SoC04 Utajiri Uliojificha Kwenye Koti La Kimaskini, Ni Mda Muafaka Sasa Wa Kulifufua. Iundwe Wizara Mpya Ya Sayansi ,Technologia na Uvumbuzi

SoC04 Utajiri Uliojificha Kwenye Koti La Kimaskini, Ni Mda Muafaka Sasa Wa Kulifufua. Iundwe Wizara Mpya Ya Sayansi ,Technologia na Uvumbuzi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mdeke_Pileme

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2013
Posts
1,596
Reaction score
2,226
TANZANIA TUITAKAYO NA MAARIFA YA KUJITEGEMEA.
Binadamu tunakabiliwa na changamoto kubwa za kimaisha ambazo zinahitaji suluhisho hasa katika masuala ya kiteknolojia. Ikiwa ni pamoja na jinsi ya kufikia maendeleo endelevu ya Tanzania Tuitakayo, hapa tunaongelea kuchochea uchumi wa masoko wenye maadili na kupambana na umaskini mpya na ule unaoendelea hadi sasa. Ingawa taswira inaweza kuonekana kuwa ni njia ya kuchosha katika upambanaji, lakini kikawaida binadamu wanashinda zaidi ya kushindwa , hasa lile eneo tunaloshindwa tukiamua kulitilia maanani. Changamoto hizi Zinahitaji hatua za ushirikiano kati ya serikali yenyewe, mashirika binafsi , vyuo vikuu, na watu wenye ubunifu au wavumbuzi wa masuala ya teknolojia ikiwa tu watashikwa mkono. Tunahitaji mawazo yakinifu kuhusu ukuaji endelevu. Kama watu na taasisi hakutakuwa na mikakati ya kushughulikia changamoto kama vile, mfumuko wa bei, kuishi kwenye teknolojia duni, mabadiliko ya tabia ya nchi, uhaba wa ajira kwa wananchi. Basi hali mbaya zaidi zinaweza kutokea kwa miaka ijayo katika jamii husika. Hivyo Tanzania tuitakayo haitakuwepo.



NDUGU ZANGU WATANZANIA , HAPA TUTAJIKITA ZAIDI KUHUSU MASUALA YA UVUMBUZI WA TEKNOLOJIA NA FAIDA ZAKE.
Teknolojia ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu ya leo na inaleta faida nyingi kwa kila mwananchi. Tunaweza kuzungumzia mambo kama vile mawasiliano rahisi, ufikiaji wa habari, na njia za kuboresha maisha kupitia teknolojia hasa katika upande wa ajira. Kuna maeneo mengi ya kuvutia ya kujadili lakini leo nitazungumzia faida za kuweka mikakati ya misingi imara katika masuala ya uvumbuzi hapa Tanzania.
1. Mvumbuzi/Mgunduzi, Kuvumbua vifaa vya kiteknolojia kunatoa fursa za biashara. Mvumbuzi atauza teknolojia hiyo kwa kampuni za utengenezaji au kuanzisha biashara yake mwenyewe.​
2. Mtumiaji, Urahisi wa Mawasiliano, Watumiaji watapata faida kubwa za kiuchumi kwa kupata teknolojia rahisi na kwa bei nafuu.​
3. Wafanyakazi, Ajira na Ukuaji wa Viwanda, Uvumbuzi wa Teknolojia itasaidia kuundwa kwa ajira mpya na zakutosha katika sekta za utengenezaji, uuzaji, na matengenezo ya vifaa vyake.​
4. Ujuzi na Mafunzo, Watu kupata mafunzo ya ufundi na ujuzi wa kiteknolojia kuhusiana na utengenezaji na matengenezo ya vifaa, ambavyo vinaweza kuongeza ujuzi wao na fursa za kazi katika jamii.​
5. Serikali kupata Mapato na Ukuaji wa Uchumi, Sekta ya teknolojia itachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kupitia kodi na mapato ya biashara.​


