KABLA HATUJAENDELEA NA SIMULIZI HEBU TUANGALIE KWA UCHACHE ASILI YA MGOGORO WA IRAN NA GERMAN WAKATI WA VITA YA PILI YA DUNIA (WWII)
KWA HISTORIA FUPI NI KWAMBA
Mnamo mwaka 1935 serikali ya uajemi ya kale maarufu kama (Persian government) iliamua kubadilisha rasmi jina la nchi hiyo. Jina lilibadilika kutoka kwenye kuitwa Persia mpaka kuitwa Iran, mabadiliko haya yalikua yametokea kipindi cha utawala wa Reza shah.
Neno shah Kwa nchi ya Iran linatumika kama title ya kiongozi mkubwa na wa juu kama vile king au emperor. Walipita wengi kwenye cheo hiki lakini kwenye record wa mwisho alikua ni Mohammad Reza Pahlavi.
History ya Iran inamambo mengi sana hususani linapokuja swala la uongozi wake kuanzia kwenye utawala wa Qajar dynasty ambayo ilitawala miaka ya 1795 mpaka 1925.
Nadhani hapa si mahala pake sisi twende moja kwa moja kwenye lengo letu kuu ambalo ni mgogoro wa kivita kati yake na ujerumani.
Sasa ni hivi Mgogoro ambao tunaenda kuulezea ulianzia kipindi cha vita ya pili ya dunia (WWII) yaani 1930's. Hapa kulikua na kambi mbili (antagonistic camps) zilizokua zinapingana kiitikadi na kisiasa, kambi hizo zilikua ni allied powers na Axis power.
Axis power ilikua na German, Italy na Japan wakati huo allied au democratic power ilikua na united states of America maarufu kama US, Britain na Soviet Union.
Kwa kipindi cha miaka ya 1935 nchi ya Iran ilijitangaza kuwa neutral ( hakufungamana na kambi yoyote kati ya allied na Axis power) kipindi hiki nchi ya Iran ilikua chini ya Reza shah.
Sababu ya kuwa neutral ni kwamba Reza shah aliwahofia umoja wa kisoviet na waingereza lakini pia alitaka kulinda faida za kiuchumi alizokua anazipata kutokana na mahusiano yake mazuri na nchi ya ujerumani.
Chanzo cha mgogoro kilizaliwa miongoni mwa nchi hizi tatu yaan ujerumani, uingereza na umoja wa kisoviet (kwa sasa urusi) kwani nchi hizi zilikua zinatoka kambi tofauti na zilipishana kiitikadi na hata kisiasa.
Nchi ya ujerumani ilikua tofauti na ile ya uingereza na umoja wa kisoviet (kwa sasa urusi), Kwan ujerumani haikuwahi kuwa na historia au background yoyote ya kuingilia mambo ya Ndani ya Iran wala kuvamia mipaka ya Iran.
Kwa background hiyo, Reza shah alijifunza mambo mengi kutoka ujerumani kama vile siasa za ujerumani na political management na wakati mwingine alijifunza ata technology za viwanda kutoka ujerumani.
Mbali na hayo yote Reza shah alidhamiria kupunguza mahusiano ya kibiashara na umoja wa kisoviet ambao mara nyingi walionekana kua na migogoro. Ambapo mpaka kufikia mwaka 1940- 41 karibia nusu ya (bidhaa za Iran) Iranian imported goods zilitokea ujerumani.
Pamoja na records hizo kwa kwa upande wa import lakini karibia 42% ( asilimia 42 ) ya kila bidhaa aliyouza Iran kwenda nje ya nchi zilienda ujerumani.
Mnamo majira ya kiangazi mwak 1941 nchi ya ujerumani ikiwa na jeshi la Nazi ilipata ushindi wa kishindo dhidi ya umoja wa kisoviet (Russia)kwenye vita vilivyopiganwa majira hayo.
Ushindi huu ulipelekea majeshi ya uingereza na umoja wa kisoviet pamoja na majeshi ya marekani (USA) kutaka kutoa msaada wa kijeshi kwa soviet kupitia Iran.
Walivamia Upande wa kusini na wengine kaskazini mwa Iran ikiwa ni njia ya kupambana na ujerumani.
Mahusiano mazuri ya kidiplimasia kati ya Iran na jeshi la Nazi ndio yalipelekea Reza shah kuendelea kukaidi maagizo ya allied power juu ya kufukuzw raia wote wa kijeruman waishio Iran.
Mwezi wa tisa tarehe 11 mwaka 1941 serikali ya uingereza ilimtuma mjumbe bwana mmoja alifahamika kama Sir Reader S. Bullard ambae alikutana na waziri mkuu wa Iran kwa wakati huo Mohammad-Ali Furuqi.
Agenda kuu ya kukutana kwao ilikua kushinikiza kuondelewa madarakani kwa aliekua emperor au shah kwa kipindi hicho ambae ni Reza shah huku wakidhamiria kumuweka mtoto wake aliejulikana kama Muhammad Reza Pahlavi.
Hii ilikua ni kwa sababu tu Reza shah alionekana kuwa Upande wa Nazi kwa sababu kuna namna serikali yake ilinufaika na mahusiano yake na ujerumani.
Baada ya majadiliano kati ya Sir Reader S Bullard na Mohammed-Ali Furuqi zilipita siku tano tu yaani mnamo September 16 Reza shah aling'olewa madarakani akimuachia mtoto wake ambae kwa sehemu kubwa alilinda maslahi ya Allied power.
Reza shah alifariki akiwa mahameni (exile) huko Johannesburg Africa ya kusini mwezi wa saba (7) tarehe 26 mwaka 1944.
Mwezi wa kwanza mwaka 1942, Iran bila kusahau umoja wa kisoviet na uingereza walisaini mkataba ulioitwa tripartite treaty of alliance. Mkataba huu ulisainiwa baada tu ya nchi hizi zilizokua zinaunda allied power kuivamia Iran.
Kwenye mkataba huu makubaliano yalikua ya aina tatu kati ya Iran na nchi hizi zilizokua zinaunda kambi ya allied power.
Kwanza kabisa; waliitambua Iran kama taifa huru lakini pia waliitambua mipaka yake bila kuiingilia kwa namna yoyote ile.
Pili; walikubaliana kuilinda Iran kiuchumi hususani kwa matatizo yote ya kiuchumi ambayo yatasababishwa na vita.
Mwisho kabisa walikubaliana kuondoa majeshi yao kwenye maeneo yote yanayozunguka mipaka ya Iran ndani ya miezi 6 baada ya kumalizika kwa vita.
Lakini hili lilikua tofauti kidogo kwa upande wa umoja wa kisoviet kwani wao hawakua tayar kuondoa majeshi yao mpaka pale shinikizo lilipo tolewa na umoja wa mataifa.
Baada ya makubaliano hayo apo juu lakini pia baada ya kutolewa madarakani kwa aliyekua emperor wa mwanzo kabisa Reza shah. Iran haikua na cha kupoteza tena kwenye mahusiano yake na ujerumani hivyo mnamo mwaka 1942 (kipindi masika).
Iran ilikata Rasmi mahusiano yake na ujerumani au na Axis power ambayo ilikua inaundwa na ujerumani, Japan na Italy. Na ni ndani ya mwaka huohuo 1942 ndipo wale wananchi na raia wote wenye asili ya ujerumani walitimuliwa Iran.
Baada ya tukio hilo la kutimuliwa kwa raia hao wenye asili ya ujerumani kutoka nchi ya Iran.
September 9 mwaka 1943 Iran ilitangaza vita rasmi dhidi ya ujerumani na hapa ile hali ya kuwa neutral ilifutwa rasmi. Lakini wajuzi wa mambo wanadai Iran ingeendeelea kuwa neutral pasipo shinikizo la umoja wa kisoviet na waingereza.
Vita hii ya Iran na jeshi la Nazi ilitangazwa baada ya viongozi wa mataifa makubwa matatu yanayounda Allied power kukutana mjini Tehran uko Iran.
Viongozi waliokutana walikua ni raisi wa USA kwa kipindi hicho Franklin Roosevelt na waziri mkuu wa uingereza Winston Churchill na mwingine alikua ni general secretary wa chama cha kikomunisti Josef Stalin.
Majadiliano ya mkutano huu yalikua ni yaleyale mikakati ya kivita dhidi ya Germany na Japan.
Anglo-soviet invasion of Iran.
(Picha kwenye PDF)
Kwenye picha hapo juu ni Jeshi la allied power lililojumuisha uingereza na umoja wa kisoviet pamoja na marekani.
Sasa kwa taswira hii fupi kila mmoja anaweza kua ameona ni kwa namna gani Iran na ujerumani zilianza kuwa na mahusiano mazuri ya kidiplomasiana baadae kuhusishwa na vita.
Korporal Schulz alikua ni moja ya ma agent wa ujerumani waliokua wakiishi Iran kabla ya machafuko hayo.
TURUDI KWENYE SIMULIZI YETU
Javier akiwa na sharmahd walikutana na Schulz kwa mara ya kwanza ndani ya jiji la Düsseldorf kwenye moja ya casino maarufu ndani ya mji huo.
Schulz alikua ni mfano wa wale wazee ambao hawakuwa tayari kukubali ukweli kama wamezeeka Hivyo alitumia muda wake mwingi kwenye kumbi za starehe.
Kutokana na shughuli walizokua wanafanya Javier na mwenzie mara nyingi walijikuta wanaingia kwenye contact na kikongwe huyo bwana Schulz.
Bwana Schulz alizidi kuweka ukaribu na mabwana hao mara tu alipogundua jamaa hao wana asili ya Asia hususani maeneo ya Persian gulf.
Baada ya siku chache za kufahamiana vizuri kikongwe Schulz aliwaambia jamaa wale kama kwenye ujana wake waliwahi kuishi Tehran. Alikaa huko takribani miaka 8 kabla ya nchi ya Iran kuwatimua rasmi raia wa ujerumani mnamo mwaka 1942.
Story hizi mara nyingi walipigia kwenye moja ya casino maarufu iliyojulikana kwa jina la Kurhaus Baden ( sina uhakika sana na hili jina).
Wakiwa Ndani ya casino hii bwana Schulz aliwaambia Javier na mwenzie kwamba miaka hiyo yote akiwa Iran alipata rafiki wa karibu sana aliyejulikana kwa jina la Shahzad.
Shahzad alitokea familia moja ya baharia mmoja maarufu sana ukanda huo wa Persian gulf, babu zake na Shahzad walishiriki au alipata umaarufu baada ya kushiriki vita ya roman-persian wars maarufu sana ukanda huo.
Ukoo wa kina shahzad ndio mara nyingi waliongoza meli za kivita za kiajemi dhidi ya warumi. Meli maarufu iliyoongozwa na shahzad iliitwa
TRIREMES AND BIREMES ( meli ya kivita ya kigiriki)
TRIREMES AND BIREMES