SoC04 Utajiri uliojificha kwenye ardhi

SoC04 Utajiri uliojificha kwenye ardhi

Tanzania Tuitakayo competition threads

RodrickMaro

New Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2
Reaction score
1
Tanzania Bara, kila halmashauri ina idara ya ardhi inayosimamia masuala yote ya ardhi chini ya Kamishna wa Ardhi. Ni muhimu kila mmiliki wa ardhi awe na hati/cheti halisi cha hakimiliki kuthibithisha haki yake ya kumiliki ardhi kisheria.

Hati/cheti cha hakimiliki ya kimila chini ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5 ya 1999 kina hadhi sawa na hati/cheti cha hakimiliki ya ardhi chini ya Sheria ya Ardhi Namba 4 ya 1999.

Hata hivyo, ardhi ambayo haijapimwa haichangii mapato ya Serikali Kuu wala zile za Mitaa, na kama upo, basi ni mchango mdogo sana kulinganisha na jinsi ambavyo ingepaswa. Ili kuongeza mapato haya, Serikali inatakiwa kuhakikisha Halmashauri zina viwanja vilivyopimwa visiyopungua 100,000 ndani ya miaka mitano.

Wananchi wanatamani kumiliki ardhi iliyopimwa na mara nyingi wametapeliwa na makampuni binafsi wakijaribu kurasimisha ardhi zao. Halmashauri zinaweza kutumia wanafunzi kutoka vyuo vya ardhi kwa kusaidiana na maafisa husika katika kupima ardhi. Ardhi hii itamilikishwa kwa wananchi kisheria, na ambao watalipia gharama za urasimishaji, na wasio na uwezo watalipa kidogo kidogo wakati wa kulipa kodi ya ardhi.

Serikali itapata mapato kwa kuuza viwanja hivyo. Kwa halmashauri 184 za miji na vijiji, vitapatikana viwanja 18,400,000 katika kipindi pendekezwa cha miaka mitano. Kwa mfano, kwa kodi ya ardhi ya sh. 10,000/= tu kwa kila mita za mraba, mapato haya yatasaidia kujenga miundombinu na miradi mingine ya maendeleo. Wananchi pia watafaidika kwa kumiliki ardhi iliyopimwa, ambayo wataweza kutumia kama dhamana kupata mikopo kutoka taasisi za fedha.

Pamoja na faida za kiuchumi tajwa, kwamba Halmashauri zitaweza kuzalisha fedha na wananchi kuweza kuwa na sifa za kukopesheka kwenye Taasisi za Fedha, ni dhahiri pia kwa kurasimisha ardhi kutapunguza sana kama si kumaliza migogoro mingi ya ardhi inayogharimu rasilimali nyingi na muda kwa vyombo vya utatuzi na wa wadaawa.

Pia urasimishaji wa Ardhi hufanya Utambuzi wa kisheria kwa mmiliki halali wa kipande cha ardhi; huongeza thamani ya Ardhi; na huweka usalama katika ardhi, hivyo kuzuia mtu awayeyote kujimilikisha au kufanya shughuli yoyote katika ardhi bila ridhaa ya mmiliki halali.

Kwa kuzingatia Tanzania tuitakayo, ni vema kutumia vitengo vya Ardhi kwa kila Halmashauri zetu nchini ili kuweza kurasimisha ardhi kwa wamiliki halali badala ya kuwa wasimamizi tu wa ardhi (kidogo) iliyopimwa. Badala yake, wakifanya zoezi la uarasimishaji wa ardhi, pia Halmashauri hizi zitakuwa ni VITENGO VYA KUZALISHA MAPATO (kupitia kodi ya pango la ardhi), miongoni mwa faida nyingine nyingi, kama zilivotajwa hapo awali.
 
Upvote 2
Wananchi wengi sana wametapeliwa kwenye kutumia pesa zao wenyewe kupima viwanja na makampuni binafsi. Mwisho was siku serikali nao ni wanufaika maana ukishapima wanakudai kodi ya ardhi. Ardhi haitambuliki, haina dhamani na haina mchango wowote kwenye serikali kama haijapimwa
 
Back
Top Bottom