Nilishakuja na uzi apa unaohusu aina za utajiri ambazo ni common Tanzania ukiwemo utajiri ambao mtu anapewa kidonda ambayo kadiri kinavoongezeka ndo pesa inaongezeka
Ila amini kwamba shetani awezi kukuacha utumie pesa zake bila mateso😂😂
Finally nimekutana na jamaa ambaye alichukua utajiri huo, pesa kweli anayo lakini hicho kidonda kinavonuka kudadeki asikwambie mtu.
Jamaa hapendezi yaani yupo yupo tu😂 nguo izo izo siku tatu.
Ni hovyo tu, tutafute hela wajumbe katu usifikiri kuna pesa ya rahis rahisi
Ni dhahiri unaona jamaa hafurahii ile pesa.
Ukisikia kafara za kichawi au za mizimu ndio hizo.... yaani wanakutesaaa halafu wanakupa Mali ya kukutana na baadae wanakukula nyama
Na hapo unawezakuta ana sharti la kutokulala kitandani au ndani ya nyumba yake nzuri. Na hatakiwi kujisaidia kwenye choo cha kisasa
Uchawi ni uchafu na upumbavu mkubwa sana
MHUBIRI 5:1
"Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya."
UFUNUO 5:5-10
"Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.
Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.
Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi. Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, akawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi."