Utafiti: Wanaopendelea ajira asilimia kubwa hufa maskini tofauti na wajasirimali

Jaribu kuwa na exposure pana zaidi. Fikiria jambo hili kwamba nafasi za ajira zaidi hupatikana kutona na nafasi zilizoachwa na wastaafu, vinginevyo kuwe na mpango wa kutengeneza nafasi nyingi zaidi za ajira. Hilo lilifanyika kipindi cha Nyerere siasa za ujamaa na kujitegemea. Leo vyuo ni vingi wahitimu ni maelefu wakati nafasi za ajira ni makumi hapo ndio tatizo.

Mtaji sio lazima uwe na kazi, ardhi tunashindwa kuitumia, nchi tajiri duniani raia wake wanaona Afrika tuna bahati ambayo hatuitumii, maana nchi za kipebari ardhi ya matajiri na ukitaka kupata ardhi unatakiwa uwe tajiri hapo ndipo kikwazo kikubwa cha mlalahoi. Kwetu ardhi ipo, hakuna gharama kuipata labda kama ni maeneo ya mijini, lakini vijijini raha tu ni bwerere.

Tunashida ya ujasiri wa kuthubutu na kujituma. Hakuna anayeshinda kulina tuta la viazi mviringo au vitamu ukavuna magunia kama matano hadi kumi. Ukiviuza hivyo bado hujafunguka kufungua kakiosk ka vitu vidogovidogo wanavyohitaji majirani?
 
Unalosema ni nzuri ndugu but ishu nikuanzia hayo uliyosema yakuchukua ardhi kulima kidogo napo panahitaji kamtaji sasa kwa graduate atatoa wapi? Taasisi za fedha nazo ni masharti magumu kupata mkopo ukiangalia kijana katoka familia ya mwananchi wakawaida hana popote pakupata fedha zakuanzisha biashara so choice inabaki kuzunguka na bahasha Mungu akinyoosha mkono wake upate kazi ndo ujue ustarabu mwingine.
 
Mimi nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa na bustani na sikuhitaji mtaji na hiyo bustani nilipanda mbogamboga na miwa, hali kadhalika migomba, ilinipatia matumizi ya kawaida bila kuwasumbua wazee, wao ni ada tu na sare za shule.

Nilipokuwa sekondari kipindi cha likizo mwisho wa mwaka nilikuwa na shamba ekari moja ambalo nililima na kupanda mahindi na kuwaachia wazee wanitunzie, na niliporudi likizo ya Juni ilikuwa ni kuvuna kwa mazingira niliyokuwa nayo magunia sita nilipata ilikuwa pesa ya kutosha kwenda nayo kunisaidia matumizi madogomadogo shuleni.

Mtaji gani unataka wakati mtaji ni jembe na ardhi? Usianze na mambo makubwa anza na shamba dogo kupata uzoefu kwa kutumia nguvu zako mwenyewe na kila siku pato lako litakufanya upanue wigo na kuongeza vifaa unavyovihitaji.
 
Hiyo ardhi unaipata wapi kwa mfano.
 
Hiyo ardhi unaipata wapi kwa mfano.

Unauliza swali ambalo linaonyesha kwamba wewe hupo Afrika na kabisa Tanzania. Kuna mambo ya muhimu kuulizana lakini si kuuliza swali ambalo jibu unalo.
 
Ningekua na jibu ningeuliza best, corz vijana hawana startin point yakuanza kujiajiri kirahisi hivo unavozani, siyo wote wametoka kwenye conducive environment yakustart a business kama ulivopitia.
 
Ningekua na jibu ningeuliza best, corz vijana hawana startin point yakuanza kujiajiri kirahisi hivo unavozani, siyo wote wametoka kwenye conducive environment yakustart a business kama ulivopitia.

Kama hujawahi kuwa na idea ya kujitegemea mtu akikwambia panga getto, kila kitu utakiona hakiwezekani...utawaza kula, kodi, vyombo nk
 
Kama hujawahi kuwa na idea ya kujitegemea mtu akikwambia panga getto, kila kitu utakiona hakiwezekani...utawaza kula, kodi, vyombo nk

Of corz nitawaza kama sina any source of income, lakini kama kipato kipo kwanini nisijitegemee mkuu.
 
Hiyo ardhi unaipata wapi kwa mfano.

Unauliza swali ambalo linaonyesha kwamba wewe hupo Afrika na kabisa Tanzania. Kuna mambo ya muhimu kuulizana lakini si kuuliza swali ambalo jibu unalo.

Ningekua na jibu ningeuliza best, corz vijana hawana startin point yakuanza kujiajiri kirahisi hivo unavozani, siyo wote wametoka kwenye conducive environment yakustart a business kama ulivopitia.

ardhi ndo mtaji na msingi wa maendeleo, lakini waafrika(watanzania) tulio wengi tunategemea zaidi kupewa maelekezo. tunasahau kuwa "kufikiri" ndo kila kitu. tunasahau kuutumia ubongo ambao ni mtaji tuliozaliwa nao ndo maana tunaulizana, " ardhi nitaipata wapi?" ardhi zipo kijini za kulima, unafanya kitu kidogo tu cha kuomba hiyo ardhi kwa mmiliki au serikali ya kijiji. ubongo( brains) ndo msaada katika plan zote.
 
Thanks mr. Econ ume eleweka.
 
Tafiti zingine bana...

Hivi research question hapa ilikuwa ni nini? Ama hypothesis iliyojaribiwa ni ipi? Ama utafiti huu ulilenga kuthibitisha kuwa Program ya Ujasiriamali ya hapo chuoni ndio most desirable Program hapa nchini?

Ama labda viongozi wa chuo wamenukuliwa vibaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…