Siku ile asubuhi asubuhi tukielekea lab (maabara) nilipata historia fupi iliyomuhusu Catarina. Hapo sasa nilipata picha japo kwa uchache nimeweza kuijua background ya Catarina.
Lakini kwa upande wa Manuela ilikua ngumu kwani ilionekana kabisa ata Javier mwenyewe hakujua chochote kuhusu background ya Manuela.
Tulipofika lab (maabara) ilikua ni asubuhi sana lakini Catarina na mwenzie walishafika hapo mapema sana wakiendelea na maandalizi mengine. Na sisi bila kuchelewa tulijiunga kuendelea na majukumu ili kuhakikisha tunata products kwa wakati.
Mimi na Javier tulianza kwa kusafisha zile drums au mapipa yaliyokua yamekatwa eneo la mfuniko. Mapipa haya yalikua muhimu sana kwenye hizi hatua za mwanzo za kuchakata koka.
Zoezi letu lilianza kwa kutoa yale mapipa yote na kuyapeleka eneo la nje kwa ajili ya kuyafanyia usafi. Wakati huu Catarina na mwenzie wao walikua ndani ya lab wakiendelea na shughuli nyingine.
Nikiwa nje na javier Catarina aliniita kisha akasema yupo kwenye stage muhimu sana ya maandalizi hivyo napaswa kuwa hapo ili nijifunze. Kwa maana hiyo hakutaka niendelee kukaa na Javier kule nje bali niingie ndani ili kujifunza cha kufanya wakati wa maandalizi.
Niliingia ndani na kukaa karibu na meza ile kubwa tayari kwa kutuzama mkemia Catarina akifanya mambo. Tukiwa hapo aliomba atoke anaenda kuchukua baking soda, hii ilikua very important kwenye hizi stages za mwanzo wakati unaandaa coca paste ili baadae kupata cocaine hydrochloride.
Baada ya Catarina kuondoka, Manuela alisogea nilipo na kuanza kuniongelesha. Hapa nilikumbuka kauli ya javier, kwamba kama nahitaji kuwepo pale maabara na kuendelea kufanya kazi kwa Amani basi nijiwekee mipaka kwa binti huyo.
Nilikumbuka maneno ya Javier kuhusu kifo cha Gatkuoth ambacho anadai Catarina alihusika kwa kutumia strychnine.
Wakati huu nilitamani ata kumfukuza Manuela asinisogelee kabisa, kwanza hakua na mvuto ata kidogo kimoyomoyo nilijiambia ata akinivulia nguo siwezi fanya chochote.
MANUELA: How was your first night at camp?
Did you enjoy sleep?
( Usiku wako wa kwanza kambini ulikuaje? Vipi ulifurahia usingizi)
MIMI: I couldn't
( Hapana sikufurahia kabisa)
MANUELA: what was the problem? Did javier left
You alone
(Tatizo lilikua nini? Au Javier alikuacha peke ako)
MIMI: no!!! it was cold and cold, Sorry can I find a way to escape here?
( Hapana baridi lilikua kali sana, Samahani hivi naweza pata njia ya kutoroka hapa)
MANUELA: why so early
(Mbona mapema sana)
MANUELA: Don't worry I'll help you, we'll talk later
( Usijali nitakusaidia nitafute baadae)
Kwa mbali nilimuona catarina akija na container ndogo ya chemicals, Ndani ya container ile kulikua na alkaline material (baking soda) wakati huu Manuela alibadirisha maongezi ghafla.
Manuela aliniagiza nikachukua benzol na maji nivilete maeneo ya karibu kwani vyote hivi vilihusika kwenye mchanganyo wa kwanza.
Hapo Manuela alinifurahisha kwani aliigiza as if hatukuongea chochote na tulikua bize na kazi. Lakini wakati naongea na Manuela niligundua kitu cha tofauti kabisa.
Manuela alikua serious sana na hakuonyesha dalili ya uteja kabisa alinihoji kama mtu mwenye akili timamu huku macho yake yakiniangalia kwa namna kama anatafuta kitu kwenye akili yangu.
Nilijiambia lazima nimtafute baadae, anaweza kunisaidia kujua namna gani naweza kuondoka ndani ya eneo hili sitakiwi kumzalau kabisa.
Lakini kingine watu hawa walizidi kunichanganya sana, mpaka wakati huo nilishindwa kumuelewa Javier na sasa hivi nashindwa kumuelewa manuela.
Kwenye hatua ya kwanza ya kutengeneza paste hua tunachanganya majani hayo yaliyopondwa pamoja na alkaline material ambayo Catarina alikuja na baking soda.
Lakini ukikosa baking soda unaweza kutumia sodium bicarbonate kwenye mchanganyo huo wa kwanza.
Baada ya hapo unachanganya na maji pia, wakati huu yale mapipa yaliyokatwa kwenye mfuniko ndio yalikua yanafanya kazi sasa.
Hatua hii ya kwanza hua haifanywi kwa haraka kwani zipo maabara zinazotumia mpaka siku tatu na wengine masaa kadhaa kuandaa paste. Hapa inategemea technology ya maabara husika lakini pia kiwango cha majani kilichopo.
Zoezi lilikua gumu kwani niliona kabisa idadi yetu kama ilikua haitoshi kulingana na energy tunayotumia pale. Maana kwenye kazi za nguvu sana sana ni mimi na javier ndio tulikua nguvu na kidogo Catarina lakini Manuela hakuweza kazi ngumu kabisa.
Baadae Catarina alikuja na mafuta ya taa, watu wa chemistry tunajua kama mafuta ya taa ni organic solvents. Sasa hapa zile alkaline material zinafanya cocaine alkaloids zilizopo kwenye majani ya koka kuwa extracted kwenye mafuta ya taa.