Nchi zilizoendelea zinaweka mkazo mkubwa kwenye uwekezaji wa teknolojia kwa sababu teknolojia inajukumu muhimu katika kukuza uchumi, kuboresha maisha ya watu, na kusaidia maendeleo ya kijamii.
Baadhi ya Mifano ya nchi zilizowekeza zaidi kwenye masuala ya uvumbuzi wa teknolojia na kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi walioajiriwa katika sekta ya teknolojia.
1. Marekani, inajulikana kuwa kitovu cha uvumbuzi wa teknolojia duniani, hasa katika maeneo ya Silicon Valley huko California. Idadi ya wafanyakazi walioajiriwa katika sekta ya teknolojia nchini Marekani inakadiriwa kuwa milioni 12.1 kuanzia wahandisi, wataalamu wa programu, wauzaji wa teknolojia, na wafanyakazi wengine katika sekta hiyo.​
2. China, imekuwa ikiongeza uwekezaji wake katika utafiti na maendeleo ya teknolojia, ikilenga kuboresha uwezo wake wa kiteknolojia na uvumbuzi. Sekta ya teknolojia ya China inakdiliwa kuajiri watu milioni 10.5 , ikijumuisha wahandisi, wataalamu wa teknolojia ya habari, na wafanyakazi wa tasnia ya utengenezaji wa vifaa vya elektroniki.​
3. Japan, imekuwa ikiongoza katika uvumbuzi wa teknolojia kwa miongo kadhaa, na inaendelea kuwekeza katika maeneo kama robotics, uhandisi wa magari, na teknolojia ya habari. Idadi ya wafanyakazi katika sekta ya teknolojia nchini Japan inafikia million 3.5.​
4. Ujerumani, ni moja ya nchi zinazochangia sana katika uvumbuzi wa teknolojia, hasa katika maeneo ya viwanda, nishati mbadala, na magari. Idadi ya wafanyakazi walioajiriwa katika sekta ya teknolojia nchini Ujerumani inakadiriwa kuwa million 3.2, ikijumuisha wahandisi, wataalamu wa IT, na wafanyakazi wengine wakawaida.​
5. Korea Kusini, imekuwa ikionyesha maendeleo makubwa katika uvumbuzi wa teknolojia, hasa katika sekta ya uvumbuzi wa elektroniki na mawasiliano. Idadi ya wafanyakazi katika sekta ya teknolojia nchini Korea Kusini inakadiliwa kuajiri watu million 2.5 , ikijumuisha wahandisi, wataalamu wa IT, na wafanyakazi wa tasnia ya utengenezaji. Mpaka hapo tutaona kunafaida kubwa sana kwenye sekta ya sayansi, uvumbuvi wa teknlojia .​

Orodha ya Wizara zilizopo Tanzania, zinajukumu kubwa la kusimamia na kutekeleza sera za serikali katika maeneo mbalimbali ya kiutawala na maendeleo ya nchi. Kila wizara ina majukumu yake maalumu yanayohusiana na sekta au eneo maalumu la utawala na maendeleo ya jamii, orodha ya wizara zilizopo nchini Tanzania.
1. Wizara ya Kilimo,
2. Wizara ya Mifugo na uvuvi,
3. Wizara ya Afya,
4. Wizara ya Ujezi,
5. Wizara ya Fedha,
6. Wizara ya Madini,
7. Tamisemi,
8. Wizara ya Maji,
9. Wizara ya Kalimo na sheria,
10. Wizara ya Viwanda na biashara,
11. Wizara ya Uchukuzi,
12. Wizara ya Maliasili na utalii,
13. Wizara ya Muungano na mazingira,
14. Wizara ya Mipango na uwekezaji,
15. Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Africa mashariki,
16. Wizara ya Utamaduni ,Sanaa na michezo,
17. Wizara ya Ardhi , nyumba na maendeleo ya makazi,
18. Wizara ya Elimu , sayansi na teknolojia,
19. Wizara ya Habari mawasiliano na teknolojia ya habari.


Hapa tutajikita kwenye mabadiriko ya wizara mbili.
1. Wizara ya Elimu, sayansi na teknolojia.​
2. Wizara ya Habari , mawasiliano na teknolojia ya habari.​


MAPENDEKEZO: WIZARA HIZI MBILI ZIPUNGUZIWE MAJUKUMU YA KIUTENDAJI ILI KUENDANA NA WAKATI, HAPA IUNDWE;-.
1. Wizara ya sayansi , teknlolojia na uvumbuzi - ijikite zaidi kwenye uvumbuzi wa teknolojia mbali mbali na kuhakikisha uvumbzi huo unaleta matunda kwa taifa.​
2. Wizara ya elimu - isimamie ubora wa elimu.​
3. Wizara ya habari na mawasiliano- isimamie ubora wa habari na wasiliano.​


Wizara ya sayansi, teknolojia na uvumbuzi - Kuanzisha Wizara mpya ya Sayansi, Teknolojia na uvumbuzi ni hatua muhimu sana katika kuimarisha maendeleo ya kitaifa na kukuza uchumi wa nchi. Kwa kuzingatia maendeleo ya haraka ya sayansi na teknolojia duniani kote hivi sasa, na kwa kuwa tunataka kuelekea kwenye uchumi wa Tanzania tuitakayo na maarifa ya kujitegemea, ni muhimu kuchukua hatua madhubuti za kukuza uvumbuzi na ubunifu katika nyanja zetu za kiuchumi, afya, mazingira, na jamii kwa ujumla.

