mkoba mweupe
Member
- Feb 25, 2017
- 89
- 144
Next please[emoji39][emoji39][emoji39]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Verry well to tell him. Wazee wa raphta tumekuja .tuone ni nini jamaa atasema kuhusu raphta tuangalie na chami amesema nini tujue wadau tunasoma. .ila kwa vile muandish ameanzia mbali na sisi tunavuta subira kuiendea raphta.navutiwa na stor za jamaa na ving anavosema mfano majina ya sehem kweli yapo.Too selfish, lack of appreciation, too biased, negative minded. Shame on you idiot!!
Umetisha Sana mzee, uandishi ulotukuka hakika. Kila la kheirTuliimaliza siku nzima tukiwa ndani ya maabara ile huku Catarina ambaye anaonekana kua ndio supervisor wa maabara hiyo alisisitiza kua nitakua bora kumzidi Javier. Alidai Javier ni mvivu sana, yupo makini kwenye misosi kuliko chochote.
Javier alikua akitabasamu kwa muda wote ambao Catarina akimsema, kwa maelezo ya Catarina ni kwamba Javier alikua mvivu sana linapokuja swala la kazi lakini alikua punctual sana wakati wa misosi.
Catarina alitumia muda huo kunionyesha sample za products zinazotolewa kwenye maabara hiyo. Kwenye ile meza kubwa kulikua na chombo ambacho ndani yake kulikua na sample kadhaa zimehifadhiwa.
Kwa maelezo ya Catarina, ni kwamba kwenye maabara hiyo wanatoa cocaine katika namna mbili tofauti tofauti ambazo ni:- cocaine hydrochloride na crack,
Cocaine hydrochloride ambayo ipo katika namnaa Fulani kama unga mweupe na matumizi yake yapo ya aina nyingi lakini njia pendwa ni kupitia injection (sindano) na snorting.
Crack hii ni namna nyingine ya mzigo unaozalishwa ndani ya maabara hii. Kwa muonekano inafanana na mapande ya chumvi ya mawe inapokua maabara, kawaida Ndani yake kuna mchanganyiko wa hydrochloride, ammonia au baking soda na maji.
Namna ya matumizi mara nyingi huvutwa kama kawaida. Huvutwa kwa kuchanganya na either bangi au sigara, mara nyingi huuzwa ikiwa kwenye solid state kisha mtumiaji anaenda kuisaga yeye mwenyewe kwa matumizi.
Sasa kulingana na wataalamu wa pharmacology cocaine hydrochloride na crack zote ni kitu kimoja ila kulingana na maabara hii kuna namna zimetenganishwa kama sample tofauti tofauti.
Kwenye zile sample zilipangwa kwa namna ya viwango vya quality lakini pia bei ya product inayozalishwa kwenye maabara hiyo.
Apa kwenye quality na bei hua tunaangalia ingredients (viungo) na level of purity (kiwango cha usafi) mzigo ukiwa na makapi mengi hupungua thamani pia.
Sasa kinacholeta makapi ni zile ingredients mfano nitroglycerin (gun powder) ambayo huwekwa kwa wingi kwenye Brown cocaine au Brown sugar kama wanavyoita watoto wa mjini, kiwango cha madhara kwa mtumiaji hutegemea na hizi ingredients pia.
Product ya kwanza iliitwa FISH SCALE COCAINE, hii ni pure cocaine ambayo purity level (viwango vya usafi) ni zaidi ya 90% yaani hakuna impurities kabisa kwenye mzigo huu na hii ndio cocaine ghali zaidi kwenye maabara hii. It is more powerful more expensive and harder to obtain hii yenyewe inang'aa sana kwa muonekano.
Product ya pili ilikua ni BROWN COCAINE ambayo ilikua ni mchanganyiko wa cocaine, amphetamine na nitroglycerin (gunpowder). Huu ni mchanganyo hatari zaidi kwani unaweza kupelekea mtumia kupatwa na madhara kama heart attack au stroke. Ile rangi wa Brown husababishwa na kuwepo kwa gunpowder kwenye mchanganyo huo.
Product ya tatu kuzalishwa kwenye maabara ile kulingana na maelezo ya Catarina ilikua ni CRACK COCAINES, hii kama nilivyoielezea hapo awali kama inafanana na crystals sometimes kama chumvi ya mawe.
Hii ndio low purity form of cocaine ( ina makapi mengi) viwango vya usafi ni sifuri kabisa kwani ndani yake kuna baking soda, maji na uchafu mwingine mwingi. Kawaida inakua na muonekano wa njano au brown inasemekana kua more addictive ukilinganisha na nyingine.
Catarina alinifundisha mambo mengi sikuile mwisho wa siku kichwa kilichoka sana kwani baada ya kugundua uwezo wangu alitaka tumalize ile orientation ndani ya siku moja.
Wakati naendelea na Catarina, Javier na Manuela walikua bize kusafisha baadhi ya apparatus kwani ilionekana siku inayofata kutakua na kazi kubwa. Nilichogundua kufanya kazi ndani ya ile maabara nilitakiwa nishukuru sana kwani hakukua na majukumu mazito ukilinganisha na wale wa mashambani.
Ila kuwepo maabara tatizo ni moja tu, kuwa teja ni kugusa hivyo nilidhamiria kuongea vizuri na Javier ili anielekeze ni kwa namna gani amefanikiwa katika hilo.
Tulitoka nje na Catarina kwa dhumuni la kunionyesha mazingira mengine ya nje ya jengo hilo la maabara. Nje hakukua na vitu vingi saaana zaidi ya sewage systems ambayo zilijengwa kwa mtindo wa kisasa zikitiririsha maji kwenye bonde hilo kuelekea mto haullaga.
Upande wa pili kuvuka sewage systems kulikua na jengo lingie refu lakini halikufikia lile la maabara kwa ukubwa. Jengo lile lilitumiwa kwa ajili ya packing ya mzigo uliokua tayari kusafirishwa, ni jengo ambalo lilikua na mfumo madhubuti wa umeme na hii ilimaanisha watu wa packing wakija hufanya kazi 24 hours.
Mazingira ya nje yalikua mazuri mno na nilivutiwa na kijani kibichi iliyotawalaa maeneo ya kuzunguka bonde lile. Kulikua na hewa safi na ya asili hakikaka taratibu nilijikuta nasahau dhiki za ile safari ya kufika hapo.
Nilimueleza Catarina hisia zangu juu ya uoto ule wa asili na hali ya hewa ya eneo lile. Catarina alitabasamu kwa muda kisha akaniambia kuwa miaka 10 nyuma eneo hilo lilikua bora kuliko hivi sasa.
Kwa maelezo ya Catarina ni kwamba maeneo ya kuzunguka bonde hilo kumekua na shughuli nyingi zinazopelekea (deforestation) ukataji wa miti. Hivyo hali ya hewa inabadilika taratibu sana tofauti na ilivyokua miaka ya nyuma. Aliendelea kusema kwamba wao ni miongoni mwa watu wanaopambana sana kuhakikisha mazingira ya eneo hilo yanatunzwa kwani wakulima wadogo wadogo ndio hufanya shughuli zao kienyeji bila kujali mazingira.
Kwa kuendelea kuchafua mazingira na kukata miti hovyo kungepelekea serikali ya Peru ku draw attention kwenye ukanda huo hivyo shughuli zao zingekua ngumu kuendelea.
Ilionekana wazi kuna viongozi wakubwa wa Peru na Bolivia wanajua au wanahusika na mashamba hayo ambayo yapo huko haullaga.
Nilimuuliza Catarina kuhusu soko la products zinazotolewa pale, bila kuchelewa alijibu kuwa wao hawahusiki kabisa na mambo ya soko kwani tayari kuna watu wa marketing ambao ndio wanajua kilakitu kuhusu soko.
Kikubwa anachojua yeye soko lao ni America ya kaskazini na ulaya na Asia wa uchache. Lakini pia alinionya kuendelea kuuliza maswali hovyo kama nitafanya hivyo kumuuliza kila mtu au kutaka kujua kila kitu kwa haraka naweza kuingia kwenye matatizo.
Bila shaka nilimuelewa Catarina anamaanisha nini, wakati wote huo nikiwa na Catarina alikua bize na sigara kwa kweli alikua mvutaji mkubwa. Nilihisi bado nahitaji kujua mengi kuhusu Catarina na Manuela nilikua kila nikimuangalia Catarina kuna kitu kinaniambia nahitaji kuendelea kuwa karibu zaid.
Sikuona haja ya kuendelea na maswali mengi zaidi kwani ata yeye alishanionya juu ya kuuliza maswali, ata hivyo kuuliza uliza maswali mengi haikua desturi yangu ila kuna muda nilitakiwa kufanya hivyo kutokana na ugeni wa mazingira hayo.
Baada ya muda alikuja bwana Javier akiwa na Manuela ambao wote kwa pamoja tuliungana kwenye meza moja iliyokua nje ya mazingira hayo na kuendelea na soga.
Wakati tunaendelea na stories, nilijiuliza ukiwa hapo mishahara tunalipwaje? Na matumizi tunafanyaje? Lakini baada ya kukumbuka onyo ya Catarina sikuona haja ya kuuliza hivyo nilitunza maswali yangu yote.
Niliamini Javier ndie mnyonge wangu ambae atajibu maswali yangu yote hapo baadae.
Nilijikuta nimekua na amani sana baada ya kuungana na kampani hiyo mpya kwenye maisha yangu. Javier alikua ana m-care sana Manuela ambaye mara zote nilipomuangalia usoni sura yake ilionekana wazi kama imebeba mengi mno.
