Utafutaji wa Dhahabu

Newword

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2019
Posts
326
Reaction score
299
Habari wataalamu.

Nina miaka kama 10 nimekuwa nazunguka migodini kuchimba madini ya dhahabu bila mafanikio.

Nimepoteza kiasi cha sh.M.6.5 katika Maeneo ya Musoma Bhuhemba, Nyarugusu Stamico, Nyaruyeye Geita, Bingwa Lwamgasa na Kaseme.

Kuna kipindi nikiwa Mgodi wa Buziba Lwamgasa nilichimbisha duara likafika na nikabahatisha kuwa na mauzo ya Gramu 8 kwa mfuko.

Nilibahatisha kupata mifuko 20 cha ajabu baada ya siku mbili mwamba ukageuka na zikawa shaba badala ya dhahabu na kusababisha mfuko kuwa na point 3 tu lakini jirani yangu mfuko ukapanda na kuwa gram 28 kwa mfuko.

Mpaka muda huu nimechoka kabisa.Najiuliza nakosea wap katika utafutaji wa madini haya?

Kwa wataalamu naomba ushauri sijakata tamaa bado.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulikuwa unachimbisha vikole au dhahabu ya mwamba?
 
Kaseme?!!! Nyamtondo, nyamalulu, nyamahuna, Nyamalimbe, nyantwiga?

Uchimbaji wa sasa sio wa moko na ponchi au mbulu na bobu ni uwekezaji wa pesa nyingi. Mwenye nacho ataongezewa. Lasivyo upate mtu wa kukushika mkono.

Ila usikate tamaa badili mfumo wa kazi ili ufanye kazi za tija na sio za kubahatisha sana.
 
Newword,
Uchimbaji wenu ni wa ujima! Madini Kama yapo sehemu yapo,mganga au ushirikina Ni kupoteza muda na kumkasirisha Mungu..tumieni teknologia mtapata dhaabu achaneni n uchimbaji wa kubahatisha Kama bahati na sibu
 
6m unalalamika namna hii??...usikate tamaa!...mbona mishe za migodini mie naziona ni nyingi?watafte wataalam wakusaidie tatizo majority wanafanya kienyeji sana sana!
Ukishindwa kbs njoo tujoin tujenge plant!...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…