Utafutaji wa Dhahabu

Utafutaji wa Dhahabu

Habari wataalamu.

Nina miaka kama 10 nimekuwa nazunguka migodini kuchimba madini ya dhahabu bila mafanikio.

Nimepoteza kiasi cha sh.M.6.5 katika Maeneo ya Musoma Bhuhemba, Nyarugusu Stamico, Nyaruyeye Geita, Bingwa Lwamgasa na Kaseme.

Kuna kipindi nikiwa Mgodi wa Buziba Lwamgasa nilichimbisha duara likafika na nikabahatisha kuwa na mauzo ya Gramu 8 kwa mfuko.

Nilibahatisha kupata mifuko 20 cha ajabu baada ya siku mbili mwamba ukageuka na zikawa shaba badala ya dhahabu na kusababisha mfuko kuwa na point 3 tu lakini jirani yangu mfuko ukapanda na kuwa gram 28 kwa mfuko.

Mpaka muda huu nimechoka kabisa.Najiuliza nakosea wap katika utafutaji wa madini haya?

Kwa wataalamu naomba ushauri sijakata tamaa bado.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mi ni mchimbaji pia. Nimeendesha shughuli zangu za uchimbaji nyamigogo...nyaruyeye enzi za baraka..nikaja nyarugusu...mugusu pamoja na nyamatagata. Niko na uzoefu mkubwa katika hayo mambo. Kiukweli kuna changamoto kubwa sana ila kuna pesa nyingi sana mambo yakikaa sawa.

Kwa uzoefu wangu mpaka sasa kuna njia ambayo sasa nimeamua kuifuata na ni njia sahihi katika utafutaji wa dhahabu.

Nakuomba kama upo kweli sirious unataka hela ya dhahabu hebu nicheki PM tushauliane kisayansi.
 
Kama mna pesa, kwa nini msitafute processing licence, mkawa mnagawana na wachimbaji wadogo percent ya kile wanacho pata?
Miaka 10 mngekuwa mshapata uzoefu wa kutosha. Labda pengine hata faida kubwa luliko mnavyowekeza kwenye "Prospect" zisizokuwa na uhakika.
Na kwa sababu ya kutokuwa na data za kutosha, ni rahisi kuambiwa hiki mara kile mwisho wa siku unatumbukia kwenye ushirikina.

Madini tunayakosea sisi watanzania....niwakati sasa wa kuachàna na njia za asili za utafuataji wa dhahabu na ķutumia sayànsi.

Wachimbaji wengi wa dhahabu wanaenda polini kwa kubuni bila kuwa na uhakika kama wanapòfànyia kazi kuna dhahabu au laa.
 
Huwa nasema siku zote madini hasa dhahabu inaendana na nature yake,huwezi kuforce nature,nature ndyo itakupandisha na hyo hyo inaweza kukushusha,uchimbaji wa sasa bora uwe na mtaji wa kutosha,kusanya data za kijiolojia kutoka kwa wataalam,fanya vipimo maabara mara kwa mara usichoke....hamna cha shetani wala maimuna,mimi binafsi nmeshawahi kuexplore virgin area na tukapata dhahabu na hadi sasa sina biashara nyingine zaidi ya dhahabu....usiamini ushirikina amini MUNGU tu
 
Watu wanapoteza million Mia tano mgodini bila kuzalisha chochote we unakuja kulalamika mbele ya wanaume Kuwa umepoteza 6.5m? Hizo hela watu wanapoteza hata kwa kulima matikikiti Maji tuu mkuu,,, never give up [emoji115]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom