exposure kidogo coz mazingira kwa sasa hayaruhusu yeye kuanza biashara.,
PS:wote wakiacha kazi wakijiajiri hii nchi itaendeshwaje?
Jaribu kuwa na exposure pana zaidi. Fikiria jambo hili kwamba nafasi za ajira zaidi hupatikana kutona na nafasi zilizoachwa na wastaafu, vinginevyo kuwe na mpango wa kutengeneza nafasi nyingi zaidi za ajira. Hilo lilifanyika kipindi cha Nyerere siasa za ujamaa na kujitegemea. Leo vyuo ni vingi wahitimu ni maelefu wakati nafasi za ajira ni makumi hapo ndio tatizo.
Mtaji sio lazima uwe na kazi, ardhi tunashindwa kuitumia, nchi tajiri duniani raia wake wanaona Afrika tuna bahati ambayo hatuitumii, maana nchi za kipebari ardhi ya matajiri na ukitaka kupata ardhi unatakiwa uwe tajiri hapo ndipo kikwazo kikubwa cha mlalahoi. Kwetu ardhi ipo, hakuna gharama kuipata labda kama ni maeneo ya mijini, lakini vijijini raha tu ni bwerere.
Tunashida ya ujasiri wa kuthubutu na kujituma. Hakuna anayeshinda kulina tuta la viazi mviringo au vitamu ukavuna magunia kama matano hadi kumi. Ukiviuza hivyo bado hujafunguka kufungua kakiosk ka vitu vidogovidogo wanavyohitaji majirani?