Manuela alikua dhaifu mno kutokana na hali yake ya uteja, hauweza kufanya kazi yoyote ile iliyotumia nguvu hivyo Javier alipenda kuwa nae karibu na wanashirikiana mambo mengi.
Kwa haraka niligundua Catarina alikua na control kubwa kwenye maisha ya Manuela kwani yeye ndio aliamua ni muda gani wa Manuela wa sniff (kunusa cocaine) na ni kiasi gani ampe.
Kitendo cha Manuela kuwepo maabara pale ndio kilimpa favor ya kutumia high purity and expensive cocaine. Lakini kama angetumia aina nyingine ambazo zinakua contaminated kwa kiasi kikubwa asinge kua pale mpaka muda huo kwani alitumia kwa kiasi kikubwa sana.
Tukiwa pale tunaendelea na mazungumzo, niligundua kitu tofauti kutoka kwa Manuela kwani alikua kimya sana.
Alianza kutapika mfululizo huku akiwa anatokwa jasho jingi mno kiasi kwamba t-shirt yake yote ililowa. Aliporudi tulipokua tumeketi alionekana kutetemeka especially Upande wa mikono yote ilikua inatetemeka.
Catarina alinyanyuka na kuelekea Upande wa pili wa maabara hiyo na kuingia kwenye kamsitu kadogo jirani na maabara ile.
Javier alisema kinachomtokea Manuela ni arosto hivyo Catarina alikua anaenda kwenye ghetto lao kwa ajili ya kuchukulia unga ili arudi kwenye equilibrium. Catarina ndio alikua anajua dozi ya rafiki ake huyo na alifanya hivyo kwani angempa uhuru wa kutumia anavyotaka ingekua hatari.
Ingekua hatari sana kwakua upatikanaji wa dawa hizo kwa eneo hilo ulikua mrahisi sana hivyo ingeweza kumpelekea overdose na mpaka kufa.
Mabinti hawa wawili walikua wanaishi nyumba moja ambayo ilikua karibu kabisa na maabara hiyo pembezoni mwa mto. Nyumba ile ilijengwa kwa mbao lakini hii ya kwao ilikua tofauti na zile za kule kwetu tunapokaa mimi na bwana Javier.
Hii ilikua na viwango vya juu at least ukilinganisha na zote kwenye eneo hilo. Sababu kubwa ya umalidadi wa jengo hilo lililokua linakaliwa na Catarina na mwenzie emanuela, lilikua pia linatumiwa kama stores ya products zote zinazotokea maabara kwa ajili ya kusafirishwa.
Baada ya muda Catarina alirudi akiwa ameshika kitu mkononi na kumpatia Manuela, Manuela alipokea kwa pupa sana na kisha akatokomea upande mwingine kutoka pale tulipokua tumekaa.
Upande alioelekea ni ule upande uliokua na jengo la pili linalotumiwa na baadhi ya watu ambao huletwa apo kwa ajili ya packaging.
Watu wa packing wanakua wapo special na hufika apo baada ya kua maabara imekamilisha tayari mzigo. Na wao huandaa mzigo huo kwa ajili ya kusafirishwa, mara nyingi mzigo huo hupimwa kabla ya packaging na muhusika mkuu apa anakuaga Miguel pamoja na Daniel wao ndio huratibu mchakato huu.
Sababu ya kupimwa mzigo kabla ya packing ni kutafuta uhalisia wa kiwango kilichozalishwa kutoka maabara na mzigo uliosafirishwa kuwafikia watu wa marketing.
Kwa wastani ni kuwa kg 400 za majani ya koka (coca leaves) zinatumika kuzalisha kilo moja (1) ya coca paste na wakati huo huo inaweza kuzalisha kg 0.5 cocaine hydrochloride.
Mara nyingi wanaotumika kupack mzigo baada ya kua umepimwa wanakua ni wadada special ambao wapo kwa ajili ya kazi hiyo. Wadada hao hutokea jiji moja linaitwa Lima na wengine hutokea Arequipa.
Kwa stories za javier ni kwamba hao wadada wanakuaga ni warembo sana kwakua nipo hapo nitawaona siku mzigo ukiwa tayari.
Hivyo basi mara nyingi kama watu hao wa packing hawapo ndipo Manuela hupenda kulitumia eneo hilo tulivu kwa ajili ya shughuli zake za sniffing.
Bwana Javier ni moja ya watu waliofurahia uwezo wangu kwani ilionekana ninaenda kubeba majukumu mengi na kumpunguzia sehemu kubwa ya majukumu yake.
0623329512 Whatsapp
NB: Wanaoisomea kwa whatapp wapo mbele zaidi
(2000 wanalipia kwa simulizi yote)
Simulizi inaendelea bado mkuuUlitokaje huko Mugabohela hadi kutupa hii story!