Kupitia Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi, tunaweza kuanzisha sera na mikakati itakayowezesha:
1. Kuongeza uwekezaji katika utafiti na uvumbuzi.​
2. Kusaidia kuibua na kukuza talanta na ubunifu miongoni mwa vijana.​
3. Kuanzisha mazingira bora ya kuvutia wawekezaji katika teknolojia na uvumbuzi.​
4. Kuendeleza miundombinu ya kisasa ya teknolojia inayovumbuliwa na vijana.​
5. Kuhakikisha kwamba kila mradi unaoazishwa uwe na mkakati wa uzalishaji ajira za kutosha na kukuza uchumi wa taifa.​


Faida na ongezeko la ajira zitakazojitokeza katika Uvumbuzi wa mradi/miradi hapa nchini Tanzania,
Mradi wa uvumbuzi wa mitambo mbalimbali itatoa ajira kwa maelfu ya watu kutoka sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wataalamu wa utafiti, wahandisi, mafundi, wafanyakazi wa ujenzi, wafanyakazi wa uendeshaji, na watoa huduma za usaidizi.
1 • Kuajiri Wataalamu na Wahandisi, Ujenzi na uendeshaji wa mtambo unahitaji wataalamu wenye ujuzi wa uhandisi wa mitambo watahitajika Watu takribani 30 hadi 50.​
2• Wafanyakazi wa Uendeshaji na Matengenezo, Baada ya ujenzi kukamilika wa mtambo utahitaji wafanyakazi wa kudumu na wasio wa kudumu kwa ajili ya uendeshaji na matengenezo ya kila siku. Watahitajika Watu takribani 100 hadi 200.​
3• Faida kwa jamii na Huduma za Msaada, Miradi mikubwa kama hiyo huunda mahitaji ya huduma za kijamii kama vile makazi, huduma za afya, na usafirishaji, ambayo hutoa ajira kwa watu katika sekta mbalimbali. watahitajika Watu takribani 800 hadi 1000.​
4• Viwanda na Sehemu ya Matengenezo, Uvumbuzi pia unaweza kuongezea uanzishwaji wa viwanda vya kutengeneza sehemu za mitambo na huduma za matengenezo, ambayo pia itatoa ajira kwa watu takribani 300 hadi 600.​


Faida za Uajiri katika Miradi ya Uvumbuzi, Miradi ya uvumbuzi huchochea maendeleo ya ujuzi na ubunifu kati ya wataalamu na vijana, ambao huleta tija kwa uchumi kwa muda mrefu. Kuongeza Ushindani katika Soko, Kuwa na miradi ya uvumbuzi inayofanikiwa italeta sifa nzuri kwa taifa na kuwavutia wawekezaji na wataalamu kutoka nje, hii itaongeza uwezo wa kiuchumi na kijamii katika taifa.


Tukiangalia baadhi ya mifano ya vijana wavumbuzi wa mitambo kutoka hapa Tanzania, wamegundua mitambo mingi Sana lakini haijeleta matokeo chanya hata kidogo ndani ya Taifa letu, baadhi ya watanzania waliovumbua mitambo hapa Tanzania ni.
1. Deogratius Lukas Charles, umri miaka 31, Mkazi wa Bungu Tanzania - Aliyebuni ndege aina ya DIH - 92 .
Screenshot_20240506-220831.png



2. Rojas Mathayo msuya, umri miaka (.......) , Mkazi wa kawe- Dsm , aliyebuni mtambo wa umeme unaotumia sumaku, pia Ni mtu wa Kwanza na pekee hapa duniani aliyebuni helicopter inayotumia nguvu ya sumaku kupaa angani.
Screenshot_20240507-165817.png



3. Faruku Hassan khalifa, umri miaka 43, Mkazi wa Turian, elimu darasa la Saba, aliyebuni mtambo wa kufua umeme.
screenshot_20240507-172329-png.2983899



