Utajiri wa Magofu ya Rapta

Utajiri wa Magofu ya Rapta

-Pale Sengerema sec ukipandisha juu Kuna Kijiji kinaitwa Mwabarui,,,,kingine Nyancheche[emoji38]

-Headmaster alienda masomoni,kurudi akakuta mkewe anawatoto mapacha(sitomtaja jina)[emoji1787]

-Vyoo vilifungwa tulikua tunatumia Chaka[emoji119][emoji119][emoji119]

-Kulikua na mafunzo ya mgambo form two,,,wanafunzi walilala wakaamka wakagoma[emoji119][emoji119]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] we kweli umepita sengerema, unaikumbuka chaka hahaha, mi niliishi kimweri baadae nikahamia mandela pale kuna maisha fulani ukimuelezea mtu hawezi kuamini kabisa.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Hii comment sikuwa nimeiona, ila ni hivi boss wangu mpaka sasa hakuna sehemu nimetaja mwaka 2016 na kama itakuwepo basi ni typing errors. huo mwaka kama nitakuja kuutaja basi baadae sana tukielekea mwishoni.

Na kuhusu kifo cha merry ni kweli kabisa kilitokea mwaka huo wa 2012 na kuhusu kifo cha mwanafunzi aliyetumbukia chooni ule mwaka wetu ni kweli kabisa.

Unachotakiwa kujua ni kuwa haya matukio yalitokea kuanzia mwaka 2012 na ikitokea nimetaja mwaka wa hivi karibuni mfano 2020 basi apo ujue na refer tukio mfano nilishasema javier alikamatwa yeye na sharmahd mwaka 2020.

Naomba tusisome simulizi kwa kutafuta weakness kwani tutapoteza concentration STAY POSITIVE.
Kama kuna mwenye maswali zaidi karibieni Whatsapp bila kusahau aftatu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
Mkuu naomba nikushauri Jambo Kama hutojali, achana na comments ambazo zipo kukosoa, kuna watu wapo kupinga Kila Jambo hata Kama hawana lolote wajualo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] we kweli umepita sengerema, unaikumbuka chaka hahaha, mi niliishi kimweri baadae nikahamia mandela pale kuna maisha fulani ukimuelezea mtu hawezi kuamini kabisa.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
Mi nilikua nakaa mirambo

Pale Kuna story ya Binti kibasila
 
Huyo Fatemeh atakuwa alifundishwa uspy na vladimiro montesinos aliyekuwa spymaster wa Peru rais fujimori akiwa chini yake
 
Najua kuna maswali mengi sana wasomaji wanajiuliza. Lai yangu ni moja tu, naomba tuisome kwa kutulia sana hii kitu inamambo mengi ndani yake.

Na nipo hapa kujibu kila doubt au sintofahamu yoyote anayokutana nayo yoyote kwenye simulizi hii.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
Kuna wajuba wanasema eti hii ni stori ya kutunga mkuu, unalizungumziaje hili? Natamani iwe true story! Napenda sana true story!
 
Hii comment sikuwa nimeiona, ila ni hivi boss wangu mpaka sasa hakuna sehemu nimetaja mwaka 2016 na kama itakuwepo basi ni typing errors. huo mwaka kama nitakuja kuutaja basi baadae sana tukielekea mwishoni.

Na kuhusu kifo cha merry ni kweli kabisa kilitokea mwaka huo wa 2012 na kuhusu kifo cha mwanafunzi aliyetumbukia chooni ule mwaka wetu ni kweli kabisa.

Unachotakiwa kujua ni kuwa haya matukio yalitokea kuanzia mwaka 2012 na ikitokea nimetaja mwaka wa hivi karibuni mfano 2020 basi apo ujue na refer tukio mfano nilishasema javier alikamatwa yeye na sharmahd mwaka 2020.

Naomba tusisome simulizi kwa kutafuta weakness kwani tutapoteza concentration STAY POSITIVE.
Kama kuna mwenye maswali zaidi karibieni Whatsapp bila kusahau aftatu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
Nimepata majibu! Tusonge mbele....!
 
