CONSULT
Senior Member
- May 8, 2011
- 194
- 204
NAMNA MOJAWAPO WAJASIRIAMALI WANAVYOPATIKANA
Palikuwapo na nchi tajiri pia na mfalme wake tajiri sana na alikuwa mzee sana kwa bahati mbaya hakujaliwa kupata mtoto wa kiume ila alikuwa na binti mmoja tu na mrembo sana,
Mila na desturi za kabila hilo hazikuruhusu nchi hiyo kutawaliwa na mwanamke, ila ililazimu atakayekuwa mume wa huyo binti mfalme ndie atakae rithi ufalme (kingdom) hali hiyo ilimfadhaisha sana mfalme pia na jamii yote ya hiyo nchi, moja ya maswali mazito waliokuwa wakijiuliza ni namna gani vijana wa kijijini hapo watakavyo posa huyo binti mrembo na tajiri sana wa mfalme ? ?
Kwa upande mwingine Mfalme alijiuliza ni kwa namna ipi atapata mkwe shupavu, hodari, mwenye karama ya uongozi atakaye mkabidhi mwanae pekee pia ufalme wa nchi yake yenye neema na utajiri na amani ? ? Lakini aligundua kuwa kwa tabia zote "ujasiri na ushupavu" ni muhimu sana katita utawala wa falme yeyote ile (risk taking) na lazima atoke hapo hapo.
Mfalme akaandaa namna ya kumpata mrithi wake/ mkwe wake/ mfalme mpya, akaamua kuchimba swimming pool kubwa nyembamba ndefu na yenye kina kirefu pia ndani yake akafuga mamba wengi sana wakilishwa mbuzi wazima wazima kila kukicha, penbeni kushoto na kulia kumejengwa kingo ndefu na uzio wa waya isipokua tu mwanzo wakuingilia na mwisho ng'ambo ya pili pa kutokea na mamba ni wengi na wakubwa sana.
Siku ya siku ilipowadia mfalme akawambia wafuasi wake kugonga kengele kwa ajili ya watu wote wakusanyike pale penye swimming pool vijana wa kiume waliokuwa tayari na umri wa kuoa ndio wawe mbele akawatangazia watu wote kama ifuatavyo " Nadhani mnaniona umri wangu umeenda sana kuendelea kuwa mfalme wenu , na mnajua kuwa sina kijana wa kiume ila nina binti pekee , na atakaye muoa ndie atakuwa mfalme wa nchi yenu hii, pia ni lazima awe jasiri hakika, na lazima atoke kati yenu nyie vijana,
Kwa maana hiyo bwawa hili nimeliandaa ili kumpata mfalme jasiri na hodari na ndani ya bwawa hili mnawaona hao mamba, (wakati huo mfanyakazi mmoja akatupa mbuzi mmoja wakanyakuana kwa fujo sana walikuwa na njaa) Mimi nasema kijana jasiri ni yule atakaye jitosa kupambana na hawa mamba kwa kuogelea kutoka ng'ambo hii na kuvuka hadi ng'ambo ya pili atakuwa amefaulu na huyo ndie ntakaye mkabidhi mwanangu pekee na ufalme wa nchi hii SASA HIVI"
Basi baada ya kumaliza usemi huo minonyono na miguno ikawa mingi sana baadaye pakapitwa na ukimya wa dakika kadhaa watu wakitafakari mtihani mzito sana wa mfalme, vijana wakitaniana wao kwa wao, wengine wakirudi nyuma la kufanya hawana na pia binti mfalme yupo akiduwaa ! !
HHHHEEEIIIIII Mungu wangu Ghafla bila kutarajia akatokea kijana mmoja akaruka ndani ya maji nayo yakaruka duuubwiiii watu wakapiga makelele jamani analiwa huyo o o o na mamba wakaruka kila mmoja kumng'ata wengine wakigongana midomo juu kwa juu na kumwacha chini na yeye kila akitokeza na kuwaona walipo anazama kupiga mbizi chini kwa chini, ilikuwa pata shika watu wengine wakishika vichwa wengine walisha anza kupiga mayowe na kulia, kumbuka mungu sio athmani hatimaye ghafla kijana anatokeza ng'ambo ya pili na mikwaruzo ya kucha za mamba damu zinavuja bila shati wala kaptura, na kuhema kwa wingi sana na kuaguka ukingoni papo hapo huku mfalme akiruka kumpokea na akishangilia na kuwahamasisha watu kumpokea mfalme mpya kwa shangwe sana,,, HAPANA ! ! HAPANA ! ! ! SITAKI ! ! ! SITAKI ! ! ! Ningekufa je ? ? ningekufa je ? ? Watu waka shangaa tena waka pigwa na butwaa ,,, kijana akaendelea kutoa maneno huku akihema ovyo NANI KANISUKUMA ? ? NANI AMENISUKUMAA ? ? watu wakaendelea kustaajabu , kasukumwaa ? amesukumwa na nani tena ?
Kumbe kilichotokea ni hivi, kama ilivyo mzaha mzaha na utani wa vijana na hasa kwa wale wanaojiona ni bora kuliko wenzao kilitokea kikundi kimoja kikala njama ya kumsukuma kijana wa watu hajui lile wala hili wakijuwa wazi kuwa lazima ataliwa na mamba awe jaribio la kupima hiyo hatari ( sijui ni chambo ?) (wale wasoni mtasema ? RISK ASSESSMENT)
Lakini Mfalme hakuwa na muda tena wa kusikiliza hayo kwani alikuwa na furaha sana sana kwa kumpata mwanae wa kiume /mrithi wake/ mkwe wake/ na akamkumbatia kwa furaha kuu na wanachi wote pia ngoma na vigelegele sherehe ikaendelea hatimaye si kijana ni MFALME MKUU wale vijana waliomsukuma wakazubaa na kustaajabu wengine wakakimbia kwa kuogopa kukamatwa na mfalme mkuu aliwasamehe.
Ndg zangu mfano huu ni namna mmojawapo wanavyopatikana wajasiriamali maarufu sana na kufaulu sana kimaisha kijana mfalme alijikuta yuko kwenye maisha HATARI SANA - KUFA AU KUPONA alichokifanya ni kuokoa roho yake/maisha yake na sio ufalme na pengine hakuwahi hata kidogo kuwaza ufalme ghafla akipigania roho yake ghafla anaibuka na Ufalme, Utajiri, Mke binti Mrembo sana mwana wa mfalme,
Ni hivyo hivyo inavyotokea kwa baadhi ya wajasiriamali unakuta amezaliwa kwenye lindi kubwa la umaskini au namna ya tabu kubwa sana ambayo inatishia uhai wake hivyo anakuwa anapigania kuokoa uhai/maisha yake hatimaye anapata ka-mwanga ka-maisha/ka-unafuu na kumtia moyo nae kukandamizia hapo hapo kwa mbinu hizo hizo za kufa na kupona mwisho anajikuta inakuwa ndio tabia yake na ndio raha yake mwisho watu wanashangaa yuko hatua kubwa na mbali sana TAJIRI HUYO.
ILI KUBORESHA ZAIDI HADITHI HII TUNAOMBA MAONI YENU HASA HEADING , MAIN STORY, etc