Utajibuje ukiulizwa utaifanyia nini Tanzania?

Utajibuje ukiulizwa utaifanyia nini Tanzania?

Nimependa hapo kwenye kuimarisha MOJO.
Hivi hii MOJO ni nini mkuu na ina umuhimu gani na inapatikana wapi hapa Tanzania?
Nini hasa faida za MOJO?

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
MOJO mkuu !au Vavumaaaa!,ni morality ya watumishi kuongezeka, maana wakija ofisini wanakua wapo fresh na sharp kutekeleza majukumu yao,kwa hiyo kazi ni kuanzia monday to Thursday, Friday to Sunday wapo off na wanapata muda wa kuwa pamoja na familia zao
 
Siwezi pewa hiyo nafasi kuongoza hii nchi maana ina wenyewe wenye mifumo yao wanayoikubali wao wenyewe na kumtaka yupi wamtakaye.

Lakn Mungu si yusuph wala si asuman hakuna lishindikanalo, kama nikipata chance ya kuongoza hii nchi ya kusadikika walahii kuna watu mtakimbia nchi kama sio kuomba ardhi ipasuke mkafute pakuficha sura zenu.

[emoji419].First of all nitafumua katiba na kuwaweka kizuizini wanasiasa wote kuanzia CCM na Upinzani wote watakuwa chini ya ulinzi na mchakato wa uchunguzi mkali wa mali za Umma utaendelea nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, ukoo kwa ukoo.

[emoji419].wanajera baadhi kama sio wote watatoka kuruhusu Space kubwa ya kuwaruhusu wafungwa wapya maana jera zitajaa kila siku kutakuwa na intake ya maelfu ya wafungwa(wanasiasa)

[emoji419].Fungia baadhi ya media uchwara zinazopenda kupost habari za uzushi na uongo, Mambe akiwepo na zile youtube channel za hovyo hovyo.

[emoji419]. Kuwarudisha waTz wote waliokimbia nchi warudi ili tupambane pamoja na kama itagundulika walikimbia wakiwa na makosa basi watawekwa kizuizini kwa upelelezi mkali.

[emoji419].Fumua Bunge lote na kuondoa baadhi ya uongoz wakipuuzi mfano uo uteuzi wa wabunge wasiochaguliwa na raia yaan wabunge viti maalumu.

[emoji419].Nitajipa Kinga ya kutoshitakiwa mimi tu maana najuwa kwa haya niyafanyayo wapo wahuni watataka kunishitaki huko walikozoea kwenda kushitaki.

[emoji419].Elimu ya shule na chuo kikuu kufumuliwa upya[emoji23].

[emoji419].Nitauaa vyama vyote vya siasa na kuforce kuzaliwa kwa chama kipya cha wananchi kisichohitaji ruzuku ya serikali[emoji23].

[emoji419].kuyawekea vikwazo makanisa uchwara na misikiti inayoibuka kama uyoga ambayo haifuati taratibu na zinapotosha mila za kiafrika.

[emoji419]kila raia atalazimika kuingia ktk database ya taifa na kutambulika kwa Special ID(micro chip) inshort kila mtu atakuwa na alama ya taifa itakayomruhusu kupata huduma mbalimbali za kijamii, na bila hiyo alama(utambulisho) utatambulika kama mhamiaji haramu na tutakushughurikia kama si kukutimua nchini,
Note[emoji117] hii ni nzuri kwa kupambana na uharifu.

[emoji419].nitajiongezea miaka ya kuitawala nchi mpaka pale nitakapoona nchi imenyooka na wahuni wote wamepotelea jela kama sio kufa kabisa na vizaz vyao vyote kufutwa ktk ramani ya nchi hii[emoji23].

[emoji419]Kiufupi chini ya uongoz wangu kuna raia watakula bata na kuna watu watakaoona kama jehanamu ya moto imehamia dunian na watatafuta pakukimbilia hawatopapata maana nitawasaka usiku na mchana na kuhakikisha wanalipia machungu ya waTanzania.

[emoji419]kila mwanafunzi atalazimishwa kutembelea vivutio vya utalii nchini ili kukuza utalii wa ndani na kuwafanya waTz watambue resources za nchi yao kilazima maana nishachoka kulazimishana.

[emoji117]kwa ufupi tu utawala wangu watu watauita udicteta na ushetan uliotabiliwa na vitabu vya dini kuwa atakuja Masih dajal , na kweli wengi wa wale wahuni watateseka sana na vizazi vyao vyote,

[emoji419] kwa haya mabadiriko madogo tu yanatosha kubainisha kuwa sistahili kuwa kiongozi wa nchi hii maana nitakiuka sheria na taratibu dharimu walizojitungia wanasiasa kufaidi nchi

Dunia haiwahitaji watu wa aina yangu maana huleta mabadiriko makubwa dunian ndiomaana hata wanapopata chance hutengwa na dunia kama sio kuuliwa ama kupewa sifa mbaya[emoji23][emoji23], watu wa aina hii kwa sasa tupo wachache lkn huwa tunatambulika kwa series ya bloodline tangu mwanzo mfano hitra, Osama, gadafi, iddi amini, kim joh hung, putin, magu, makonda[emoji23], na the last nipo hapa nawakilisha bendera ya wanadicteta
View attachment 2280168
Ndani ya siku tatu unaweza kufanya haya yote!?
 
Asante kwa swali zuri Mimi Kama Mjamaa wa Kisasa ningepata nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mambo ambayo ningeifanyia nchi yangu pendwa ya Tanzania ni haya yafuatayo:-

[emoji404] MAGEUZI MAKUBWA YA MFUMO WA KISIASA/KIUTAWALA NCHINI

* Kuanzisha mchakato wa Katiba mpya upya utakao wahusisha wasomi nguli katika taifa pamoja na maoni mbalimbali ya wananchi ili iletwe katiba bora kwa wananchi kwa manufaa ya nchi.

* Nitapendekeza bunge litunge sheria kali [ kunyongwa mpaka kufa ] dhidi ya wala rushwa , wabadhilifu wa fedha za umma , wauza madawa ya kulevya , wacheleweshaji na wakwamisha miradi mbalimbali ya nchi n.k

* Mabadiliko makubwa juu ya mfumo wa elimu utakao zalisha wasomi ambao watakuwa viongozi bora katika nchi kwa ngazi mbalimbali na taasisi mbalimbali za kiserikali na kibinafsi ndani ya nchi mfano ujenzi na uanzishwaji wa vyuo/chuo cha uongozi.

* Mapendekezo ya uanzishwaji wa taasisi imara itakayo isimamia na kuilekeza serikali namna inchi inavyotakiwa kuendeshwa. kwa kila kiongozi mkuu wa nchi[ Rais ] atakaye ingia madarakani kwa mujibu wa sheria itakuwa ni lazima afuate utaratibu uliowekwa na hiyo taasisi namna na utekelezaji wa sera za nchi inavyotakiwa kuwa, Rais hapaswi kuwa juu ya hiyo taasisi.

* Kupunguza baadhi ya vyeo katika serikali Kama kuondoa cheo cha umakamu wa Rais, vyeo vya unaibu waziri kwa wizara zote, kufuta nafasi za wabunge wakuuliwa na Rais , kufuta ubunge wa viti maalumu n.k

* Kuipa Uhuru mihimili yote mitatu isiingiliane [ mahakama, bunge na serikali ].

* Pendekezo la ufutwaji wa vyama vyote vya siasa na kuamuru uundwaji wa vyama vipya bora vya kisiasa visivyozidi viwili na kutengeneza mfumo unaohusu vyama viwili vya siasa pamoja na mgombea binafsi.

* Uundwaji wa sheria utakaoamuru mikataba yote ya kiserikali inayosainiwa lazima ipitie bungeni ifanyiwe upembuzi yakinifu pia iwekwe wazi wa wananchi wote ndipo isainiwe.

* Kupunguza idadi ya mikoa kwa kuunda mfumo unaoshabihiana na serikali za majimbo lakini zitakuwa ni serikali za mikoa mbalimbali iliyounganishwa pamoja na kuzalisha mkoa mmoja utakaojitegemea na kujiendesha lakini ukisimamiwa na serikali kuu.

* Kuwajibishwa kwa wote waliyoihujumu serikali kwa zile serikali zilizopita [ Vifungo vya maisha kutokana na makosa waliyo fanya pia kwa wengine kunyongwa mpaka kufa kwa makosa walivyofanya ].

* Kuruhusu tume huru ya uchaguzi na kuruhusu uchaguzi wa Uhuru na haki katika nchi.

* Kuondoa chembechembe za utawala wa kidikteta nchini kwa kuruhusu Uhuru wa watu kimaoni kwa kushauri pia na kuikosoa serikali , pamoja na kuruhusu Uhuru wa kisiasa nchini pasipo watu pasipo kuletewa kadhia yoyote kutoka kwa jeshi la polisi.

* Kuanzisha mipango ya kimaendeleo ya muda mrefu kwa manufa ya nchi , mipango ya kimaendeleo ya miaka 5, 10, 50 na 100 hii itasaidia kuwa na serikali imara itakayo juwa imefanya nini na kipi kinafuatia kufanyiwa.

* Kupunguza madaraka makubwa ya cheo cha urais na kuondoa kinga ya kutokushitakiwa afanyapo kosa.

* Kuunda serikali na kuweka mfumo utakao ilazimu serikali iheshimu Sheria na katiba ya nchi.

* Kuunda mfumo utakoitenga serikali pamoja na dini zisiingiliane .pawepo na mpaka Kati ya serikali na dini.

* Nitajitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kupambana na chembe chembe zozote zitakazo leta ubaguzi wa kidini , kikabila , na kiitikadi za kivyama ndani na nje ya serikali.

* Nitaakisha upunguzwaji wa mishahara ya wabunge kwa mshahara wa mwezi usiozidi million mbili na mishahara ya mawaziri isizidi zaidi ya millioni tatu

* Nitapendekeza na kulishauri bunge kubadili Sheria na kumuru muongoza bunge spika wa bunge asiwe miongoni mwa wabunge pia mawaziri wasiwe wabunge na kigezo Cha mtu kuwa mbunge lazima awe na elimu ya kiwango cha degree.

[emoji404] MAGEUZI MAKUBWA YA KIUCHUMI NCHINI

* Nitahakikisha nafanikisha uundwahi wa special economic zones [ SEZ ] kwa kuanza na maeneo yapatikanayo / yanayopakana na nchi za jirani hili litafanyika kwa maeneo yote yale yanayopakana na nchi kuanzia kaskazini mwa nchi kuja magharibi mwa nchi, mashariki mwa nchi , pamoja na Kusini mwa nchi.

* Baada ya kuanzishwa kwa special economic zones [ SEZ ] kwa maeneo yanayo pakana na nchi nitaanzisha special economic zones [ SEZ ] kwa maeneo yaliyo ndani ya nchi ili kufanikisha uinuaji wa kiuchumi kwa maeneo yaliyomo ndani ya nchi pia.

* Mabadiliko makubwa ya mfumo wa elimu utakao chochea maendeleo ya nchi . nitahakikisha sekta ya elimu inafanyiwa mabadiliko makubwa yatakayo endana na sayansi na teknolojia ili elimu iweze kuzalisha wasomi watakao isaidia nchi kukua kiuchumi zaidi na Kisayansi na kiteknolojia.
i, kuomba ushirikiano wa kielimu na Kisayansi na kiteknolojia baina ya Tanzania na mataifa yaliyo fanikiwa na kwenye hizi sekta mfano U.S.A , China , Korea ya kusini , Japan , England n.k
ii, kupelekea wanafunzi wa kitanzania kusoma kwenye nchi tulizoomba ushirikiano ili wanafunzi wakihitimu warudi nyumbani kugawa maarifa kwa wazawa.

* Usafirishaji[ Anga , maji na ardhi] nitahakikisha na shirikiana na serikali niliyoiunda pamoja na wachumi wa nchi ni kwa namna gani tutaweza kuteka sekta ya usafirishaji katika bara la Africa kwa kuhakikisha nchi nyingi barani Afrika zitatutegemea kwa asilimia kubwa sisi kuhusu swala la usafishaji katika anga , ardhi na maji kwa usafirishaji wa bidhaa zao walizo agiza nje ya bara la Africa kwa kuhakikisha tunaua bandari za majirani zetu kwa sisi kuwa na bandari zitakazo kuwa tegemeo na nchi nyingi barani Afrika bandari zitakazo na ukubwa na ubora wa hali ya juu , pia tutahakisha pia tunateka sekta ya anga kwa kuhamasisha zaidi utalii utakao chochea njia ya anga , pia nita hakikisha serikali inajitolea kuboresha usafiri wa ardhi kwa miundombinu iliyo bora ya bara bara na reli zitakazo rahisisha usafirishwaji wa mizigo kwenda nchi jirani pamoja na kurahisisha usafiri nchini utakao chochea zaidi maendeleo nchini.

* Nitahakikisha na boresha wizara ya Mambo ya nje ya nchi lazima iwe na wataalamu wa maswala ya uchumi wa kutosha pamoja na waziri wa wake lazima awe na uwezo wa kurahisha mambo mbalimbali baina ya nchi na mataifa mengine awe anauwezo wa kutengeneza ushawishi wa kiuchumi wa mataifa ya nje pamoja awe na uwezo wa kuisaidia serikali kuingia ushirikiano wa kiuchumi na mataifa mbalimbali utakoweza kuisaidia zaidi nchi yetu.

* Nitahakisha na boresha wizara inayohusiana na mikataba ya nchi ni lazima iwe na wasomi wa maswala mbalimbali ya kimikataba na kiuchumi ili kuweza kuiokoa serikali isiingie mikataba mibovu isiyo na manufaa bali kuisaidia serikali kuingia mikataba yenye manufaa kwa nchi.

* Uboreshaji wa wizara ya kilimo . nitahakisha nakaa na wataalamu wa maswala ya kilimo waliomo ndani ya nchi na kupelekea wanafunzi wengi kwenye nchi zilizoendelea kwenye maswala ya kilimo ili waje kusaidia kwenye uundwaji wa sera itayofanikisha sekta ya kilimo inaijuliwa na kuwa tegemeo kwa asilimia kubwa kiuchumi katika Taifa letu .
i, kuanzisha benki bora na yenye nguvu ya kilimo
ii, serikali kutoa mikopo nafuu kwa watu wenye mawazo bora kuhusu kilimo
iii, kupelekea wasomi nye ya nchi wakasomi elimu bora na kuja nchi kutoa hiyo elimu bora ya vitendo waliyo ipata kwa mataifa yaliyofanikiwa kwenye kilimo
iv, nitaalika wawekezaji wa nje na ndani ya nchi kwenye sekta ya kilimo
V, kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo kuhusu tafiti mbalimbali za kilimo
Vi, kukifanya kilimo kuwa cha kisasa na kilicho bora

*Nitahakisha uwepo wa sera bora itakayo amua uanzishwaji wa viwanda vingi vya Kati maeneo ya vijijini ili vikuze uchumi wa maeneo hayo pamoja na uanzishwaji wa viwanda vichache vikubwa maeneo ya mijini ambavyo navyo vitahakikisha vinakuza uchumi wa maeneo ya mjini.

* Nitahakisha Tanzania inakuwa kitovu Cha biashara barani Africa kwa kuandaa mazingira bora, sheria bora , pamoja na elimu bora ilikuchochea wawekezaji na wafanyabiashara watokao nje ya nchi , pamoja na walio ndani ya nchi wadogo kwa wakubwa ili kuifanya Tanzania kuwa na shughuli nyingi zaidi za kibiashara Africa . Nitaruhusu soko huria litakalokuwa linasimamia ipasavyo na serikali.nitahakikisha na kaa na wafanyabiashara ili kuona namna gani tunasaidiana kukuza sekta ya biashara nchini Tanzania.

* Nitahakikisha Kama taifa tunatengeneza sera zitakazo zalisha wanauchumi wengi pia Wana sayansi wengi ili nchi iweze kupiga hatua .

* Kila mkoa nitahakikisha unakuwa na wanauchumi wabobevu angalau wawili watakaosaidia kupanga sera za kiuchumi kwa kila mkoa watasaidia pia kuona fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana katika mikoa yao na kusaidia serikali za mikoa kuweza kutazama hizo fursa na kuziboresha ili ziweze kuchochea uchumi wa mkoa husika.

* Pia nitahakikisha na shirikiana na serikali niliyoiunda ili kuiwezesha wizara ya utalii kuifanya Tanzania kuwa kitovu Cha utalii barani Africa na dunia kwa ujumla . Hili litawezekana kwa kujifunza kwa mataifa yalifanikiwa kwenye utalii na pia kwa kutenga sera bora zitakazo saidia kukuza na kuimarisha utalii nchi , pamoja na kupunguza sheria ka ndamizi katika sekta ya utalii pia nitamuru wizara ya utalii iendeshwe kisomi na wasomi wanaojua maswala ya kiutalii kiundani zaidi, pamoja na kuweka mazingira bora ya kuvutia kwa watalii, pia kuhamasisha ,kutoa elimu na kutangaza vivutio vyetu vyote vya utalii sehemu mbalimbali dunia. Hii itasaidia kukuza pato la taifa kupitia utalii.

* Kwenye uchumi kiujumla nitapeleka wataalamu wangu waliopo nchini waende kwenye Kama China , Singapore, Korea Kusini , Uingereza, Japan wakajifunze namna gani wameendelea na maswala mbalimbali ya kiuchumi kwenye hizo nchi. Pia nitashirikiana na wachumi mbalimbali wapatikanao ndani ya nchi ili kuunda sera mbalimbali zitakazo saidia kukuza taswira nzima ya uchumi wa Tanzania.

* Nitahakikisha pia rasilimali zote za Tanzania zinawanufahisha pia WATANZANIA wote pasipo ubaguzi wowote au kunufahisha wachache tu.

Ziada: Nitahakikisha tunakuwa na jeshi bora la kisasa lililo na wataalumu na wabobevu katika sekta ya sayansi na teknolojia ili kuhakikisha usalama wa ndani na nje ya nchi yetu ya Tanzania.

Note: Haya yote hayawezi kufanikiwa ndani ya miaka mitano tu au kumi bali lazima yawe na mwendelezo kwa tawala zinazo fuata zaidi hata ya miaka Thelathini au hata arobaini mbeleni.

Ni hayo tu machache kwa leo[emoji404][emoji110]
 
Mi nitamaliza haraka miradi ya kimkakati Nyerere Dam na SGR ili tuanze haraka uchumi wa viwanda

kisha nitahakikisha katiba mpya inapatikana.

Mnasema Vasco da Gama anaupiga mwingi wakati uchumi wetu unashuka kwa kasi ya Mwewe kuchukua kifaranga na sasa eti tunapitwa na Kenya waliojawa na ukame na ufisadi ambao tayari tulishawakanyaga vibaya na kuwachakaza enzi za Mwendazake (Soma data za nyuma).

Soma hapa chini uone difference ya ukuaji uchumi kati ya Tanzania, Kenya na Libya utaacha kupiga piga makofi kama punguani , tuache kusifia tu bila kuwa tunapitia World Bank data.

Mkiambiwa Beijing hawafai kujazana maofisini ila wakae home kulea watoto mnaona tunawaonea wivu kumbe jibu ni kuwa "hawawezi hii ngoma nzito ya wanaume tu"

Data za kupikwa na sukuma gang
 
Back
Top Bottom