TUNAENDELEA KAMA KAWAIDA

Tuliongea mambo mengi sana na Malugu lakini pia ule uhuru wa kuongea kiswahili nilijiskia kama nimerudi nyumbani tu lakini sio mimi pekee ata bwana Malugu alionekana kuwa na amani.

Damião aliniambia ananipa nusu saa ya kubadilishana mawazo na malugu kwani nilionekana kufurahia sana kuonana nae. Yaani utafikiri tulishawahi kukutana apo kabla kwa jinsi tulivyokua tunaongea.

Malugu aliniuliza nina mishe gani kule kwani ni mara chache kukuta wabongo kwenye nchi hiyo. Nilitamani kumueleza kila kitu lakini niliona bado mapema sana.

Nilichomwambia ni kwamba nimekuja huko kufanya kazi mgodini na kwa bahati mbaya ule mgodi siujui ata jina.

Alioniuliza ni mgodi gani akitaka kujua jina la mgodi lakini pia akaniuliza ni sehemu gani ndani ya nchi hiyo nilishindwa kumpa jina la mgodi ila nilimwambia mgodi upo Cerro de Pasco.

Malugu alinielewa na alisema mji huo wa Cerro de Pasco una migodi mingi kwani hata kijana niliyeongozana nae yaani Damião alishawahi kufanya kazi kwenye moja ya mgodi kwenye mji huo huo wa Cerro de Pasco.

Kwenye hiki chuo kwakua kozi zote au kozi nyingi ni zile zinazohusu engineering basi wengi wanaitana kwa initial za engineer. nilisikia wengi wakimuita jamaa engineer Simon huku wakiacha kutumia jina la Malugu nadhani kwakua lilikua gumu kwa upande wao.



Malugu aliomba anipeleke mpaka kwenye makazi yake ili ikitokea nimepata changamoto yoyote iwe rahisi kumfikia kwani nilimueleza kwamba sikua na ndugu yoyote uko.

Kwa maelezo ya malugu aliniambia nisiwe na hofu kwani sisi tayari tumeshakua ndugu. Tuliunganishwa na rangi lakini pia na utaifa yaani utanzania wetu.

Nilitumia saa nzima kupiga stories na Malugu baada ya nusu saa niliyopewa na Damião, hata yeye Damião aliniachia muda wote huo kwakua alikua bize na mambo yake.

Nilimueleza malugu kuwa nilisoma sengerema lakini yeye pia aliijua vizuri sana shule hiyo. Na mara nyingi aliijua shule hiyo kupitia mashindano ya umiseta kwenye ngazi ya mkoa.


Miaka ile shule yetu ilikua inatoa wachezaji wengi kwenye timu ya mkoa ya basket ball, kwa waliowahi kusoma pale miaka ile wanaweza kuwa na kumbukumbu nzuri kuhusu hili.

Taratibu nilianza kupata matumaini ya Maisha mapya na kuhisi mambo yangu yanaenda kunyooka sasa.

Damião alinifuata na kunitaka tuondoke kwani fatemeh alikua ameshamaliza mipangilio yote hivyo nilitakiwa kuonana nae.

Malugu aliniomba namba ya simu, lakini nilipo mjibu sina simu alistuka sana kwamba inawezekana vipi nipo nchi ya watu na sina simu. Hivyo machale kama yalianza kumcheza akahisi kuna kitu hakipo sawa kwenye safari yangu hiyo.


Hakuongea chochote akaniacha niondoke lakini tulipoachana umbali mdogo aliita

MAKUNGU, MAKUNGU MAKUNGUUU

( Yaani bora angeniita mustapha ningekumbuka kama naitwa Mimi, hili jina la makungu halikua limekaa kichwani kabisa)

Hivyo basi aliniita karibia mara tatu lakini sikuweza kustuka wala kuhisi naitwa mimi. Mpaka aliponifuata na kunishika mkono,
( Nadhani alitumia jina la makungu makusudi ili kupima ni kweli jina hilo ni langu)

MALUGU: dogo niambie ukweli umekuja kufanya kazi gani huku maana mpaka sasa nimethibitisha hili jina sio lako.

