Utajiri wa Magofu ya Rapta

Kweli kabisa wangemtumia awe mtu wao bongo wanamfungulia biashara kubwa kumbe jasusi
Nashangaa asee meku anakuja kuchukua buku tatu wakati alikuwa na dhahabu mfukoni (Fatemeh) Meku umeniangusha. Mm nisingerudi bongo bila kuwa jasusi
 
TUNAENDELEA WAKUU

Nikiwa bado natafakari mambo mengi ndani ya blanket nilikosa usingizi kabisa, mwisho wa siku nikajitoa kwenye blanket na kukaa kitandani huku nikiwaza usiku huo naumaliza vipi kwani ulikua ni mrefu sana.

Niliwaza au nitafute demu ili nisogeze masaa lakini pia nipunguze stress za hawa CIA na wa Israel, mbali na hapo nipunguze na hasira za kumkosa fatemeh.


Lakini pia niliwaza ni uzembe uliokubuhu kulala peke yangu kwenye room kubwa na nzito kama ile japo sijui bei yake mi niliwekwa tu umo. Kimoyomoyo Nikasema ngoja nitafute Peruvian bitch ( mdada wa kiperu) wa kusogeza nae masaa.

Ni wanaume wachache sana duniani wanaoweza kulala lodge au hotel nzuri bila demu, hili swala ni gumu sana yaani ulale sehemu umelipia laki mbili au at ef hamsin alaf ulale mwenyewe. Si bora ukalale stendi au zile gest za buku buku ukitaka kuchaji simu unaenda kwa father gest (jokes)

Sasa napataje demu wakati sina ata buku mfukoni na kwa bahati mbaya sijawahi ata kuiona kwa macho pesa ya peru mpaka wakati huo.

Unaweza kushangaa kwanini mpaka muda huo sikuwa nimebahatika ata kuiona kwa macho yangu pesa ya peru lakini huo ndio ukweli.

Kwenye mizunguko yangu yote hakuna sehemu nimepewa hela au nimekutana na mazingira ya kudaiwa au kulipwa pesa. Hivyo ilikua ni halali kabisa kwa mimi kutokuijua pesa ya Peru mpaka wakati huo.

Mtu wa kwanza kunijia kichwani kwangu alikua ni Damião, Damião alikua ni bata boy au mtoto wa mjini pale Lima. Lazima angejua ni wapi ningepata demu usiku huo wa kunisaidia kusogeza masaa.

Changamoto ilipokuja sikua na namba ya simu ya Damião hivyo ilikua ngumu kumpata kwa wakati ule bila ya kuwa na simu.



Lakini ata hivyo nilitakiwa kutafuta namna ya kumuingia Damião kwani alijua Mimi na fatemeh tulikua wapenzi sasa ningemuacha na mshangao kwa kumwambia natafuta demu usiku huo hivyo basi isingekua rahisi kwa Damião.


Mtu wa pili kumfikiria alikua ni bwana Malugu m'bongo mwenzangu huyo nae ndio ilikua rahisi kwani nilikua na namba yake lakini pia hakumjua fatemeh na ata angemjua hakujua kama nina nilizushiwa mahusiano nae.

Nilitoka kitandani kwa haraka na mbwembwe nyingi kusogelea eneo au meza iliyokua na simu kisha kupiga namba zile ambazo code yake ilianza +51.

Kulikua na maelekezo kwenye ile simu ya hotel, kuna namna ya kupiga simu ndani ya hotel yaan kama unashida na mtu wa room ya jilani apa ulitakiwa uijue namba ya room yake. Pia namna ya kupiga simu za nje ya hotel na mwisho kabisa unabonyeza 0 kwa msaada kutoka reception.

Nilifuata maelekezo ya kupiga simu za nje ya hotel ambayo kama sikosei ilikua nabonyeza namba 9 kwanza, kisha nafuata maelekezo mengine na kuendelea na mchakato.

