Utajiri wa Magofu ya Rapta

Kuna mambo mengi sana yalinishangaza yanayomuhusu Javier, kwanza Javier alikua smart sana kwenye mambo kadhaa. Mfano, alikua smart kwenye maongezi yaani kila anachoongea kina maana na logic pia. Javier hakua muongeaji sana ila ni wale watu ambao wakianza kuongea huchoki kuwasikiliza.

Javier hakua mtumiaji wa mihadarati wala aina yoyote ya madawa ya kulevya. Kitanda anacholala Javier kilikua kimetandikwa muda wote tofauti na kile kitanda nilicholala kilikua rough sana.

Mtu Yoyote asinge gundua u smart wa Javier kwa kumuangalia mara moja tu, kwani kilichokua kinaficha utanashati wake ni zile nywele ndefu pamoja na ndevu zilizoonekana kuwa hazikuchanwa kwa zaidi ya miezi 12.


Kuhusu bwana Javier, Kwa maumbile ya nje ukimuona unaweza kuhisi ni mtu Fulani legelege au dhaifu na asiye na afya. lakini binafsi nilikanusha hilo baada ya kukaa nae muda usiopungua masaa matatu tukiongea mambo kadhaa.

Nilimuuliza swali Kuhusu uwepo wa baadhi ya vitu nilivyoviona juu ya kenchi eneo ambalo kitanda changu kilikuwepo.

Kwa mujibu wa maelezo yake vitu hivyo vilikua mali ya muafrika mwenzangu ambaye alikua anatumia kitanda hicho nilicholala kabla sijafika.

Nilimuuliza pia vipi kuhusu muafrika huyo je! Aliondoka eneo hilo?

Javier alitabasamu kidogo kisha akaniambia kwenye akili yangu nisahau kabisa kuhusu kutoka eneo hilo. Kwani kuna wengi walikuwepo hapo wakiwaza kurudi nyumbani baada ya ku accumulate kiasi fulani cha pesa lakini ilishindikana na wakafia hapo.

Hapo niliuliza je! Tunazuiliwa kutoka baada ya kuingia humu au inakuaje?
( binafsi Nilihisi tunazuiliwa kutoka baada ya kuingia, maana eneo hilo kulikua na ulinzi mkubwa japo haikua rahisi kuona kwa macho)

Kwa maelezo ya Javier ni kwamba hawakuzuii physically bali psychologically,
Sikumuelewa kabisa alimaanisha nini na yeye alisema nitaelewa baada ya muda. Kwakua nimefika hapo bado nina ugeni hivyo siwezi kuelewa kilakitu kwa wakati mmoja.

Aliendelea kwa kusema kuna kijana ye alimkuta hapo alikua akiitwa Gatkuoth, Gatkuoth kwa Miaka kadhaa alikua na ndoto ya kufika hapo kisha kukusanya pesa na kurudi nyumbani kwao lakin kwa bahati mbaya umauti ulimkuta akiwa hapohapo huku ndoto za kurudi nyumbani zikiishia hewani.

"Gatkuoth ndiye kijana wa kiafrika aliyekua anatumia kitanda hicho ulicholala" aliongea Javier
Alikua ni kijana mweusi sikuwahi kupata kuona mweusi wa rangi ile hapo kabla japo nimekutana na vijana weusi kadhaa kwenye maisha yangu ila Gatkuoth alizidi.

Nilikutana na vijana weusi maeneo tofauti tofauti ya dunia hii kama vile Quebec na wengine California ila hawakumfikia Gatkuoth. Ukiachana na rangi Gatkuoth pia alikua mrefu nadhani alifikia 7ft, tulithibisha hilo wakati tunajiandaa kuzika mwili wake.

Baada ya kukaa nae kwa muda mrefu nilipata kuyajua mengi kuhusu Gatkuoth, kwanza nilifanikiwa kujua kua Gatkuoth alikua anatokea South Sudan Western Bahrel Ghazal.

