Utafiti:Wanawake msichelewe kuzaa

Utafiti:Wanawake msichelewe kuzaa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
110413114523_pregnant_woman_generic_304x171_bbc_nocredit.jpg

Kuchelewa kuzaa kuna matatizo yake. Je unayafahamu?


Wanawake wanaochelewa kuzaa wanakabiliwa na tisho la kupata matatizo ya afya ya uzazi. Huu sio utafititi tu balo maoni ya daktari mmoja mkuu mjini Nairobi Kenya.

Athari za kuchelewa huko ni pamoja na kukumbwa na utasa, tisho la kupata Saratani ya kizazi na matiti pamoja na matatizo wakati wa kujifungua.

Wanawake wengi wanaofanya kazi huchelewa kuzaa mtoto wao wa kwanza hadi wanapofika umri a miaka 35 badala ya kuzaa wakiwa na umri wa miaka 24-28.
Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya afya ya uzazi.

Mtaalamu wa afya ya uzazi mjini Nairobi, Daktari John Ong'ech aliyehojiwa kuhusu hoja hii alinukuliwa akisema kuwa ''wanawake kwanza wanataka kusoma masomo ambayo hayaishi, daima wako madarasani na ofisini na kuahirisha kuzaa mtoto wao wa kwanza hii ni hatari kubwa.''

Bwana Ong'ech alisema kuwa wanaochelewesha kuzaa, wanaweza kupata Fibriods au uvimbe katika kizazi, na hata kupata magonjwa kama Saratani ya kizazi au HIV.

Fibroids zinasababishwa na kuzagaa kwa homoni mwilini, kutokana na kutumia mbinu moja ya kupanga uzazi kwa mda mrefu.

Wanaochelewa kuzaa pia wanakabiliwa na tisho la kuzaa kwa njia ya upasuaji au Caesarean .
Hatari hizi ni nyingi tu, sasa chaguo ni kwako.

Mbali na kazi kwa nini wanawake wengi wanachelewa kuzaa? Tupe maoni yako kwenye ukurasa wetu wa Facebook, Bofyahttps://www.facebook.com/pages/BBC-Swahili/160894643929209?ref=ts&fref=ts
 
Moja ya factor inayo affect Family plaanning sio education structure?
 
Sasa hii imekaaje kijamii au kisayansi maana ukiwa na miaka 24 ndio ukazaa unaambiwa umewah kuzaa.

Eti had ufikishe miaka 28 mbona kuchanganyana DR
 
Sasa hii imekaaje kijamii au kisayansi maana ukiwa na miaka 24 ndio ukazaa unaambiwa umewah kuzaa.

Eti had ufikishe miaka 28 mbona kuchanganyana DR

Kwahiyo unasubiri hadi ufike miaka 28? Mimi nipo tayari kabisaaa kukupa huyo mtoto usije kupata madhara huko mbeleni.!!
 
Kwahiyo unasubiri hadi ufike miaka 28? Mimi nipo tayari kabisaaa kukupa huyo mtoto usije kupata madhara huko mbeleni.!!

Wangu nimesema hvyo coz nimepata mtoto nikiwa na miaka 24 bt wazazi hawakupenda na kusema bado mtoto
 
Wasikudanganye mie nimepata nikiwa na 23 miaka chuo mwaka wa kwanza na mtoto wangu anakimbia vizuri!
 
Back
Top Bottom