Huu Ndio Utajiri Unaotambuliwa wa Msanii Diamond Platnumz Jumanne, Oktoba 26, 2021 by Frumence M Kyauke.
Nasibu Abdul Juma Issack, almaarufu Diamond Platnumz, ni miongoni mwa wasanii Afrika wenye vipaji vikubwa na matajiri. Umaarufu wake ni kuanzia mwak wa 2010 baada ya kuachia albamu kwa jina Kamwambie. Bingwa huyo wa muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania tokea hapo amefaniiwa kuachia vibao vikali na vinavyovuma mfano Tetema, Inama, Marry You, Jeje, na cha punde zaidi Waah.
Anamiliki studio kubwa ya muziki na mali nyingi za thamani ya mamilioni ya pesa ambazo inakubidi uzifahamu. Kutokana na mafanikio yake, mali na madili mengine, unahisi Diamond Platnumz ni tajiri kiasi gani?
Bila shaka yoyote Diamond ni kipenzi cha wengi. Kando na kuwa na kipaji, ni mwanamuziki anayeiheshimu kazi yake na anayechapa na kuipenda kazi yake.
Kwa sababu hii pekee, ameweza kupata mafanikio ambayo hakutarajia miaka ya nyuma. Labda hili linaeza kutusaidia kueleza ni kwa nini yeye ndiye mwanamuziki tajiri zaidi Tanzania.
Utajiri wake Diamond Platnumz Je, Diamond Platnumz ni tajiri kiasi gani? Wengi wa mashabiki wake huuliza kila mara. Utajiri wa staa huyo wa Bongo Flava ni mkubwa kutegemea na kazi zake, anavyoishi, mali na uwekezaji. Mnamo mwaka wa 2014, utaji wa Diamond Platnumz ulikisiwa kuwa wa thamani ya dola za Marekani $4 milion
View attachment 1988269