Utafiti wangu Kuhusu APP za Mikopo

Utafiti wangu Kuhusu APP za Mikopo

uttoh2002

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
17,060
Reaction score
32,400
Ninawasalimu wote katika Jumapili hii Njema, na tulivu. Naomba nisipoteze mda na niende kwenye mada moja kwa moja.

Baada ya kuwa napata matangazo ya App za mikopo, nikaamua nifanye ka utafiti kadogo kuona zinavyofanya kazi.

Kwa kipindi cha Miezi 2 nili download up 10, na nikakopa na kurudisha, na haya ndo niliyoyaona:

#1. Uongo na utapeli wa ajabu:

Hawa watu ni matapeli, na hii ni scam kabisa, Hakuna jambo lolote wanalosema ni la kweli.

#2. Unapoteza Privacy yako:

Unapo dowload app yao na kukubali masharti, wanakuwa na uwezo wa ku upload contact list yote.

#3. Mikopo yao haina Msaada:

Hii mikopo haina msaada, itakufanya desperate zaidi, na tegemezi kwao milele.

#4. Mda wa Mkopo:

Imagine 30% interest kwa mkopo wa siku 8, ukishaulipa kwa watu wenye shida watakopa tena, ni cycle ya kimasikini.

#5. Hawana kauli kabisa.

Kuanzia siku 2 kabla ya siku ya kurejesha nimetumia messages 58, Whatsapp, na namba tofauti.

Swali kwa Serikali/Wito:

Hivi hawa watu wanapopewa leseni, serikali haina namna ya kuingilia Policy za uendeshaji wao kuwalinda wananchi wao?

Haiwezekan mtu awe na ruhusu ya kufanya haya yanayofanyika jamani kwa wa Tanzania Maskini na kuwapeleka kwenye utumwa.

Nitarejea kuelezea kila buletin hapo juu, na kama ni sahihi nitataja app zote nilizozifanyia utaratibu na kuanika conduct zao hapa.
 
Serikali kupitia BOT haiwezi kuruhusu taasisi itoze lipa asilimia 30, uongo

Nimefanya utafiti wangu na wanatoza, tena kwa siku chache pungufu ya mwezi, sasa sijui argument yako ni nini? Nina fact!

Na kama wanafanya kwa uhuni wao, je serijali kwa nini haiingilii kati kuwasaidia hawa watu maskini wanaofanywa victims?
 
Mimi mtu akishaanza kulalamika kwamba vigezo vya mkopo wa taasisi X au mtu X vinambana huwa nashindwaga kuelewa kabisa yaani,kwani kabla ya kuomba mkopo na kuja kulalamika hukusoma vigezo na masharti?! Kama uliona masharti ni magumu kwanini uliomba?
 
Sasa nisikilize, sijalalamika mimi, na nilichukua makusudi kwa ajili ya kujifunza.

Nachosema, ni kweli kuna watu desperate ambo wanautaji huo msaada, na labda hawana namna.

Issue yangu, ni je, serikali haina Policy na conduct ya namna ambayo ina control haya makampuni yasiumize watu?
 
Nimefanya utafiti wangu na wanatoza, tena kwa siku chache pungufu ya mwezi, sasa sijui argument yako ni nini? Nina fact!

Na kama wanafanya kwa uhuni wao, je serijali kwa nini haiingilii kati kuwasaidia hawa watu maskini wanaofanywa victims?
Sijakaa kuwa hawafanyi, concern yangu ni kuwa serikali kupitia mamlaka zake haiwezi bariki asilimia 30
 
uongo mwingine wa mwenz huu...Hakuna app inayotoa mikopo mitandaoni,, wanataka mdamload hzo app wapige vihela vyenu vya mb..siku nyengine acha kulialia mamb usiyoyajua...

usiwe kama mke wa mjumbe.😂😂
 
uongo mwingine wa mwenz huu...Hakuna app inayotoa mikopo mitandaoni,, wanataka mdamload hzo app wapige vihela vyenu vya mb..siku nyengine acha kulialia mamb usiyoyajua...

usiwe kama mke wa mjumbe.[emoji23][emoji23]
We ni tajiri local saaana!! App ni nyingi na wakopesha, humu kuna uzi unatambaa hatari ukielezea visa vya hizo app baada ya watu kukopa na kulalambele
 
uongo mwingine wa mwenz huu...Hakuna app inayotoa mikopo mitandaoni,, wanataka mdamload hzo app wapige vihela vyenu vya mb..siku nyengine acha kulialia mamb usiyoyajua...

usiwe kama mke wa mjumbe.😂😂
Kama hujui jambo kaa kimya App ziko nyingi sana.
 
Hawa majamaa matapeli kabisaa, wanatumia fear na intimidation kupata pesa, riba za kitapeli, mfumo umekaa kuteka na kuongezea mtu matatizo sio kupunguza. Waangaliwe, na ukifatilia ni kampuni kama 2-3 ila wanamiliki apps nyingi nyingi
 
Hapo kuna kampuni 3 mmiliki ni mmoja...jina walilosajiliwa na kupata leseni ya bank kuu ni tofauti na majina ya app zao..
Yes actually kampuni hiyo ina apps nyingi ziko chini yao. Wamesajili jina tofauti, hizo apps ndo kama vifurushi vyao tofauti vya huduma. Na ni wachina, information tu ya wanapatikana wapi hawasemi. washachafua kwao, asia yote, wanakamua waafrica sasa, walianza wanigeria washalia sana wakazifungia nyingi.
 
Back
Top Bottom