Daaaaah!!!! Tutasameheana najitahidi sana pia najaribu kutumia lugha rahisi Lakini bado naona wanangu wa HKL nawavuruga. Na sio wa HKL ata wale waliosoma chemistry kwa kukalili Nadhani mnatoka patupu.
Twendeni mdogo mdogo, ni hivi apa tunadili na alkaline material ( kiswahili chake sijui) pia tunadili na organic solvents ( pia kiswahili chake sijui) mwisho tunaweka na maji. Dhumuni la kufanya hivi ni ku extract ile cocaine ambayo ipo kwenye majani.
Kama tunakumbuka nilisema kiwango cha alkaloids cocaine kwenye majani ndio huthibitisha ubora wa majani hayo.
Sasa hii alkaloids cocaine hupatikan kwenye mimea inayoitwa erythroxylon plants, hii mimea ipo mingi lakini species kuu mbili ndio hutoa cocaine alkaloids nyingi nayo ni:-
I)erythroxylon coca na
II)erythroxylon novogranatense --
Hizi zote hupatikan sana maeneo ya chini kuzunguka safu za Andes principally in Peru, Bolivia, and Colombia.
Ukitaka kujua changamoto ya lugha ya kiswahili jaribu kuelezea matukio ya kisayansi ambayo hayana tafiri ya kiswahili.
Ndio maana wengi husema kiswahili ni lugha changa sana inahitaji kukua zaidi kuendana na technology. Mfano maneno mengi ya kitechnolojia hayapo kwa kiswahili. Mara nyingi BAKITA wanajitahidi kubumba bumba tu, utaskia oooh!!! Kimemeshi, mara tarakirishi mara tarairishi mpakato. Ebu tuyaache hayo.
Naomba nijaribu kwa kiswanglish tuone kama Hatua mambo yataenda
Hatua inayofata baada ya ile pale juu,
Cocaine alkaloids are extracted from the kerosene (mafuta ya taa) into a dilute acid solution.
Alkaline material (sodium carbonate) is added to the remaining solution which causes a precipitate to form. An acid and the water are drained off and the precipitate is filtered and dried to produce coca paste, off-white to light brown,
Hii coca paste ipo kama puti kwa wale walipita pita kwenye ufundi tutaelewana apa
Baada ya hapo tunakua tumemalizana na coca paste kinachofata hatua nyingine ni ku convert coca paste kwenda kwenye cocaine base.
Hapa tuliona tupate break kidogo hivyo tulienda zetu nje kwa ajili ya misosi. Catarina na Manuela waliongoza kwenye nyumba yao huku mimi na Javier tulibaki nje tunapunga hewa safi ya mto haullaga.
Wakati tunatoka Manuela alinisogelea na kutamka maneno mawili tu " keep promise".
Hapo nilijiuliza mimi ndio mwenye shida na nimemuomba anisaidie namna ya kutoroka kwenye maeneo haya. Lakini yeye ambae anahitajika kutoa msaada ndie anasisitiza nitimize ahadi ni wazi na yeye anajambo lake.
Na jambo lake si lingine litakua lile lile aliloniambia javier napaswa kua makini yote hayo yalikua ni mawazo yangu wakati huo.
Tukiwa nje tunasubiri, nilimuuliza javier kuhusu kisa cha JUAN CARLOS RAMIREZ ABADIA kwani hakua amenisimulia nilitaka afanye hivyo ili at least tusogeze muda.
Ila javier alionekana kuwa na njaa sana so mpaka muda huo hakuwa tayari kunieleza chochote mpaka atakapo shiba. Aliniambia kama ana njaa hawezi fanya lolote wala hatoweza kunisimulia vizuri na nikamuelewa.
Hapo nilikumbukua maneno ya Catarina kwamba Javier yupo punctual sana wakati wa misosi kuliko chochote kile.
Javier aliomba tusimame twende kulekule kwenye nyumba anayoishi Catarina na Manuela kwani wanakawaida ya kuchelewa sana wakiingia ndani humo. Hivyo wa kuwasubiri pale wanaweza kutuweka mda mrefu na njaa.
Kwa utani javier alisema wale wadada wakiingiaga ndani lazima wapige ata kimoja kwanza ndio wanaandaa msosi.
Wakati tunatembea Javier alihoji kwanini natamani sana kujua kuhusu Juan Carlos.
Nilimjibu kuwa binafsi napenda wapambanaji na ma hustlers wanaotafuta hela au utajiri kwa namna yoyote.
Javier aliuliza je nahitaji kuwa tajiri??
Bila shaka nilijibu ata kilicho nipeleka huko ni hizohizo harakati za kutafuta utajiri.
Javier alicheka sana na kisha akaniambia mbona utajiri umeuacha East Africa, nilimuuliza kivipi akasema atanipa story ya babu yake ambae aliniambia kuwa babu huyo aliishi mkoa wa Lindi.
Nilimsisitiza Javier kuwa namdai mambo mawili, jambo la kwanza ni kuhusu mzee wake ambae anadai aliishi bongo kabla ya uhuru na jambo lingine kuhusu Juan Carlos.
Kwa hakika javier alikua na mambo mengi anayoyajua hivyo kukaa naye nikinufaika na mengi.
Kuhusu juan Carlos na cartel yake ya kuuza madawa
Javier alinieleza kwa ufupi sana kuhusu jamaa huyo ambae ndie alipelekea Catarina kufika hapo.
Kilichonifurahisha kwenye story ya Juan Carlos ni namna alivyofanya plastic surgery na kubadili muonekano wake.
JUAN CARLOS RAMIREZ ABADIA
Picha ya Kabla na baada ya plastic surgery alivyofanya juan ili kubadili muonekano wake.