Javier aliendelea kusema "naomba nikueleze kila kitu kuhusu kijana mwenzio wa Africa ili na wewe yasije yakakukuta yaliyomkuta. Na kisha ndoto zako zikaishia hapa. Sababu unaonekana kua Innocent na umekuja bila kujua nini kinaendelea apa UHV"

Maisha ya Gatkuoth yalianza kua magumu alipofikia umri wa miaka 16 baada ya kupoteza wazazi wote wawili April mwaka 2003. Alipoteza wazazi kwenye machafuko huko magharibi mwa Sudan (Darfur) wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Kwakua hakua na msaada mwingine Gatkuoth alijiunga na kikundi cha waasi kilichoitwa janjaweed. Chenye makazi yake hukohuko Sudan na nchi nyingine jilani Chad, alidumu kwenye kikundi hicho kwa miaka isiyopungua 7 mpaka pale siku alipogundua ata mauaji ya wazazi wake yalifanywa na kikundi hicho hicho cha janjaweed.
Baada ya kugundua kuhusika kwa janjaweed kwenye mauaji ya wazazi wake ndipo alipojitoa kwenye kikundi hicho kwa kukimbilia nchini somaria ambapo alikutana na marafiki ambao walioshauriana kutimkia South America.

Akiwa Sudan hakuwahi kabisa kutumia dawa zozote za kulevya isipokua baada ya kufika somaria ndipo alipoanza kujiunga na vikundi hivyo ambavyo vilijihusisha pia na utumiaji wa dawa hizo.

Akiwa somaria ndipo alipata fursa ya kuja huku, target yake ilikua atafute pesa ili arudi tena nchini kwao.

Aliichukia sana siasa akiamini ndio chanzo cha vita kwenye nchi yake lakini pia ni chanzo cha kifo cha wazazi wake wote wawili. Hivyo ndoto yake ilikua ni kutamani kuimaliza vita hiyo kwa namna yoyote japo haikua kazi rahisi kwa mtu ambaye hajawahi kufika shule kabisa.
Mpaka hapo niliamini Gatkuoth alikua hajui kusoma wala kuandika.
Baada ya kusikia hakuwahi kufika shule kabisa kwenye maisha yake.

Gatkuoth alijikuta ameingia kwenye matumizi ya kupindukia ya madawa ya kulevya baada ya kua amekata tamaa kabisa ya maisha aliamini hana future. Alitamani sana kurudi kwenye kaburi la mama yake na baba yake lakini haikua rahisi tena.

Javier alimalizia kwa kusema "mwaka jana yaani 2011 Sudan kusini ilitambaulika rasmi kama nchi huru. Nilitamani sana kumuona Gatkuoth anarudi kwao kwani ndoto yake ilikua imetimia ya kuiona Sudan kusini inakua sehemu salama kwa raia wake.

Lakini ilishindikana kwa Gatkuoth kurudi kwani alikua kwenye hali mbaya huwezi mpeleka popote.

Mpaka sasa mwezi umepita tangu Gatkuoth afariki akiwa amelala kitandani hapo, ilituchua mpaka siku mbili kujua kama Gatkuoth alikua amefariki. Hakuna aliekua anamjali ata akiumwa kwani hakua na msaada kabisa, sababu hakua tena ata na uwezo wa kufanya shughuli yoyote hivyo alikua useless.

Gatkuoth nimemzika mi mwenyewe kwa mikono yangu nikisaidiana na watu wengine wawili waliokuja kunipa msaada baada ya kuona hakuna mtu anaejali msiba ule.

Umejifunza nini kwenye maisha ya Gatkuoth? Lilikua ni swali la Javier.

Wakati nataka kumjibu aliniambia kama kuna chochote nilichojifunza it's ok haina haja ya kumwambia.


Nilitamani kujua Javier anamda gani mashambani hapo ila niligundua kuna baadhi ya maswali hayupo tayari kuyajibu.

Nilimuuliza kwa namna gani naweza toka hapo, ila alichojibu ni maneno mawili tu STAY POSITIVE.

Apo niligundua Javier anajua mengi kuhusu eneo hilo lakini Javier pia anaweza asiwe mfanyakazi wa kawaida kama wengine hivyo natakiwa kumsikiliza sana.

Siku hiyo iliisha huku tukiwa free bila kufanya shughuli yoyote nadhani ile ilisababishwa na ugeni wetu hivyo tulipewa muda wa kupumzika.

Javier alipotea kwa zaidi ya masaa matano na nilikuja kumuona muda wa kulala, alirudi kulala na nilistuka kumkuta yupo ndani sikubahatika ata kusikia hatua zake akiwa anaingia.

Alishangaa kunikuta bado sijalala na nilimwambia kua nimeshindwa kupata usingizi muda huo kwa kua mchana wote niliutumia kwa kulala.

Alikuja akakaa juu ya kitanda chake na kunyanyua pillowcase (foronya ya mto) ambayo alikua anaitumia kama begi la kuhifadhia nguo zake na baadhi ya vitu vingine vikiwemo vitabu.

Kwenye pillowcase ile alitoa kitambaa cha sufi ambacho alikifungua na kutoa copper bracelet (bangili ya shaba).
Alinikabidhi mikononi niichunguze kwa makini kisha akauliza.



JAVIER: do you real know what is this
( Hivi unajua hiki ni nini)

MIMI: yes I do! It's copper bracelet
( Ndio najua ni bangili)

JAVIER: even myself I know that it's a copper bracelet but how does it work on human body?
( Ndio najua ni bangili ya shaba lakini inafanya kazi gani kwenye mwili kulingana na taratibu za kiafrika)

Javier alisema week kadhaa nyuma kabla ya kifo cha Gatkuoth, Gatkuoth mwenyewe alimuomba ikitokea amefariki na yeye yupo kiasi kwamba atahusika kwenye mazishi yake.
Basi anamuomba asikubali Gatkuoth azikwe na hiyo bangili, aivue then na kama atakua tayari aitumie yeye au ampe mtu yoyote ambaye atai value kama kinga na dawa.


Kwa maelezo ya Javier ni kwamba bangili hiyo aliitoa kwenye mwili wa Gatkuoth ambaye alimuomba ikitokea amekufa asizikwe na bangili hiyo kulingana na tamaduni za kwao.

Kwa taratibu na miiko ya koo zao marehemu hazikwi na aina yoyote ya mapambo au urembo kwenye mwili. Hivyo kwakua Javier alihusika moja kwa moja na mazishi hayo alikumbuka swala hilo, lakini hakujua umuhimu wa bracelet ile ndio maana aliponiona mimi aliamini nitajua chochote kulingana na uafrika wangu.

Kwa bahati mbaya na mimi sikua na taarifa za kutosha zinazohusu uvaaji wa bangili hizo. Kikubwa nilichokua najua ni kwamba niliwaona watu kadhaa mtaa wakivaa bangili hizo. Lakini pia mara kadhaa nimekutana na wamasai wakiuza bangili hizo japo sijawahi kuuliza zinamanufaa gani kwa mvaaji.
Nilimuuliza Javier kama yeye alijaribu kumuuliza Gatkuoth kuhusu matumizi ya bangili hiyo. Alisema alimuuliza na akampa majibu, alichotaka kujua kutoka kwangu ni je! Na mimi nafahamu chochote kuhusu bangili hiyo.

Nilipomwambia kwamba nimeona watu kadhaa wakivaa bangili hizo mtaani kwangu basi lilikua jibu tosha kwamba naifahamu.

Nilijaribu kuongea na Javier anielezee japo kwa uchache Kuhusu bangili hiyo na alisema kwakua imetokea kwenye tamaduni za kiafrika basi atanikabidhi kabisa nitumie.

Alisema Gatkuoth alipewa bangili hiyo na marehemu baba yake kabla kifo hakijawakuta huko Darfur akiwa na mama yake mzazi miaka hiyo ya 2003


Javier aliambiwa na Gatkuoth kwamba waafrika especially watu wa misri ya kale ndio waligundua uvaaji wa shaba (genuine copper) na wakasambaza ustaarabu huo duniani kote.

