Utafiti wetu na ugunduzi uendane na wakati....

Utafiti wetu na ugunduzi uendane na wakati....

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Nimekuwa nikisikia mwanafunzi wa Chuo kikuu anafanya utafiti au umefanya ugunduzi wa gari, au pengine ndege au hata helcopter bila kusema ni nini cha ziada kilichopo au kitakachokuwepo na kunipa wasiwasi kama vijana wetu wanajua tofauti ya kugundua na kujifunza. Kwa ufahamu wangu, kutengeneza gari , Helcopter, majiko ya gesi/Sola, baiskeli, pikipiki ya kawaida ni sehemu tu ya mafunzo na sio kugundua

Hii ni kwa sababu magari yapo tayari na yanafanya vizuri, ndege zipo tayari nk
Ila mtu akija na aidia mpya mfano agundue lori la tani 10 litumie lita 1 kwa umbali wa klm 15/20 huo utakuwa ni ugunduzi au pengine Engine ya paso iweze kuvuta tani 5 pia huo ni ugunduzi nk lakini sio kutengeneza kitu chenye ufanisi duni kuliko vilivyopo sokoni, atangaze kuwa amegundua; wanachofanya ni sawa na mtoto ajifunze 2+3 = 6 akuambie amegundua kuwa 2+3=6 na wewe uanze kutangaza kwenye Radio na TV kuwa mtoto amegundua

"Hapa nimeongelea kwa wasomi wa ngazi ya juu ya Elimu; hawa vijana wetu wa bunifu huku mtaani tuwaache waendelee kwa kadri ya uwezo wao"
 
Back
Top Bottom