4. Zuberi Ismail, kutoka kigoma ujiji, umri miaka(........), aliyebuni Radio( kigoma Fm 87.5 inayoshika umbali wa masafa mita 150) alibuni mtambo ndani ya mienzi mi nne, pia alifanikiwa kubuni pikipiki ndogo.
Screenshot_20240507-175400.png




5. Mwanadada aliyegundua njia ya kukontrol umeme kwa kutumia kivuli ( jina lake halisi sikufanikiwa kulipata), Mkoa wa Iringa, ( chanzo cha taarifa YouTube channel @jimmykyando.9992)




6. Frank Leonard shauri , mkazi wa mwasenga -kigoma ,Tanzania. umri miaka 23, elimu kidato Cha nne , aliyebuni video mixer ( video dj) inayotumia baadhi ya vifaa ikiwemo kadi ya bank.
Screenshot_20240506-134002.png



7. Said honza , kutoka mkoa wa tanga, umri miaka (.......), aliyebuni mnara wa simu( little base transmitter station),:alitengeneza mtambo huo ndani ya mienzi mi nne , mtambo huo unatumia betri inayokidhi uwezo wa volti tano ili mtambo uwake.
Screenshot_20240506-135358.png



8. Anwari Athuman Kivunuga , umri miaka (.........), Alihitimu kidato Cha nne Shule ya Sekondari Anzania mwaka 2021, ni mbunifu wa magari pamoja na Scavators.
Screenshot_20240507-162738.png


.Hii Ni baadhi tu ya mifano ya wavumbuzi ambayo nimeambatanisha katika chapisho langu... Lakini kuna watanzania wengi sana wenye uwezo wa kubuni mitambo mbali mbali ambayo inaweza kutufikisha sehemu sahihi hasa katika maarifa ya kujitegemea na Tanzania tuitakayo. Naomba kuwasilisha 🤝🤝.
 

Attachments

  • Screenshot_20240507-172329.png
    Screenshot_20240507-172329.png
    898.5 KB · Views: 35
Upvote 8
1. Mvumbuzi/Mgunduzi, Kuvumbua vifaa vya kiteknolojia kunatoa fursa za biashara. Mvumbuzi atauza teknolojia hiyo kwa kampuni za utengenezaji au kuanzisha biashara yake mwenyewe.
Ni ndoto nzuri kuwa na kampuni zinazonunua teknolojia mpya na kuzibiasharisha. Nadhani pia SIDO ama COSTECH kuna mmoja analo jukumu linaloendana na hilo.


2. China, imekuwa ikiongeza uwekezaji wake katika utafiti na maendeleo ya teknolojia, ikilenga kuboresha uwezo wake wa kiteknolojia na uvumbuzi. Sekta ya teknolojia ya China inakdiliwa kuajiri watu milioni 10.5 , ikijumuisha wahandisi, wataalamu wa teknolojia ya habari, na wafanyakazi wa tasnia ya utengenezaji wa vifaa vya elektroniki.
Waliwekeza sana hawa jamaa, hasa kule Shenzen, China's Silicon Valley. Na kweli hadi kufikia sasa uwekezaji wao umelipa maana China ndiye anayeongoza kwa hatimiliki za teknolojia mpya hadi sasa 'patents'
 
SEma kitu kimoja, katika mifano ya uvumbuzi uliyoitoa naomba kuuliza.
Je bunifu hizo ni mawazo mapya? Na katika yale yasiyokuwa mapya je inaleta taarifa mpya? Yaani tafiti zao kuna nafasi (gap)zinajazia kwenye teknolojia iliyopo?

Nauliza hivyo ili tusije kurudisha nyuma maendeleo, na tukatengeneza kitu kisichoweza kuuzika kibiashara. Mfano mchina aliyegundua 5g ni maboresho kwenye 4g hivyo inabiasharishika. Lakino mtanzania aliyeunda helicopter je ni maboresho kwa apache zilozopo? Au labda yake inapanda juu kwa kasi zaidi, na mzigo mzito zaidi? Ili isije kuwa yake ndio hata kuruka hairuki hapo tutakuwa tunampa moyo bure. Sambamba na aliyevumbua umeme wa sumaku, je ina ubora zaidi ua teknolojia ya majenereta yalipofikia?. Huyo wa mnara unaweza kuta amepata teknolojia isotumia nishati kubwa sana, au kaipunguza ukubwa vyovyote vile ni lazima uvumbuzi uwe ni aidha kipya au maboresho ya kakipengele fulani.

Vinginevyo kama lengo letu ni maonesho na kusisimua udadisi wa watoto tu hapo sawa
 
SEma kitu kimoja, katika mifano ya uvumbuzi uliyoitoa naomba kuuliza.
Je bunifu hizo ni mawazo mapya? Na katika yale yasiyokuwa mapya je inaleta taarifa mpya? Yaani tafiti zao kuna nafasi (gap)zinajazia kwenye teknolojoa iliyopo?

Nauliza hivyo ili tusije kurudisha nyuma maendeleo, na tukatengeneza kitu kisichoweza kuuzika kibiashara. Mfano mchina aliyegundua 5g ni maboresho kwenye 4g hivyo inabiasharishika. Lakino mtanzania aliyeunda helicopter je ni maboresho kwa apache zilozopo? Au labda yake inapanda juu kwa kasi zaidi, na mzigo mzito zaidi? Ili isije kuwa yake ndio hata kuruka hairuki happ tutakuwa tunampa moyo bure. Sambamba na aliyevumbua umeme wa sumaku, je ina ubora zaidi ua teknolojia ya majenereta yalipofikia?. Huyo wa mnara unaweza kuta amepata teknolojia isotumia nishati kubwa sana, au kaipunguza ukubwa vyovyote vile ni lazima uvumbuzi uwe ni aidha kipya au maboresho ya kakipengele fulani.

Vinginevyo kama lengo letu ni maonesho na kusiaimua udadisi wa watoto tu hapo sawa
wanatakiwa kupatiwa elimu zaidi,pia kukua kwa teknolojia hakumaanishi kuwa hakuna watu ambao watakaotumia hii mifumo ya zamani coz teknolojia mpya ni gharama hivyo ni vyema kuwatunza hawa jamaa but kwa bahati mbaya watakuwa wanauza madafu au chawa kwa sasa.
 
wanatakiwa kupatiwa elimu zaidi,pia kukua kwa teknolojia hakumaanishi kuwa hakuna watu ambao watakaotumia hii mifumo ya zamani coz teknolojia mpya ni gharama hivyo ni vyema kuwatunza hawa jamaa but kwa bahati mbaya watakuwa wanauza madafu au chawa kwa sasa.
Yas elimu, inakuwa kama waleta mada mbalimbalinwanavyosisitiza programu za uatamizi wa uvumbuzi wa hawa wabunifu wetu.

Sawa sawia
 
Bandiko zuri sema kwa nchi za kwetu hasa Tz, tunawaza kuiba kura tu na kujaza viriba tumbo.....
 
SEma kitu kimoja, katika mifano ya uvumbuzi uliyoitoa naomba kuuliza.
Je bunifu hizo ni mawazo mapya? Na katika yale yasiyokuwa mapya je inaleta taarifa mpya? Yaani tafiti zao kuna nafasi (gap)zinajazia kwenye teknolojia iliyopo?

Nauliza hivyo ili tusije kurudisha nyuma maendeleo, na tukatengeneza kitu kisichoweza kuuzika kibiashara. Mfano mchina aliyegundua 5g ni maboresho kwenye 4g hivyo inabiasharishika. Lakino mtanzania aliyeunda helicopter je ni maboresho kwa apache zilozopo? Au labda yake inapanda juu kwa kasi zaidi, na mzigo mzito zaidi? Ili isije kuwa yake ndio hata kuruka hairuki hapo tutakuwa tunampa moyo bure. Sambamba na aliyevumbua umeme wa sumaku, je ina ubora zaidi ua teknolojia ya majenereta yalipofikia?. Huyo wa mnara unaweza kuta amepata teknolojia isotumia nishati kubwa sana, au kaipunguza ukubwa vyovyote vile ni lazima uvumbuzi uwe ni aidha kipya au maboresho ya kakipengele fulani.

Vinginevyo kama lengo letu ni maonesho na kusisimua udadisi wa watoto tu hapo sawa
Mkuu kumbuka hawa watu, mawazo yao yanatoka kichwani., nafasi ikiwepo kuna vichwa vingine vitajitokeza tofauti na hawa wavumbuzi.
 
Naunga mkono hoja
Shukran sana mkuu, tukiangalia hata nchi zilizoendelea, ziliaza na vipaji walivyonavyo nchini mwao. Bila kusimika mizizi ya sayansi hapa nchini kwetu, Hatuwezi kuendelea kiteknolojia hata siku moja.
 
Back
Top Bottom