Utajiri wa Magofu ya Rapta

Utajiri wa Magofu ya Rapta

.....Haikutuchukua muda mrefu kuelekea kwenye rifti kisha kushuka flow ya chini ambako tulitoka nje na kukutana gari iliyofanana na jeep. Ilikua na rangi kaki ambayo haikuiva sana na ndani yake kulikua na kijana alivalia t-shirt ya jeshi ni wazi alikua hapo kutusubiri sisi...
rIft = lift
frow = floor

Mkuu nanogesha kidogo
 
Nchi ya Iran kwa sehemu kubwa ni waislamu wale wa dhehebu la shia, sasa apa utashangaa kitu kimoja.

Yaani inasemekana hawa jamaa wa central intelligence agency CIA kuna muda walisapoti vikundi vya kigaidi vya sunni mfano hao jundallah dhidi ya serikali ya Iran japo taarifa hizi zinapingwa vikali na CIA wenyewe.

Kutokana na migongano hii ya apa na pale baina ya Iran na marekani au baina ya CIA na MOIS hii imepelekea ata mahusiano ya nchi hizi mbili kusuasua sana na sidhani kama marekani kuna ubalozi wa Iran.

Turudi kwenye simulizi yetu sasa, hapo awali nilikua naelezea uwepo wa Kambi ile ya NAMRU-6 ambayo ni kambi pekee ya marekani kwa ukanda huu wa America ya kusini.

Uwepo wa shughuli hizi za kijeshi za mmarekani zimekua tishi pia kwa shughuli zote zilizomuhisisha Iran hivyo MOIS walikua wanajitahidi sana kuwakwepa hawa jamaa.

Na pia MOIS waliamini washirika wa javier wanaweza kuwepo miongoni mwa wale ma agent wa CIA.

Hivyo basi kwa mujibu wa fatemeh na Crew yake waliamini uwanja wa ndege wa kimataifa wa peru ulioitwa Jorge Chavez International airport haukua salama tena kwa upande wao.
Alternative ilikua ni kutumia uwanja mwingine ambao usinge ingiliwa kirahisi lakini licha ya kuingiliwa kirahisi waliamua kutumia mbinu zote ili wapate uwanja ambao isingekua rahisi kuamini kama ungeweza kutumika na mois hivyo option ilikua ni Las Palmas Air force base.

Alternative A ilikua ni uwanja ulioitwa Cusco airport au jina jingine huitwa Alejandro Velasco Astete international airport. Lakini baadae wakajua pia kwamba system za kiwanja hiki pia zilikua tayari zimedukuliwa na CIA kuanzia mfumo wa kamera na system yote ya ulinzi kuzunguka hapo.

Hivyo baada ya kuona system za Cusco zimekua conquered ndio wakaenda alternative B ambayo ni las Palmas Air force base. Nani alitoa msaada huo mpaka wakakubaliwa au wakapewa kibali cha siri kutumia uwanja huo, hayo ndio yalikua majukumu ya fatemeh.

Mtaalam wa MOIS aliyekua bize kufuatilia au kujua ni kwa namna gani mifumo ya viwanja hivi iko salama au hapana alikua ni fatemeh,na hicho ndicho kilikua kimemuweka macho usiku kucha.

Baada ya uwa nimejua kwamba fatemeh usiku ule alikua bize kwa ajili kuchungulia mifumo ya viwanja vya ndege lakini pia kujua kama kuna mikono ya CIA kwenye viwanja hivyo nilijikuta najuta kwa jinsi nilivyokua namsumbua.

Kwa namna moja ama nyingine niliamini huyu binti ana level za juu za busara kwani hakuonyesha kabisa kama alikua na majukumu makubwa kiasi hicho.

Licha ya sababu hizo za kiusalama zilizowakwamisha MOIS lakin pia uwanja wa Cusco airport haukua rafiki kwenye hali ya hewa kwa wakati huo na kingine kulikua na kitu kilichoitwa visibility restrictions yaani shughuli zote zilifanyika mchana tu Kwani usiku ingekua ngumu kwa marubani kufanya landing.

Kwa utashi wa fatemeh aligundua sehemu Salama ni Las Palmas Air force base peke ake na ndio sehemu tuliyokua tunaelekea.

Ukimuangalia fatemeh kwa haraka unaweza kumchukulia poa sana Kwan alikua bado Binti mdogo sana kiumri Lakini kimajukumu alikua amekomaa.

Kwa bahati mbaya mpaka muda huo sikuweza kufahamu nafasi yake kwenye idara hiyo aliyokuwa akiitumikia.

Lakini kitu kingine yeye mwenyewe hakua amenieleza chochote kuhusu kuhudumu kwenye idara hiyo.

Baada ya masaa takribani mawili tulifika Las Palmas, kama lisaa limoja nyuma mpaka tunafika hapo fatemeh alikua bize kwenye maongezi ambayo lugha haikueleweka nadhani ilikua ni lugha za kiajemi kwao huko.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Wakati wote tukiwa safarini fatemeh mara nyingi alikua bize kuongea au kufanya mawasiliano na mtu ambaye hatukumjua lakini pia alitumia lugha ambayo ata yule dereva alionekana kutokuijua.

Kuna muda nilijaribu kuchungulia kwenye tarakirishi mpakato yake (laptop) lakini sikuambulia kitu chochote zaidi ya kuona namba namba nyingi zikishuka na kupanda.

Nyingine zikipungua na kuongezeka hivyo sikuelewa Chochote na nilimshangaa sana kwani kwa upande wake ni dhahiri alikua anajua ni nini anafanya.

Kwa wakati ule mfupi niligundua fatemeh alikua na uwezo mkubwa sana kwenye matumizi yote yaliyohusu computer.

Tuliingia ndani ya uwanja ule usiku huo, mandhari ya uwanja ilinivutia lakini pia kuniogopesha kwa namna nyingine.

Kikubwa kilichoniogopesha ni namna ulinzi ulivyoimarishwa uwanjani hapo. Lakini pia kilichonifurahisha ni mazingira kwa ujumla kwani kulikua na tambalale iliyochukua hekari nyingi sana.

Ukiacha tambalale hiyo uwanja ulizungukwa na milima mikubwa na mirefu ambayo kwa usiku ule niligundua milima hiyo kutokana na taa zilizokua zikiwaka nje ya uwanja kutoka kwenye majumba ya milima hiyo.

Ilionekana wazi kuwa maafisa waliokuwa on duty siku hiyo tayari walishapewa taarifa za fatemeh kwani kila mmoja alimkaribisha kwa namna ya kama walikua na taarifa zake.

Tulipokelewa na bwana mmoja ambae alitupeleka mpaka kwenye chumba ambacho fatemeh pekee ndie aliyeruhusiwa kuingia ndani na mimi niliambiwa naweza kumsubiri nje ya ofisi hiyo.

Nje ya ofisi ile kulikua na viti pamoja na meza vilivyopangwa kama kulikua na mkutano uliokua ukiendelea eneo hilo.

Nilikaa hapo kwa zaidi ya dakika 20 (ishirini) nikimsubiri fatemeh amalize maongezi yake ndani ya ofisi ile. Lakini kabla fatemeh hajatoka alipita bwana mmoja aliyevalia sare zilizofanana na marubani na kuingia ndani ya ofisi ile ile.

Bwana yule alikua tofauti kabisa na askari waliokuwepo pale kwenye uwanja ule wa Las Palmas Peruvian Air Force Base. Huku wenzetu hawana utamaduni wa kusalimia hovyohovyo, yaani mtu anakupita tu na wala hajistukii ata kidogo.

Jambo hilo nilishuhudia mara kadhaa kwenye miji tofauti tofauti na mwisho kabisa nilikuja kulithibitisha nilipofika kambini hapo.

Nikiwa uwanjani pale nilijiuliza inawezekana vipi mimi na fatemeh tukiwa raia kabisa kutumia uwanja huo ambao unaonekana kua ulikua ukimilikiwa na jeshi.

Swali hilo nililitunza nikimsubiri fatemeh aje ili nipate kumuuliza, nikiwa naendelea kushangaa shangaa na kujiuliza maswali mengi kichwani walitoka watu watatu wote kutoka kwenye ofisi ile.

Alitoka fatemeh, yule bwana rubani aliyeingia kwa mara ya mwisho na kisha akafuatia bwana mmoja aliyechafuka sana vyeo. Bilashaka bwana yule ndio alikua mkuu aliyekua akisimamia kambi hiyo kwa wakati huo.

Fatemeh alinipa ishara ikitaka niwafuate kule wanapoelekea, kiukweli sikuweza kufahamu kabisa kule ndani walipokua wanafanya maongezi yao waliongea kitu gani.

Niliwafuata bila kuchelewa na tulivuka mlango mmoja mkubwa wa kioo uliokua au uliotumika kuingilia au kutokea runway.

Mita chache sana kutoka ule mlango ulipofunguliwa mbele yetu kulikua na ndege kubwa ya wastani ambayo ilikua tofauti na ndege zote za eneo hilo. Ndege nyingi za eneo hilo zilikua ni military planes (ndege za kijeshi) wakati ndege iliyokua mbele yetu ilikua ni civilian plane ( ndege ya kiraia).

Ni wazi ndege ile ilikua pale ikitusubiri mimi na fatemeh (Manuela) tukifika ndio tuendelee na safari. Nikiongozwa na fatemeh tuliingia ndani ya ndege hiyo.

Lakini ndani ya ndege ile nilijua tutakua wawili tu ila nilishangaa baada ya kukuta watu waliokaribia kumi na sita (16). Watu hawa walikua bize na serious sana, fatemeh alisogea mpaka kwenye siti ambayo nadhani ndio iliandaliwa kwa ajili yetu.

Wakati Tunaingia ndani ya ndege ile wengi walikua bize ila wachache sana ni kama walishtushwa na uwepo wangu eneo lile. Yule bwana alievalia kama rubani aliongoza moja kwa moja mpaka cockpit au cabin kama wengine wanavyoita.

Kwa wasiojua cockpit ni kile chumba anachokaa rubani kwa ajili ya kuendesha ndege mara nyingi huwa na siti mbili yaani rubani mkuu na msaidizi wake.

Nikiwa nimekaa na fatemeh nilikua na maswali mengi kichwani lakini kilichonikera zaidi ni kwamba fatemeh hakua akipenda kuulizwa maswali mara kwa mara.

Yaani ikitokea utamuuliza maswali matano au matatu atajibu moja tu au asijibu kabisa akaishia kukuaangalia tu.

Nilimuuliza swali moja tu wakati huu, ilikuaje kwenye ule uwanja wa ndege wa jeshi ikapaki ndege ya kiraia?

Kwa mujibu wa fatemeh ni kwamba sio kweli eti ndege za kiraia haziwezi kutua kwenye viwanja vya jeshi, mara nyingi tu ndege hizi hutua lakini kama kutakua na emergency ambazo hazitaweza kuathiri hali ya usalama wa uwanja.

Lakini pia aliniambia ndege ile tuliyopanda haikua ya kiraia kama nilivyofikiria na yenyewe ilikua ni ya jeshi, na alinidokeza ata wale abiria mule ndani wote walikua ni makomando wa Iran wakiongozwa na rubani kule kwenye cockpit.

Sasa kuanzia muda huo tulianza safari ya kuitafuta Tehran, mji wa Tehran unapatikana north-central ndani ya nchi ya Iran pembezoni mwa milima maarufu kama Elburz.

Kwa wageni wakifika mji huu ni dhahiri wataona maisha magumu kutokana na kuwepo kwa baadhi ya sheria kali kama tunavyoona kwa nchi ile ya north Korea.

Huu ni mji wa kiislamu au kwa lugha rahisi niseme umetawaliwa na sheria nyingi za kiislamu, utaligundua hilo ukifika tu kwa kuuona muonekano wa wanawake. Kwani wakina mama wa Iran wanatakiwa kuwa wamejistili muda wote katika muonekano wa kiislamu.

Mitandao kama TikTok, telegram au YouTube mara nyingi hufungiwa ikiaminika kutumika kama siraha ya kupolomosha maadili kwa vijana wao ambao ndio wanakua na kutegemewa na taifa hilo.

0623329512 Whatsapp

Leo tumeanza kupata majibu taratibu ya kwanini Manuela haonekani tena kuwa na arosto kama alivyokua haullaga, hivyo mpaka kesho tutakua na majibu kamili yanayomuhusu Manuela au fatemeh kama ni junkie ( mtumiaji wa unga).

Kuhusu Gatkuoth nadhani wote mnakumbuka alikua teja kabisa na si unajua teja hapewi dhamana popote pale yaani teja hajawahi kuaminika popote pale.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
Mi sijaona wapi umeeleza kwanini hana alosto tena
 
...
JamiiForums790734876.jpg
 
Mi sijaona wapi umeeleza kwanini hana alosto tena
Episode 15C kuna tukio lilitokea, hilo tukio litatupa picha mpya ya maisha ya fatemeh kwenye episode 16B.
leo tulikua episode 16A hivyo kesho kuna nondo moja ya msingi sana tena especially wale wenye watoto wanaokua.

Hivyo kesho mapema tukijaaliwa tutajua kwann fatemeh hana arosto tena,

Kama kuna mpenzi wa rap kwenye huu uzi basi leo alale ameiskiliza ngoma moja inaitwa

moment of truth _ guru

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Episode 15C kuna tukio lilitokea, hilo tukio litatupa picha mpya ya maisha ya fatemeh kwenye episode 16B.
leo tulikua episode 16A hivyo kesho kuna nondo moja ya msingi sana tena especially wale wenye watoto wanaokua.

Hivyo kesho mapema tukijaaliwa tutajua kwann fatemeh hana arosto tena,

Kama kuna mpenzi wa rap kwenye huu uzi basi leo alale ameiskiliza ngoma moja inaitwa

moment of truth _ guru

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
Hapa hapa mpaka kieleweke meku, hatoki mtuuuuu
 
Back
Top Bottom