Uvaaji wa bangili ya shaba husaidia mambo mengi kwa mvaaji ikiwepo afya ya mvaaji na Mambo mengine ya kiroho yaani (physical and spiritual world).

Mara nyingi tiba hizi ni tiba zisizoonekana na ni tiba za kimaajabu lakini huleta matokeo chanya kwa mvaaji. Mfano:

Mvaaji wa bangili ya shaba huponywa taratibu maumivu ya misuli na viungo hivyo wavaaji wa bangili ya shaba (copper bracelet) huwa ni wenye nguvu, afya njema na wasio na woga na hujiamini sana hii ndio nguvu ya kiroho isiyoonekana ambayo inapatikana kwenye bangili ya shaba.


Kuimarisha afya ya mishipa na moyo, kukosa madini ya shaba hupelekea mtu kuugua magonjwa yanayohusisha mishipa na moyo Aortic aneurysm
Hivyo uvaaji wa bangili ya shaba huwalinda watu na magonjwa hatari kama moyo na kupooza ni mara chache sana kukuta mtu aliyevaa copper bracelet kwa mda mrefu kuugua magonjwa ya moyo.

Huimarisha mfumo wa kinga, Javier alitoa mfano kama ambavyo chuma cha shaba huchimbiwa ardhini kwa ajili ya kupambana na nguvu za umeme wa ziada. basi hivyo hivyo ikivaliwa shaba hufyonzwa taratibu kwenye mwili wa binadamu. Na kupambana na nguvu zote chafu zinazoweza kumshambulia mvaaji.

Hupunguza uzee (anti-aging) kwakua copper ina viua sumu viitwavyo antioxidant ambazo huzuia taka na sumu za mwili kuharibu cell na kuzilinda pia. Wavaaji wengi huonekana vijana ikiwa umri umeenda.
Kwenye mambo ya kiroho alizungumzia vitu kama channel spiritual vibrations na Spiritual Energy mwisho kabisa Positive Energy ambayo tutaizungumzia huko mbele.

Hapa sasa utafanya uchunguzi wako binafsi kuhusu hizi copper bracelet either kwa wavaaji au wauzaji na ina sisitizwa kama unavaa basi vaa genuine copper kwa matokeo chanya zaid.
Kuna zaidi ya 90+ spiritual benefits of copper bracelet
( Binafsi naamini uvaaji wa copper bracelet na ukihitaji genuine unaweza kuniona au watafute madereva wa maroli wanaoenda Congo wanazijua)

Binafsi bwana Javier alinipa ile bracelet ya Gatkuoth yeye hakutaka kukaa nayo aliamini ile ni tamaduni ya waafrika hivyo haiwezi kuwa na impacts au matokeo chanya kwa wazungu.

Je! Na sisi ni tamaduni ngapi za wazungu tumezishikiria na hatufikirii kama zinaweza kuleta matokeo chanya kwenye mazingira yetu.


Next episode tutaongelea spiritual benefits za uvaaji wa dhahabu especially Kwa wankina mama

0623329512 Whatsapp


Copper bracelet
 
Poor narration... umeweka mambo mengi sana un necessarily imeboa.
 
Hahahaha Aaya bhanaa,..nimekusoma mwamba
 
Asubuhi na mapema Javier aliniamsha tukatoka nje na kushuka chini ya ngazi za banda lile ambalo lilikua na vyumba kadhaa vya kulala. Watu wote walikua bize, ilionekana wageni wote tunapokea maelekezo kutoka kwa room mate ambaye umemkuta kwenye chumba ulichopangiwa.

Baridi lilikua kali sana asubuhi ile huku wenyeji walionekana kutokua na shida yoyote hivyo ni dhahiri jamaa walizoea mazingira hayo.

Kiukweli nilikua najivunia sana kupata mwenyeji kama Javier alionekana kutokua na makuu kabisa kwenye kambi ile.

Mgawanyo wa kazi ulikua kwenye sehemu kama tatu hivi, kulikua na wale wa mashambani hawa majukumu yao yalikua ni kulima na kupanda wakati mwingine kuvuna.
Kuna waliohusika na usafirishaji wa bidhaa kuanzia majani yenyewe, chemicals na baadhi ya vifaa.

Na wengine walikua Upande wa Lab (processing lab) huku kwa upande huu wa lab kulihitaji ideas za chemicals lakini pia na uzoefu wa kutosha.

Kwa asubuhi ile nikiwa na Javier tulitembea umbali wa zaidi ya mita 400 kushuka bonde lililokaribiana na mto haullaga ambao ulikua ni tributary ya mto Maranon. Kabla ya kufikia upande wa kulia kwa juu kwenye kamsitu kadogo kulikua na banda kubwa lenye urefu wa kama madarasa mawili.

Banda hili lilijengwa kwa mbao ngumu za porini likiwa na madirisha yaliyopitisha hewa ya kutosha. Kwa juu lilifunikwa au liliezekwa kwa turubai kubwa jeupe kwa ustadi wa hali ya juu, eneo hilo kulijengwa ngazi za magogo ilikupanda kufikia banda hilo.

Kwa haraka nikajua huko ndipo yatakua majukumu yangu kwani ilionekana ndio sehemu ambayo ata Javier nae hufanya shughuli zake.

Tulipanda ngazi zile na kuribia jengo lile (banda) ambalo naendelea kusisitiza lilijengwa kwa ustadi sana. Tulipolifikia banda lile ndipo nilipogundua ilikua ni maabara, hivyo mahala hapo ndipo wajuba huchakata coca paste na kupata cocaine hydrochloride.

Kwenye akili yangu niliamini hivyo Lakini sikutaka kujithibitishia hilo mpaka nitakapo tambulishwa na Javier ambae alikua mwenyeji wangu.

Tuliingia ndani ya lile banda, kiukweli kwa ndani lilikua na space kubwa sana tofauti na nilivyokua nikiwaza hapo awali.

Kwa ndani Upande wa kushoto kutoka mlango wa kuingilia ulipo, kulikua na meza kubwa pana na nzito kiasi kwamba ata ukiwa powerful kiasi gani huwezi tingisha meza ile. Mwishoni mwa banda lile upande wa kulia kulikua na drums au mapipa mengi yaliyokua wazi.

Katika kulikua na kabati pamoja na mashine ambayo sikuweza kuitambua kwa haraka lakini mashine ile ilikua kuukuu yaani imechoka na sikudhani kama inaweza kua nzima.

Eneo lile lilikua tulivu sana na haikua rahisi kila mtu kufika hapo kama huusiki kabisa, tukiwa ndani kabla Javier hajaongea chochote walifika wasichana wawili wote wana asili ya kibrazil.
" Hi Javier, is this the new guy"
(Habari Javier, huyu ndio kijana mpya)
JAVIER: Of course
(Bilashaka)

Javier alinitambulisha kwa wale wasichana wawili ambao mmoja wapo hakukua na haja ya kuuliza alionekana ni teja kabisa. Wasichana wale waliitwa Catarina na Manuela, Catarina hakua amechoka sana ukilinganisha na Manuela lakini Wote hawa walikua ni wenyeji wa Brazil kutoka mji mmoja unaitwa Rio de Janeiro.

Catarina na Manuela walielezwa kama naitwa mustapha kutokea East Africa, Javier alimalizia kwa kusema anajua machache sana kuhusu mimi hivyo tutaendelea kujuana taratibu kwakua tutakua pamoja kipindi chote.

Catarina alikua na element flani flani kama tom-boy japo wote miili yao ilijaa tatoo. Catarina alikua ni Chainsmokers (mvutaji wa sigara aliyepindukia) niligundua hilo kwani tangu afike hapo alishamaliza kama pisi mbili za CARIBE.

Jambo lingine lililonishangaza ni kwamba toka jana yake tunafika mpaka muda huo sikukutana na mtu mnene kabisa. Wengi walikua wembamba tena wembamba kweli kweli kiasi kwamba mi sikua na mwili mkubwa kiivyo ila nilionekana kibonge kwa maeneo hayo.

Na hapa ndipo nilipogundua watu wote au asilimia kubwa ya watumiaji wa cocaine na pombe kali hawanenepi kabisa kwa sababu zifuatazo:-
Kwanza kabisa matumizi ya dawa za kulevya na pombe kali hufanya watu kupoteza hamu ya kula kwa point hii unaanzaje kupata mwili.

Matumizi ya dawa za kulevya kwa wingi Hupunguza uwezo wa mwili kutunza fat ( reduce body ability to store fat)

Mwili hupoteza au huchoma calories nyingi kwa mvutaji wa dawa hizo na mtumiaji wa pombe kali.

All in all utumiaji uliokithiri wa dawa hizi especially cocaine, madhara makubwa huja kwenye ubongo na mwili kwa ujumla.

Kwa kuwaangalia tu, Catarina na Manuela walionekana ni watu ambao wapo huko kwa muda mrefu na maisha yao yote wataishi huko.
Wote kwa pamoja walivalia tshirts pana za mikono mifupi zilizofanya tattoo zao za mikononi kuonekana kirahisi sana.

Asilimia kubwa ya wafanyakazi wa eneo hilo ni wale watu ambao waliwahi pia kua na criminal cases kubwa hivyo kuwepo eneo hilo ilikua kama wapo mafichoni. Yaah ni mafichoni kwakua hakukua na serikali yoyote kule na haikua rahisi mtu yoyote kufika maeneo hayo.

Nilihisi hilo ata wale mabinti pia kwa mfano Manuela alionekana kuwa mrembo sana ila ni unga ndio ulimdhoofisha na kumuharibu. Mpaka anaenda huko lazima kuna sababu iliyompush kwenda huko, niliamini ninavyoendela kuwa nao karibu nitajua mengi.

Baada ya utambulisho, Javier aliwaambia kuwa mi ni mgeni kabisa kwenye tasnia husika na hakuna ninachofahamu hivyo nahitaji msaada wao ili kuanza kazi.
Catarina alikua wa kwanza kuniuliza kama nimewahi kutumia cocaine.

CATARINA: have you ever taste cocaine
( Umewahi kuonja cocaine)
MIMI: NO!!!!!
(Hapana sijawahi)
CATARINA: do you want to make a try
(Vipi unataka kujaribu)
MIMI: i don't
(Sitaki kabisa)
Walicheka sana baada ya jibu langu lile kwamba sitaki kujaribu kabisa, ni wazi kilichowachekesha ni kilekile alichokisema Javier kwamba vijana wa kiafrika hua tunakuja na mipango mingi lakini baadae inapotela hewani.

Manuela hakua muongeaji sana zaidi ya kuvuta sigara muda wote na wakati huu niliona ameshika chupa ambayo ni dhahiri ilikua ni chupa ya pombe. Mabinti hawa waliridhika na maisha ya hapo huwezi kudhania eti wanawaza maisha mengine mbali na hapo.

Catarina alinipa assignment moja ambayo kwangu ilikua simple sana kwani nilitumia idea zangu chemistry kujibu kila nilichoulizwa.

Catarina swali la kwanza kuniuliza ni alitaka kujua tokea nimeingia ndani ya jengo lile ni kitu gani nilichokiona na nakijua vizuri.

Lilikua swali rahisi sana,
Kwa kujiamini nilimjibu kuwa cha kwanza ndani umo niliona organic solvents ambazo zilikua ni benzol, gasoline na kerosene
(Apa kama hukuwahi kusoma chemistry kwakweli sina msaada kwako we kalili tu)
Kama huzijui ni nini organic solvents subiri wakati wa maelekezo ya kutengeneza cocaine hydrochloride nitaelezea kwa undani kila kitu.

Kwa kujiamini tena nilimwambia nimeona alkaline material (baking soda) lakini pia kulikua na sulfuric acid.

Kwa mara ya kwanza niliiskia sauti nzito ya Manuela akiuliza
MANUELA: you are a lab technician
(We ni mtaalam wa maabara)

MIMI: I'm not a lab technician anymore but I knew them when I was highschool
( Hapana mimi sio mtaalam wa maabara ila nimezijua nilipokua highschool)

Catarina alitabasamu na kusema sasa wamepata mtu sahihi kwani kama nimezijua chemicals hizo bila kuelekezwa basi ata kazi ya michanganyo haitokua ngumu wakinielekeza.

Sijisifu ila kwakweli nilikua na kichwa chepesi sana, namshukuru mwalimu wangu wa chemistry SENGEREMA alikua anaitwa dibro jina la utani, concept zake zilinifanya nionekane genius na specialist ambae nilikua moto wa kuotea mbali ndani ya muda mfupi sana kwenye maabara lie ya porini.

Mwanzoni Catarina alionyesha dalili ya kunidharau lakini baada ya kuzichambua chemicals zile sio tu kwa kutaja majina bali na kuzielezea sifa zake nyingine ambazo ata yeye hakua akizijua. Catarina alianza kua mpole na kuonyesha kutaka kujua vingi kutoka kwangu.

Muda huu Javier alikua pembeni anatuangalia niigundua ata yeye hakuamini alichoisikia kutoka kwangu.

Ni hivi kwenye lab zile za coca hazihitaji mkemi wa elimu kuuubwa bali zinahitaji ujue kwenye hatua ipi unatumia chemical ipi na kwa kiasi gan basi.

Hivyo ata hawa niliowakuta lab ni kama walikalilishwa tu chakufanya na sio kwamba walikua ni ma expert kiiivyo.

Manuela aliniangalia mkononi na kuona copper bracelet ambayo nilipewa na Javier. Alinishika mkono na kuingalia vizuri, Javier aligundua kama Manuela anaifananisha bracelet hiyo na ile ya Gatkuoth.

JAVIER: what are you wondering? I am the one who gave him
(Unashangaa nini Manuela, mimi ndio nilimpa)
Wakati Manuela amenikamata mkono anaishangaa ile copper bracelet, niligundua Catarina hakua comfortable kabisa na ata Javier aliligundua hilo hivyo alikuja kuingilia maongezi yale kwa makusudi.

Nilihisi kitu kati ya mabinti wale wawili hivyo niliamini baadae Javier atanieleza chochote kuhusu ukaribu wao. Kwani mmoja alikua na wivu sana especially huyu mwenye asili ya u tomboy hakupenda kabisa contact ya mimi na Manuela.

Niliamini amini kati yao mmoja ata kua mwanaume na mwingine mwanamke yaani wanashiriki mapenzi ya jinsia moja.

Javier baada ya kuingilia maongezi yale alianza kunipa maelekezo mengine yanayohusiana na vyombo especially yale mapipa makubwa yaliyokatwa kwa juu.

Kwenye ile meza kubwa kulikua na kitu mfano wa putty, Javier aliniambia ile haikua putty bali iliitwa coca paste au BASUCO.

Nchi nyingi za South America wanaivuta paste kama ilivyo bila hata kui process mpaka kufikia kua powder. Hii sasa ndio inaitwa cocaine crack, inavutwa sana maeneo ya temeke (mtongani mpaka kwa azizi ali). Wale wapiga deba wanaitumia sana ni cheap likija swala la gharama ukilinganisha na cocaine hydrochloride.

Huko united states uvutaji wa coca paste haupo kwa kiasi kikubwa wengi hawatumii kabisa hii coca paste kama ilivyo kwa America ya kusini na Africa.


MNAWEZA KWENDA WHATSAPP 0623329512 KWA PDF NA USOMAJI WA HARAKA
 
Kuna story nyingi.. mim binafsi sio mtu wa kufatilia story nyingi humu ila kwa chache nilizopitia nimegundua kuna aina mbili za uandishi

1- Uandishi wa kutumia Akili
2- Uandishi wa kutumia mihemko (Vibes)

Mara nyingi uandishi wa kutumia Akili unavutia sana, na aina hii ya uandishi ni mfno wa hii story hapa.

Kuna mambo mengi yanaguswa ya kitaalamu ambayo kwa mwandishi (Kilaza) si rahisi kufit in.

Nafatilia story.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…