Umewahi kujiuliza kwanini Matajiri au watu waliofanikiwa ni wachache Sana kwenye jamii?Je unafikiri kwanini wengi wanashindwa kuupata UTAJIRI?Kuupata UTAJIRI unahitaji NGUVU ziwe za kiroho (za Giza au za kimungu) Ili ufanikiwe.Kwenye Biblia imeandikwa Kumb 8:18 "nawe utamkumbika BWANA Mungu wako maana ndiye akupaye NGUVU za kupata UTAJIRI" Pigia mstari neno NGUVU.
Kwa ufupi, occultism kwa Kiswahili ni imani na vitendo vya kificho vinavyohusu nguvu za ajabu, siri za ulimwengu, na maarifa ambayo si rahisi kuelezeka kwa akili ya kawaida.
NGUVU HIZO ZINAFANYAJE KAZI?
Nguvu hizi Huwa kama Sumaku zikivuta Kila aina ya utajiri kumuelekea anayezimiliki,hivyo huhitajika kufanya ibada Naam lazima ibada iwepo Ili kuzimiliki hizo nguvu.Na ukimuondolea nguvu hizo utashangaa utajiri unapukutika ndani ya siku chache.
UNATAKA UTAJIRI UTAWEZA MASHARTI?
Nimesikiliza visa kadhaa vya Matajiri hapa Tanzania na kwingineko Kila mmoja ana Sharti lake ambalo hutakiwa kulifanya Ili kulinda Mali zake na ukikosea Sharti Hilo athari kubwa hutokea Kwa mhusika.Kiufupi Wengi hufikiria ni biashara tu lakini Kuna NGUVU isiyoonekana nyuma ya biashara unayoiona na ukiiondoa Mali huisha ndani ya muda mfupi.
Kisa 1.KIJANA WA KAHAMA
Kwa umri wake ni miaka 30 hajafika 40 lakini pesa anazomiliki ni hatari,kijana huyu anafanya biashara ya nafaka Kwa jumla mikoa mbalimbali,Dar es salaam,Dodoma na Arusha.Kijana anasema akimuona mtoto anaenda shule huhuzunika Sana maana alipewa Sharti kuwa hawezi kupata mtoto Kwa namna yoyote Ile.Alioa na mke akawa anahangaika na Kila aina ya tiba za kisasa na kienyeji Hadi makanisani bila mafanikio ikabidi jamaa amwambie hali halisi,MKE alimkimbia.Kiufupi pamoja na pesa ndefu alizonazo ni mtu wa huzuni Sana Huwa anajitahidi kupata warembo mbalimbali na kuwahonga Ili tu apoteze muda lakini maisha yake yamejaa majuto.Anatamani Sana kuwa na mtoto na anapenda hata kuwapa zawadi lakini ndiyo hivyo Tena.
MKINGA ALIYEKOSEA MASHARTI,
Unaambiwa MKINGA mmoja alipewa Sharti kuwa asiwahi kufua nguo yake ya ndani na katika shughuli zake rasmi aivae Kila siku.Bahati mbaya hakumweleza mkewe juu ya Sharti Hilo ikatokea siku jamaa kupumzika ndani kwenye jengo lao,MKE kaona mbona hii boxer chafu Sana akaamua kuifua,baada ya siku chache yeye mhusika na mke wake wote walipata ukichaa,yaani Kwa sasa wote wanaokota makopo.
MPARE NA SIRI YAKE,
Tajiri mmoja wa kipare anafanya biashara ya vifaa vya ujenzi yaani Hardware amepewa Sharti la kufuga Chatu ndani,baada ya muda ishara fulani zikitokea yeye na mke wake huingia chumbani alimo huyo Chatu,na Kwa namna ya ajabu wanaingiliwa kimwili! Baada ya muda hutoka na kuendelea na biashara zao kama kawaida na wanazidi kufanikiwa.
Visa ni Vingi,Je inawezekana kupata UTAJIRI bila kuwa na nguvu?Jibu ni HAPANA ukiona tajiri yoyote mkubwa lazima awe na nguvu za kiroho ni lazima aidha awe MWANGA au GIZA ukiwa neutral hautoboi.
Biblia imeandika Mkumbuke Mungu wako akupaye NGUVU za kupata UTAJIRI,na UTAJIRI wake Huwa hauna MAJUTO lakini pia hauna Shortcuts
Haya niitieni
Mshana Jr ,na wataalam wa ulimwengu wa kiroho waje kutuelimisha.