KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
Nchi nyingine vitengo vya intelligence vinajaza watu wenye akili kubwa, na maono mapana. Idara yetu inajaza makada tu wa CCM ambao hawana tija wala uwezo wa kuishauri serikali ifanye nini ili ijikwamue na huu umasikini unaolimaliza taifa, ndio maana utaona machawa wa mama wanazunguka ndani na nje ya nchi kwa kodi zetu na hawana mchango chanya wowote kwa taifa letu. Mfano, Steve Nyerere alienda India kwa gharama zetu kufanya nini? Hii ni kashfa kwa idara ya usalama wa Taifa, ilitosha kabisa kumtoa Mkurugenzi wa Idara Ofisini.
Mimi sio mwanasiasa wala mtu wa lawama, ni mtu wa solutions. Kama mimi nilikuwa fukara na leo nimekuwa TAJIRI MKUU WA MATAJIRI basi naamini kwamba naweza kuishauri serikali iyatumie mawazo na fikra zangu ili iweze kujinasua na ufukara na kutunisha akiba yake ya fedha za kigeni.
Leo nitaongelea eneo moja tu, ambalo serikali inaweza kuokoa mamilioni ya dola kwa mtaji kidogo tu na ika stabilise uchumi na kupunguza sana utegemezi.
Tanzania tumekuwa watumwa wa kiuchumi. Hatuna uwezo wa kudhibiti mfumuko wa bei unaosababishwa na soko la mafuta ulimwenguni, kwa kuwa tunahitaji mafuta kwenye shughuli zetu za kila siku, lakini hatuzalishi mafuta. Hivyo tunatumia mamilionibya fedha za kigeni kuagiza mafuta.
Nini tufanye?
Serikali isambaze vituo vya kujazia gesi asilia nchi nzima. Badala ya JWTZ kufungua ma bar, kumbi za harusi na ma fremu, wasaidiane na TPDC kuweka vituo vya kujaza gesi asilia nchi nzima.
Itungwe sheria kali kwamba Magari yote ya serikali, ya binafsi, ya abiria na mizigo yafungwe mfumo wa kutumia gesi asilia.
Gesi asilia ni shilingi 1,500/ kwa kilo na inakupeleka zaidi ya mara mbilì ya umbali ambao mafuta yangefika. Bei ya mafuta ni zaidi ya 3,000 na bei inazidi kupanda na hatuna namna ya kudhibiti mfumuko huo.
Kwa kufanya hivi, serikali itaokoa mamilioni ya dola zinazopotea kwenye uagizaji wa mafuta.
Pia serikali itaweza kudhibiti upandaji holela wa nauli, hii itapelekea mwananchi kupata huduma kwa bei nafuu kwani gharama za usafiridhaji zitakuwa chini.
JamiiForums under Maxence Melo wazo hili wapeni wizara ya fedha na wizara ya nishati. Wakiona lina tija walifanyie kazi, kama wanapenda kubaki na umasikini wa wananchi, basi tuendelee na mfumo uleule wa miaka yoye.