Room ile ndani ya hotel hiyo ya Costa del Sol Wyndham ilikua ni Grand residence, kulikua na huduma nyingi sana ndani ya chumba hicho ukilinganisha na room nilizowahi kukaa kwenye hotels nyingine hapo kabla.
Tukiwa ndani kabla fatemeh hajaondoka kuelekea kwenye room yake, nilimuomba fatemeh jambo moja kama ataweza kunisaidia.
MIMI: can you please do me one big favor
( Kama hutojali naomba unisaidie jambo moja )
FATEMEH: what is that thing?
( Ni jambo gani hilo)
MIMI: i need to meet someone at Tehran (Shahzad)
( Nahitaji kukutana na mtu mmoja huko Tehran anaitwa Shahzad)
Fatemeh aliuliza Shahzad ni nani?? Alionekana kutokumjua kabisa wala kusikia taarifa zake mtu huyo.
Nilijaribu kumueleza kwa ufupi sana kama ni mtu ambaye yeye na ukoo wake wanaijua vizuri historia ya mji wa zamani uliopatikana huko pwani ya Africa mashariki.
Mji huo ulizama baharini na hazina kubwa sana ya mali hususani dhahabu. Habari hizo kwa mara ya kwanza niliziskia kwa bwana Javier ambae naye habari hizo alizipata huko Düsseldorf kwa aliyekua veteran wa ki-NAZI bwana Schulz.
Nilimueleza fatemeh nia ya kukutana na jamaa huyo aliyejulikana kwa jina la Shahzad, nia yangu ilikua kuonana nae kama tunaweza kushirikiana turudi tena bongo kupambana na kuona tunaipataje mali hiyo iliyo ndani ya mji huo.
Fatemeh aliuliza kwanini nisirudi tu bongo alafu hilo zoezi nilifanye mi mwenyewe kwani tayari nimeshajua mji huo ulipo kupitia taarifa ya Javier.
Hapa nilimjibu kuwa taarifa za Javier hazijitoshelezi bado kuna uhitaji wa kuwa na ile original document iliyoandikwa na muasisi mwenyewe ambae ni Claudio Ptolemy.
Lakini ukiacha documents hizo, uwepo wa watu wa familia hiyo ni muhimu kwani wao wana taarifa nyingi za ziada zilizohusu mji huo.
Nilimsisitiza kuwa ndani ya nchi yetu sijawahi kabisa kusikia watu wakiongelea mji huo apa maana yake wengi bado hawajui lolote kuhusu mji huo.
Apa nilimsisitiza kuwa ata mimi mwenyewe nilimaliza shule level ya sekondari bila kusikia taarifa zozote kuhusu mji huo.
Fatemeh aliuliza swali lingine ambalo lilikua ni la msingi sana hapa alitaka kujua kama anatakiwa sasa kubadili destination sio tena dar es salaam hivyo nitafatana nae Tehran.
Kwa kujiamini sana nilijibu hivyo kwamba bado nahitaji kufuatana nae ili nikakutane na mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Shahzad.
Kuna muda fatemeh alisita lakini nikaona kabisa amekubaliana na mimi kuhusu kughaili safari ya bongo na kuelekea Iran.
Hapa sasa nilipewa masharti machache sana kuhusu Iran na ni kwa jinsi gani nitakaa huko kabla ya kurudi tena dar es salaam.
Fatemeh alisema nikiwa huko sitafanya chochote wala sita kwenda popote wala sitakutana na yoyote pasipo idhini yake.
Kwangu lile lilikua jambo jepesi sana kwani sikua mwenyeji huko hivyo nisinge kua na mishemishe zozote ndani ya mji huo.
Aliendelea kunisisitiza kuwa tulikua na vita mpya tumeianzisha na Javier, hapa aliendelea kusisitiza kama Javier sio mtu wa kawaida alikua na mtandao mkubwa hivyo amani yetu itatengemaa pale ambapo Javier atakua ametiwa nguvuni.
Shida kubwa iliyokua inawapa hofu idara ya MOIS na wale agents wake wengine akiwemo fatemeh, ni kwamba kikundi kile ambacho alikua anatokea Javier kilikua kinapata support kubwa kutoka kwa USA yani (taifa la marekani) lakini pia Israel intelligence service hawakua nyuma kwenye kuwasapot kikundi hiki cha TONDAR pia.
Fatemeh alisema toka kuanzishwa kwake kikundi hicho miaka ya 1999 chini ya bwana mmoja aliyeitwa Fathollah Manouchehri au maarufu kama Farvand Fooladvand.
Kumekuwepo na shaka kubwa baina ya serikali ya Iran kwamba kikundi hicho kilipata support kubwa kutoka kwa washirika wake hao ambao ni marekani na Israel.
Hivyo basi serikali ya Iran inachukulia jambo hili kwa umakini mkubwa kwani linahusisha mataifa makubwa yenye taaluma kubwa ya kiinteligensia.
Na ushahidi waliokua wakiutafuta utaenda pia kuwathibitishia uwepo au ushirika wa marekani kwenye kikundi hicho ambacho serikali ya Iran ilikiita kikundi cha kigaidi.
Hivyo basi fatemeh aliendelea kunisisitiza kuwa tunatakiwa kuwa makini sana ata mimi mwenyewe mpaka muda huo natakiwa kuwa under intensive care mpaka pale jambo lao litakapo kuwa limefikia muafaka.
Fatemeh aliniomba nipumzike, lakini mpaka wakati huo kuna ka uoga kalikua tayari kameniingia baada ya kujua nipo kwenye hatari kubwa muda wowote.
Lakini fatemeh alinitoa hofu hiyo kisha akaniambia kwa uwepo wake eneo hilo hakuna kitu kitaharibika kwani ata room ambayo naenda kulala ipo safe zaidi ndio maana yeye alitangulia hivyo hakuna baya lolote litanipata.
Sura yangu ya uoga na hofu haikujificha kabisa kwa yoyote ambaye angeniona kwani jasho lilinitoka usoni especially baada ya kusikia kuna mkono ata wa Israel kwenye jambo lile dogo sana.
Kwa story nilizowahi kusikia kuhusu Israel niliamini wanaweza ata kuingia ndani ya room ile bila yoyote kujua na kisha wakaondoka na mimi.
Nilitamani kumuambia fatemeh tukalale wote ila nilijua hatowaza kwamba naogopa ila atawaza ni miongoni mwa mbinu zangu za kutaka kuchakata mbususu.
Hivyo niliamua kujikaza kiume tu kwani mpaka wakati huo nimeshapitia magumu mengi nimesha lala kwenye deck ya meli ( hatch cover) usiku kucha tena ndani ya bahari ya pacific.
Sasa napataje uoga kulala kwenye grand residences room nzuri kama hiyo huo utakua ujinga wa kiwango cha rami.
Fatemeh aliondoka na kuniacha room, kwa staili aliyoondoka fatemeh au manuela ni kama mama anaemlaza mtoto na kisha kufunga mlango na yeye kuelekea chumbani kwake.
Kwani baada ya kuondoka fatemeh ( Manuela) nilijifunika blanket bila kuchelewa kwa namna kama najificha.
Sababu ya kufanya hivyo nilikua nahofia mengi sana wakiwemo CIA na hao wazee wa kazi wana wa israel. Kuna muda niliwaza mawazo ya kitoto sana eti ikitokea wamekuja wazee wa kazi wa Israel ( MOSSAD) nitawaambia kuwa mi ni mchaga.
Wote si mnajua zile story zinasema wachaga asili yetu ni Israel, naogopa kusema nitawapa hii story wakati mwingine maana nimeahidi mambo mengi lakini unachotakiwa kujua ni hivyo sisi wachaga huku bongo tulipotea njia kabisa kwetu ni mashariki ya kati.
Kifupi tu wachaga asili yetu ni kaskazini mwa Ethiopia na maeneo ya Eritrea ambapo kuna kabila dogo lenye asili ya huko Israel kabila hilo lilikua kwenye miliki ya watu wa aksumite na liliitwa Beta.
NONDO ZINAENDELEA KUSHUKA WHATSAPP 0623329512
Sent from my ZTE T1002 using
JamiiForums mobile app