MIMI: ebwana kaka malugu mambo vipi?

( Malugu aliposikia kiswahili moja kwa moja alijua ni mimi)

MALUGU: poa dogo!!!. naona jamaa alikutoa kwa haraka sana.

MIMI: kuna mtu tulikua tuna muwahi alitusubiri muda mrefu. Sasa bro naweza kupata manzi usiku huu.
(apo natafuta connection sasa)

( Kama kawaida yetu wabongo namuuliza swali na yeye analeta swali baada ya kujibu swali)

MALUGU: kwani we uko wapi?

Ghafla!!! Simu ilikata na network ikapotea kabisa, nilijaribu kupiga tena simu hazikutoka lakini ndani ya sekunde kadhaa mlango ulifunguliwa na fatemeh akiwa ni mwenye hasira nyingi.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
We mbishi sana, ulishaambiwa usiongee na mtu yeyote yuke
 
TUENDELEE SASA!!!
 
Fatemeh aliingia kwenye room yangu kwa speed kubwa sana lakini wakati huo huo akiwa serious kupita maelezo.

Mpaka wakati huo sikua nimejua sababu ya yeye kuja akiwa katika muonekano huo, lakini pia muonekano wake haukuonyesha kama alikua amelala kabisa kwani alikua na earpieces masikioni au wengine huita covert earpiece.

Kwa kutumia lugha rahisi Kwa wale wasio jua earpieces, ni vile vidude ambavyo wana usalama huweka masikioni kwa ajili ya mawasiliano yao ambayo mara nyingi huwa ni mawasiliano ya siri.

Mara nyingi huwekwa kwenye sikio moja na huku kukiwa na kawaya nyuma ya sikio hilo. Waya huo huenda moja kwa moja kwenye radio na wakati huo mic akiwa karibu na mdomo.
mara nyingi wanashauri mic ikae kwenye kola ya shati au kwenye mikono ya mashati yale ya mikono mirefu na maeneo mengine ya karibu ila sio mdomoni kabisa.

bongo tunaziona sana kwa wale wazee wanaovaaga kaunda suti nyeusi. Kazi yake hizi hutumika kwenye mawasiliano baina ya afisa mmoja na mwingine au hutumika purposely kwa ajili ya kupokelea maelekezo kutoka command center.

Mataifa ya wenzetu walishaendelea kwenye hizi technology sikuhizi wanatumia invisible earpieces yaan kanakua ni ka chip kadogo sana. Kanaweka sehemu ambayo ataukiangalia huwezi gundua kama huyo mtu anahiyo kitu masikioni kwake.

Turudi kwenye simulizi yetu sasa tuachane na habari za earpieces kwani nadhani kila mmoja ameelewa nazungumzia nini nikitaja hizi covert earpiece.

FATEMEH: Who were you talking to?
( Ulikua unaongea na nani?)

MIMI: a friend
( Mshkaji wangu)

FATEMEH: what is his name and where is he?
( Anaitwa nani na yupo wapi)

Kabla sijajibu maswali yake nilimsikia anaongea na mtu kwenye zile earpieces, ilikua ni kama anapewa maelezo kuhusu kile nilichokua naongea na bwana Malugu.

Hawa jamaa wapo fasta sana kwani mpaka muda huo kulingana na nilivyomsikia fatemeh ilionekana walisha track namba ya mtu niliyekua naongea nae.

Kwa lugha rahisi ni kwamba walishafika mpaka chuo na muda huo walikua na Malugu lakini bila Malugu mwenyewe kujua nini kinaendelea.

Mpaka hapo nilijua jamaa wapo serious na wananifuatilia kweli kwani ata ningetaka kuvusha demu nisingefanikiwa. Japo sina uhakika ila nilihisi kutakua na camera pia ndani ya chumba kile.

Swala la mimi kutumia simu ilionekana liliwastua wengi Kwan walikua na uhakika sikua na mawasiliano na mtu yoyote ndani ya mji huo.

Hapo niliwaza ata yule Damião kuna uwezekano mkubwa akawa ni miongoni mwa ma agent wao na anaujua mchongo mzima.



Fatemeh aliniamisha chumba nikaenda kwenye room yake hakutaka nichukue Chochote kwenye room ile. Niliacha kila kitu kama kilivyokua au kama nilivyokikuta.

Tuliingia kwenye room yake ambayo nayo pia ilikua ni Grand residence lakini kwenye room yake kama kulikua na mambo mengi ya ziada.

Kitanda nilikikuta kikiwa vilevile nikimaanisha hakukua na dalili ya mtu kulala kwenye kitanda kile. Nilifika nikakaa kwenye sofa iliyokua karibu kabisa na dirisha kiasi kwamba nililiona jiji kwa sehemu kubwa.

Fatemeh au Manuela alikua bize kwenye tarakirishi (computer) yake, Lakini pia alikua bize kusikiliza kitu kupitia earphones za kawaida sio tena zile earpieces na hapo niligundua alikua ana sikiliza yale mangezi yetu na Malugu.

Ilionekana wenzie walimtumia tafsiri ya kile tulichokua tunakiongea kwani fatemeh hakujua kabisa kiswahili ata cha kuombea maji.

Baada ya kuwa ameipata tafsiri ya maongezi yetu aligeuka akaniangalia kwa namna kama ameni mind hivi.

FATEMEH: there is a necessity for you to have sex
( Kuna ulazima wa wewe kufanya mapenzi leo)

Fatemeh hakua muongeaji kabisa toka tutoke haullaga, aliuliza kama kuna ulazima wa mimi kufanya mapenzi.

Alisema kama nikikosa mbususu naweza kufa au ku paralyze basi aongee na Damião aniletee demu, ila sharti moja tu nitafanya palepale yeye akishuhudia.
maana hawezi kuniacha peke yangu tena nisije chana mkeka kama anavyoenda kuchana leo Man City (jokes).


Karibia Whatsapp tuko mbele sana kutoka hapa 0623329512, leo tulikua na shahzad ila tatizo la shahzad na wale wazee wenye story nyingi mpaka anatoka kwenye nje ya mada.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
😂😂😂😂🤣🤣Unitag mkuu
 


😂😂😂Mkuu unitag jaman.
 
Duuuh!! Wenzetu wapo mbele ya muda mkuu. Yaaani chap wakadukua na maongezi na kupata tafsiri chap na Manuela akatumiwa asikilize. Hatari Sana hiyo ukifananisha na huku kwetu. Watu wanatekwa katikati ya mji na watekaji hawajulikani. Noma sana
 
Masawe! Katika jambo ambalo huwa ninatafiti ni asili ya sisi watu weusi.
Nadharia ambazo nimewahi kusoma ni kuwa wabantu sio watu wenye asili ya Africa, hivyo basi yawezekana ukawa kweli wachaga sio watu wenye asili ya Africa ila ni kweli kabisa wachag mpo kundi la wabantu kimuonekano wa maumbile.
Ktk kutafiti kwangu watu wenye asili ya kuwepo haspa Afrika ni bushmen na pilgrim.
Katika kutafiti kwangu wabantu walivamia maeneno ya hawa watu na kuwaua na sehemu kama kongo waliwala(carnibalism).
Wachaga mnafanana sana na kabila la wakati lililopo kongo.
Masawe historia yetu haituoneshi moja kwa moja who are we, and where we come from.
There is vacuum of knowledge!
 
Daah ni kweli mkuu, historia yetu ya hapo kabla haikuandikwa popote hivyo tunaishi kwa assumptions tu.

Kitu kinachoumiza zaidi ni kuona leo tunasoma historia yetu ambayo imeandikwa na wageni unadhani wataandika nini hawa wageni.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…