Ni kama fatemeh hakunisikia kauli yangu ile ya kwamba nitamsubiri aje tulale kwani alionekana kuipuuzia kabisa. Hakujishughulisha na mimi kabisa zaidi aliendelea na mambo yake ambayo toka nafika hapo sikuyaelewa kabisa.
Mpaka hapo niliona kama maisha yangu yamebadilika kidogo japo sio sana, nilianza kuona dalili ya kurudi tena home na kuendelea na hustling za maisha.
Sikumbuki ni kwenye mazingira gani nilipitiwa na usingizi lakini nakumbuka niliamshwa na fatemeh majira ya saa 7 usiku. Wakati naamka nilikua nimefunikwa na blanket kubwa sana na hapo niliamini aliyenifunika hakua mwingine bali ni fatemeh.
Huyu binti kuna namna alikua na upendo ila hakua tayari kunionyesha moja kwa moja alihisi kuna mambo hayatakua sawa.
Baada ya kuamka nilisogelea dirisha na kisha kuuangalia mji wa Lima ulionekana kuchangamka zaidi kwa majira yale ya saa 7 za usiku. Sikutaka kuamini kabisa kwamba fatemeh hakulala kabisa, Kwan hakuonekana na dalili ya kulala muda wote alikua active.
Wakati mimi naamka fatemeh alionekana alikua amemaliza ku pack mizigo yake ambayo haikua mingi zaidi ya begi dogo alilotumia kubeba tarakirishi (computer) yake.
Hapo aliniambia kama kuna maandalizi nahitaji kuyafanya niyafanye kwani tuna safari ndefu ambayo itatuchukua masaa kadhaa kuanzia muda huo.
Kwa Upande wa fatemeh alishajiandaa tayari kwani alikua kwenye dressing code ile ile niliyoiona jana yake. Alikua na koti refuu lililofunika miguu na suruali yake ( roo poosh) bila kusahau head scarf (roo-sari).
hakika alikua kwenye muonekano wake ambao ungemuona tu ungejua alikua ni mwanamke mwenye asili kama sio turkey basi Persian.
Kuna muda nilitamani kujua fatemeh historia yake ya maisha hapo kabla yaani kuanzia makuzi yake ya utoto mpaka anafikia hapo. Nilitamani kujua yote hayo kwakua alikua wa tofauti sana kwa kadili nilivyokua nae karibu niliendelea kuona tabia nyingi za tofauti sana.
Nilijikuta nimekumbuka maneno ya aparecida kwamba alilelewa na kukulia kwenye kituo kilichoitwa nursery imam Ali Huko Tehran apa nilitamani yeye mwenyewe ndio anipe history yake.
Sikutaka kuamini moja kwa moja maneno ya aparecida kuhusu kulelewa kwenye kituoa cha watoto yatima huko Tehran yaani nursery imam Ali. Sababu ya kutokuamini taarifa hiyo ni kwa sababu tu bado taarifa nyingi zilizomuhusu fatemeh zilikua very controversial.
Lakini pia nilikumbuka ile kauli ya kwamba kuna kitu aliwa ahidi wazazi wake, sasa kama alilelewa kwenye orphanage ( kituo cha yatima) hao wazazi wake aliwaahidi nini na akiwa kwenye umri gani?.
Anyways mpaka muda huo kwa kiasi Fulani nilivutiwa sana na maisha ya fatemeh ambae hapo awali nilimtambua kwa jina la Manuela.
Alikua binti mmoja cool sana lakini pia makini sana kwenye kila jambo analolifanya cha mwisho na kikubwa alikua anajua mambo mengi sana.
Fatemeh alinistua na kunirushia koti kubwa la ngozi hapo nilijua aliona jinsi nilivyokua napata shida na baridi la mji huo. Nilivaa koti lile na kisha kumwambia kama nilikua tayari kwa safari kwani sikua na chochote kingine cha kubeba.
Haikutuchukua muda mrefu kuelekea kwenye rifti kisha kushuka flow ya chini ambako tulitoka nje na kukutana gari iliyofanana na jeep. Ilikua na rangi kaki ambayo haikuiva sana na ndani yake kulikua na kijana alivalia t-shirt ya jeshi ni wazi alikua hapo kutusubiri sisi.
Bwana yule alitufuata ili kutupa escort ya kuelekea sehemu moja ambayo ilikua na uwanja wa ndege uliomilikiwa na jeshi.
Uwanja huo uliitwa Las Palmas Air force base, ambao ulipatikana ndani eneo lililoitwa Santiago de Surco ndani ya mji huo huo wa Lima.
Uwanja huu ulikua mbali kidogo na kutoka ulipo uwanja wa ndege wa kimataifa wa peru ulioitwa Jorge Chavez International airport. Lakini kutoka pale tulipokua muda huo mpaka Jorge Chavez International airport ni umbali usiozidi kilometers 10.
Hivyo ndani ya usiku huo tuliondoka ndani ya ile hotel ya Costa del Sol Wyndham, by the way ilikua ni miongoni mwa hotel nzuri nilizowahi kuzitembelea mpaka nafikia umri huu.
Ndani ya jeep ile kulikua na askari huyo mmoja tu ambae walionekana kutokufahamiana kabisa na fatemeh. Kwa maelezo au stories zilizokua zinaendelea wakati tukiwa safarini niligundua mambo machache.
Kwanza kabisa niligundua Ndani ya mji huo wa Lima nchini Peru kilikua na Kambi kubwa ya Jeshi inayomilikiwa na marekani au kwa maneno marahisi naweza kusema ni Kambi ya marekani.
Kitu kikubwa zaidi ni kwamba kambi hiyo ndiyo military command pekee ya marekani inayopatikana America ya kusini.
Sasa kwanini hii kambi iliwekwa huku? Iliwekwa lini na inafanya misheni gani huko. Tutajua baadae ila kikubwa kambi hii inajulikana kama NAVAL MEDICAL RESEARCH UNIT SIX (NAMRU-6).
Kwakua yule jamaa askari hakua amemfahamu fatemeh hapo kabla Hivyo ndio alikua anamuelezea mambo mengi ya kijeshi ndani ya nchi hiyo. Na mimi pia nilifaidika kujua mengi kupitia story hizo japo muda wote nilikua kimya nikisikiliza tu.
Hivyo askari huyo ndiye aliyetuelezea kwa kina mambo mengi yaliyohusu kambi hiyo ya NAMRU-6 yaani NAVAL MEDICAL RESEARCH UNIT SIX.
Kwa jinsi nilivyokua naiona ile scenario ni kwamba safari yetu kuelekea Tehran tulikua tunaenda kutumia uwanja huo wa jeshi wa Las Palmas Air force base.
Sikua nimeijua sababu ya kutumia uwanja huo wa jeshi lakini nilihisi tu inawezekana jamaa wa MOIS walikua wanaepuka muingiliano ambao ungepelekea washirika wa Javier kutupata kirahisi.
Kwani ni kama Javier aliamua kuwekeza nguvu kutusaka basi lazima angeanza na msako wake kwenye viwanja vya ndege kwani njia rahisi ya kukimbia nchi hiyo ilikua ni kupitia ndege.
Na ni matumaini yangu alishajua tayari kama tulifanikiwa kupata hati za kusafiria hivyo kama tulichangamka kupata passport basi ni wazi tulikua na mipango ya kuhama nchi.
Uwepo wa Kambi ile ya wamarekani ya NAMRU-6 ilikua ni tishio pia kwa shughuli zote za nchini Peru zilizowahusisha ma agent wa Iran au MOIS.
Kwakua tunajua marekani na Iran hawana mahusiano mazuri ya kidiplomasia, uhasama wao nilishaueleza hapo mwanzoni kama walianza enzi zile za second world war.
Lakin pia ata CIA ( central intelligence agency) mara nyingi sana wanashutumiwa kuingilia mambo ya ndani ya Iran kuanzia kwenye lile tukio la mossadegh coup la mwaka 1953 hadi hivi sasa.
Wapo wanaoamini kuwa marekani kupitia CIA walikua wanashirikiana na shah wa mwisho au (emperor) aliyejulikana kwa jina la Mohammad Reza Pahlavi.
Lakini pia miaka ya hivi karibuni yaani miaka ile ya 2006 kuelekea 2007 bado central intelligence agency au CIA walihusishwa na tuhuma za kusapoti vikundi vya kigaidi ambavyo vimefanya matukio kadhaa nchini Iran rejea tukio la TONDAR au wale wa sunni wa jundallah dhidi ya Iran.
Nchi ya Iran kwa sehemu kubwa ni waislamu wale wa dhehebu la shia, sasa apa utashangaa kitu kimoja.
Sent from my ZTE T1002 using
JamiiForums mobile app