Safari hii Malugu alinifuata akiwa serious kwani alionekana kuwa na wasiwasi sana hivyo alikua ana sisitiza kama nipo huko kwa magendo ni bora nimuweke wazi anaweza kunisaidia kutoka huko.

Aliendelea kusema wengi hutolewa Africa na kupelekwa huko kwenda kufanya kazi kwenye mashamba ya cocaine na wengi wa vijana hao huteketea huko.

Alitumia kiswahili akiwa na uhakika kwamba Damião asingeambulia kitu.

Nilichomjibu ni kimoja tu asiwe na hofu huyo aliyeniona nae ni moja ya wanafamilia walionisaidia kutoka kwenye kadhia hiyo ya mashamba hayo ya cocaine. Hivyo kwa wakati huo nilikua nipo mikono salama, japo malugu hakuonyesha kuridhika kabisa niliagana nae na akanipa karatasi iliyokua na namba yake ya simu.

Mpaka hapo tulikua nje ya muda sana kwani tulijiongezea ratiba nyingine ambazo hazikua rasmi kwa muda huo.

Hivyo basi Damião alisisitiza tuchangamke kuelekea eneo la kuegesha magari ili tumuwahi fatemeh (Manuela).

Kulikua na umbali mfupi sana kwa gari kutoka eneo tulilokuwepo mpaka kufika kwenye hotel moja iliyojulikana kama Costa del Sol Wyndham.

Ilikua hotel moja ya hadhi ya juu sana ukilinganisha na hotel kadhaa nilizowahi kuingia mpaka siku hiyo. Damião ambae ndio alikua mwenyeji wangu alionyesha kuwa familiar sana na maeneo yale.

Kwani tuliingia ndani kabisa na hapo tulikuta counter moja ya kisasa na kuna bwana mmoja kama ana asili ya kiarabu.
Bwana huyo alionekana kuwa ndio mtaalamu wa mambo ya cocktail kwenye counter ile ya hotel hiyo. Apa niligundua Damião alikua ni mtumiaji mzuri wa cocktail kwani kuna maelekezo aliyotoa na jamaa akaanza ku mix vitu vyake ili kutoa kinywaji.

Simu ya Damião iliita, baada ya kuipokea nilisikia akisema kwamba namleta muda si mrefu hapo nilijua fatemeh alihitaji kuniona na yupo ndani ya hotel hiyo.

Tulitoka na Damião pale counter na kuelekea eneo la makutano ya watu, Damião alinionyesha meza ya kukaa na yeye akarudi zake kwenye cocktail kuendelea kuchoma maini.

Nilipofika kwenye meza aliyonielekeza Damião nikakae nilimkuta mwanamke akiwa tayari amekaa eneo hilo akiwa na kinywaji ilikua ni juice.

Mwanamke yule alikua amevaa kiremba maarufu kwa jina la roo-sari kwa nchi zile za Iran huku akiwa na koti refu kwenda chini likijulikana kama roo-poosh.

Uvaaji huu zilikua ni codes za wanawake wa Iran katika kujistili maungo yao yasionekane. Kwa kuwa nilielekezwa meza hiyohiyo niliamua kukaa bila kujali aliyekaa hapo alikua ni nani.

Kwakua aliyekuwepo eneo hilo alikua ni muislam basi na mimi nikasema ngoja nishushe salaam kama ya shekhe kipozeo (mzee wa mizigo) jokes

MIMI: asalaam aleykum

Waleykum salaam ( kumbe alikua manuela bana au fatemeh kama wanavyomjua wengine)

HUKO KWENYE PDF TUPO NA SHAHZAD ANAANZA KUSHUSHA NONDO ZAKE KUHUSU MJI WA RAPTA

0623329512 Whatsapp tu!!!!!

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom